Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1381 to 1390 of 2123.

  • 13 Apr 2021 in Senate: Bw. Spika, tajiriba yake inajulikana na hakuna haja ya kuikariri hapa. Mtume wetu Suleiman anasema kwamba mtu anapoondoka duniani huwa amali yake imekwisha isipokuwa mambo matatu. Kwanza, ni Sadaqah Jariyah yaani sadaka ambazo ametoa mbeleni ambazo zitamsaidia. Pili ni mtoto mwema ambaye atafanya mambo mazuri na tatu ni kama aliweza kujenga shule ama kuwasomesha watoto ambao wataweza kumuombea dua. view
  • 13 Apr 2021 in Senate: Bw. Spika, marehemu Sen. Haji aliweza kutekeleza mambo hayo yote matatu. Mtoto wake Sen. Haji Abdulkadir Mohamed wakati kulipokuwa na shambulizi la kigaidi aliweza kuwatetea watu ambao hawajua kabisa. Na hiyo ni ishara kwamba ni mtoto mwema. Kwa hiyo, ninamtakia kila la kheri katika jukumu lake jipya kama Seneta wa Kaunti ya Garissa. view
  • 13 Apr 2021 in Senate: Jambo la mwisho ni kumshauri kuwa marehemu Sen. Haji alikuwa na jukumu la kitaifa. Aliweza kuhudumu Serikalini katika nyanja mbalimbali na alitegemewa na wengi kusimamia maswala mazito ya usalama katika Seneti. Hata alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Pili katika Kamati ya BBI ilikuwa ni jukumu lake kubwa sana. Hii iliiona kama nafasi ya kuwaunganisha Wakenya. Unapochukua majukumu yako ndugu Sen. Haji Abdulkadir Mohamed ni lazima ufuatilie kwa makini na ufuate nyayo za mzee kuhakikisha malengo aliyoyasimamia hayawezi kutofautiana na malengo yako binafsi. view
  • 13 Apr 2021 in Senate: Mwisho, kuna baadhi wameanza Ramadan leo na wengine wataanza kesho. Nachukua fursa hii kuwatakia Ramadan Mubarak. Ndugu yangu ameapishwa wakati tunaanza mwezi mtukufu wa Ramadan leo, hii ni heshima kwetu sote. view
  • 13 Apr 2021 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa ugawaji wa rasilimali katika Muhula wa 2020/2021. Kwanza, ningependa kujiunga na wenzangu ambao wamezungumzwa kabla yangu wakichangia Mswada huu. Ninaunga mkono Mswada huu. Donda sugu ambalo liko katika nchi yetu hivi sasa ni ufisadi. Ufisadi umetanda katika kila sehemu ya Serikali, iwe ni serikali za ugatuzi au Serikali Kuu. Hii ilidhibitishwa na Rais Uhuru Kenyatta hivi majuzi aliposema kwamba kwa siku moja, Kshs1 billioni zinapotea kwa sababu ya ufisadi. Kwa hivyo, Sisi kama Seneti, katika jukumu letu la kuchunguza na kuangalia Serikali, inafaa tufanye mambo zaidi kuliko tunavyofanya ... view
  • 13 Apr 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 13 Apr 2021 in Senate: Iwapo usafiri utacheleweshwa, mashirika ya meli yataweka delay surcharge kwa Bandari ya Mombasa. Hii yote imesabaishwa na Serikali kutohusisha wananchi katika zile miradi wanapanga kufanya. Asante. view
  • 24 Mar 2021 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja hii ya kubadilisha ratiba ya vikao vya Seneti. Ni kweli ugonjwa wa korona umerudi kwa raundi ya tatu kwa vishindo. Raundi hii ni hatari zaidi kuliko raundi zile mbili zilizo tangulia. Wakati ugonjwa huu ulipozuka, Bunge la Seneti lilichagua Kamati ya COVID-19. Kamati ilifanya kazi nzuri sana. Ilikuwa inatoa mwelekeo kila wiki kuhusu kazi yao na vikao vyake na taasi nyingine za Serikali. Bw. Spika, kutoka muhula wa Kamati hiyo kuisha, hakujakuwa na mwongozo wowote katika Bunge hili kuhusiana na masuala ya COVID-19. Ni aibu kwamba mpaka sasa kutoka ... view
  • 24 Mar 2021 in Senate: Bw. Spika, tutakapobadilisha ratiba hii ya vikao, nina hakika kwamba tutachukua fursa hiyo, Jumatano na Alhamisi kuona ya kwamba Kamati zinazohusika zinafanya kazi kama ilivyokuwa imepangwa awali. view
  • 2 Mar 2021 in Senate: Asante Bw. Spika. Nasimama kuambatana na Aya ya 48(1) ya Kanuni za Kudumu kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Barabara na Uchukuzi kuhusu uboreshaji wa barabara ya Mshomoroni-Mwakirunge kufikia hali ya barabara ya lami. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus