21 Jul 2020 in Senate:
Madam Temporary Speaker, Standing Order No. 221(4) says- “If the Committee accedes to the Statutory Instruments, the Clerk of the Senate shall convey the message to the relevant authority.” If the Committee does not accede, the Committee may recommend annulment of the instrument to the Senate. If the Committee fails to avail agree, the instrument shall stand approved.” I am entirely in the hands of the Senate. If you guide us to make a Statement, we shall make a formal report with regard to these Regulations. However, our Standing Orders say that it is only when we annul that we ...
view
21 Jul 2020 in Senate:
Thank you, Madam Temporary Speaker. I want to echo what Sen. Wetangula and Sen. Mutula Kilonzo Jnr., have said with regard to Petitions. On Statements, I made that Statement in the month of May concerning the shooting of a Kenyan aircraft in Somalia. Up to now, nothing has been done about that Statement. According to the International Air Transport Association (IATA) Regulations, there is supposed to be an interim report within 30 days after the incident. That report has not been issued. Although it has been signed by the Kenyan Government and the investigator, the Somali Government has refused to ...
view
26 Jun 2020 in Senate:
Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ripoti hii. Kwanza kabisa, nawapongeza wawakilishi wa bunge ya Kaunti ya Kirinyaga kwa ujasiri wao wa kuleta mashtaka hapa Seneti pamoja na walivyoendesha mashtaka mbele ya Kamati Maalum iliyokuwa inashughulikia swala hilo. Wawakilishi wa Bunge la Kaunti ya Kirinyaga walionyesha kwamba nia yao haikuwa tu kumwondoa Gavana bali wanataka kuona marekebisho fulani katika kaunti yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
26 Jun 2020 in Senate:
Naipongeza Kamati Maalum iliyoongozwa na naibu mkuu wa wachache katika Bunge la Seneti, Mhe. Malalah na naibu mwenyekiti wake, Sen. Halake. Nawapongeza Maseneta wengine pia waliohudumu katika kamati ile wakiwemo, Sen. Madzayo, Sen. Mugo, Sen. Mwangi na wengineo wote walioendesha kazi ile kwa tajiriba kubwa kabisa. Kamati ile ilijitolea na kuhakikisha kwamba imekamilisha ripoti yake kwa muda uliowekwa. Nampongeza Gavana Waiguru kwa kujitetea mbele ya Kamati. Pia, tuliona umuhimu wa familia katika maswala kama haya. Wakili Kamotho Waiganjo alichukua mambo mikononi mwake ili kuhakikisha kwamba ndoa yake haiwezi kusambaratika kwa kumtetea mke wake, Gavana Waiguru, asing’atuliwe mamlaka ya ugavana.
view
26 Jun 2020 in Senate:
Masomo ambayo tunasoma hapa ni kwamba si makosa yote yanaweza kusababisha gavana kuachishwa kazi. Ni kama vile si makosa yote yanaweza kusababisha kuwe na talaka. Ni jukumu letu kama Seneti kukubalina na mapendekezo ya Kamati hii. Ninaomba Kamati ya Ugatuzi itekeleze mapendekezo ya Kamati hii. Vilevile Kamati ya Uhasibu yaani County Public Accounts and Investments
view
26 Jun 2020 in Senate:
(CPAIC) iangalie ni mapendekezo yapi inaweza kuchukua kutoka Ripoti hii ili kuhakikisha kwamba Bunge za Kaunti zimetiliwa nguvu ili wakifanya kazi yao ya uhasibu na uchunguzi wa serikali za kaunti tuhakikishe kwamba wanafanya mambo sawa sawa.
view
26 Jun 2020 in Senate:
Wakati huu ni msimu wa kuwafurusha magavana. Ni wajibu wetu kama Seneti kuhakiksiha kwamba hatuathiriwi na mambo yanayozungumzwa nje ya Bunge. Tuangalie ushahidi ambao utaletwa mbele yetu au mbele ya Kamati kuhakikisha kwamba tunatenda haki katika maswala kama haya.
view
24 Jun 2020 in Senate:
Asante, Bi Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Arifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherargei. Maswala ya rasilimali za nchi na maeneo ambayo zipo ni swala nyeti sana katika nchi yetu. Tumeona kwamba rasilimali nyingi ambazo ziko katika nchi hazifaidi watu wetu ambao wako katika maeneo yale ambayo zinatoka.
view
24 Jun 2020 in Senate:
Tumezungumziwa mambo ya Nandi, Migori, Kakamega, ambako kuna madini lakini watu wetu hawafaidiki. Hivi majuzi Kaunti ya Turkana kulipatikana mafuta ya petroli lakini rasilimali hiyo haiwafaidi Waturkana na Wakenya wote kwa jumla. Kule kwetu Pwani, rasilimali kubwa tuliyopewa na Mungu ni bahari. Watu wengi wanajikimu kimaisha kutokana na bahari. Bandari ya Mombasa haijafaidi Wapwani kisawasawa tulivyotarajia. Hivi majuzi, tulileta Arifa hapa Bungeni kulalamikia utendakazi inayohamisha bandari kutoka Pwani kuipeleka kule Naivasha. Hili ni swala linahusiana na rasilimali za maeneo ambazo mpaka sasa hazifaidi wale ambao wanakaa maeneo yale.
view
24 Jun 2020 in Senate:
Bi. Naibu Spika, nilitarajia kwamba wakati tulipata serikali za ugatuzi, serikali hizi zingekuwa mbele katika kuhakikisha ya kwamba leseni ambazo zinapewa wale wanaokuja kutafuta madini yale, zitapewa nafasi ya kwanza wananchi wanaokaa katika maeneo yale lakini yote yamekuwa ni ndoto kwa sababu wengi wanaopata leseni hizi huzipatia hapa Nairobi na wakienda katika kaunti zetu, wengi wao huwa wa shirika au wandani wa magavana na wakubwa wengine katika kaunti zile hivyo rasilimali zinakwenda kwa wachache wengi wakiendelea kudhalilika na kupata shida.
view