Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1401 to 1410 of 2123.

  • 16 Feb 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kumuomboleza marehemu Sen. Mohammed Yusuf Haji, ambaye alikuwa Seneta wa Kaunti ya Garissa. Ninampongeza Sen. Orengo kwa kuleta Mswada huu wa kumkumbuka mwendazake Sen. Haji, kwa mchango mkubwa aliyofanya katika Taifa hili. Kwanza akiwa kama afisa wa Serikali ambapo alifanya kazi kama Mkuu wa Wilaya, kisha The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Feb 2021 in Senate: baadaye akawa Mkuu wa Mkoa. Ninakumbuka alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo makao makuu yalikuwa Mji wa Mombasa. Sen. Haji alikuwa mnyenyekevu sana. Ungemwona katika shughuli zake, hungedhani alikuwa mtu mwenye mamlaka makubwa na kwamba alikuwa amefanya kazi kubwa katika Serikali ya Kenya. Binafsi, niliwahi kuswali naye Swala ya Alfajiri katika msikiti karibu na nyumbani kwake, Westlands. Alikuwa anakuja msikitini alfajiri peke yake hata bila mlinzi. Inamaanisha kwamba hakuwa na hofu kwa lolote ambalo lingemfika huku akiwa na umri wa karibu miaka 80. Hakuwa na uoga kwamba jambo lolote lingempata wakati huo wa alfajiri. Bw. Spiaka wa Muda, pia ... view
  • 9 Feb 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono uteuzi wa Kamati ya Kuongoza Ratiba ya Seneti. Kwanza, ningependa kukupa mkono wa tahania. Tuko tayari kuendelea kufanya kazi kuhakikisha kwamba Miswada yote ambayo inakuja katika Bunge hili inachunguzwa na kupitishwa kama inavyohitajika kisheria. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 9 Feb 2021 in Senate: Mwaka uliopita, tulipita milestone kubwa wakati Spika wa Muda, Sen. (Dr.) Mwaura, aliendesha ratiba ya Bunge kwa lugha ya Kiswahili, lugha ya kitaifa. Ni matumaini yetu kwamba, katika mwaka huu, tutakuwa na fursa kama hiyo kuhakikisha kwamba tunakuza lugha ya Kiswahili ili wengi wanaosikiza mijadala katika Bunge hili wapate kujua ni mambo gani yanajadiliwa. view
  • 9 Feb 2021 in Senate: Bw. Spika, kwa Muhula ambao tuko na mambo ya mabadiliko ya Katiba itakayokuja, itakuwa ni muhimu kufanya kazi kwa bidi ili kuhakikisha kwamba Bunge hili halitapata vipindi ambavyo hatuna mijadala ya kuendeleza katika Bunge hili. view
  • 9 Feb 2021 in Senate: Asante. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Asante Sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa kuzuia madawa ya kutitimua misuli katika michezo. Kwanza, kabisa, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia ya mchezaji wetu mmoja kwa jina maarufu Ali Kajo, ambaye alifariki jana Mombasa. Marehemu Ali Kajo ni mojawapo aliyecheza na marehemu Joe Kandenge, James Yanga, Farah Ahmed na wengineo ambao waliletea nchi hii sifa nyingi katika miaka ya 1960. Marehemu Ali Kajo na wenzake walishinda Gossage Cup mwaka wa 1965 na kuiweka nchi yetu ya Kenya katika zile nchi ambazo zilikuwa zimebobea kwa kandanda. Nachukua fursa hii kutuma rambi rambi zangu kwa familia, ... view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika, kwanza kabisa, sheria inapendekeza kujumuisha federation za nchi na vile vile za kimataifa katika utekelezaji wa masuala ya anti-doping. Pili, katika Kifungu cha tano, wanapendekeza kuleta elimu ya masuala ya madawa katika risala za kufundihsa wanamichezo ili wajue dawa fulani zikitumika mtu atakuwa amevunja sheria. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Vilevile katika Kifungu cha tisa, World Anti-Doping Agency (WADA) itakuwa taasisi huru katika nchi ambayo haitaegemea upande wowote kwa Serikali ama kwa shirika lolote la michezo katika kutekeleza jukumu lake. Hii ni muhimu kwa sababu bara nyingine itakuwa inalemea upande mmoja na federation fulani. Ina maana kwamba hawataweza kutoa uamuzi huru katika masuala muhimu kama haya. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Katika Kifungu cha 31, Sports Tribunal ama jopo la kusimamia masuala ya kesi za michezo limepewa uwezo wa kuangalia na kusikiliza kesi ambazo zinahusiana na ukiukaji wa sheria hii ya anti-doping . Hii ni muhimu kwa sababu masuala kama haya mara nyngine inabidi yapelekwe katika taasisi za kimataifa kama vile Court ofArbitration for Sport (CAS) Louisiana, Ufaransa, ambayo ni ghali. Vilevile sisi kama Wakenya hatuna uwezo wa kuchukua mawakili kwenda kusikiliza kesi kama hizo. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus