Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1361 to 1370 of 1994.

  • 3 Nov 2020 in Senate: Mwisho, sisi kama Seneti lazima tuwe macho wakati huu wa BBI ili kuhakikisha yote ambayo tumeweza kuyapata yanaendelea kuimarika na kuimarisha Seneti kwa maana ni taasisi pekee ambayo inaweza kulinda ugatuzi katika nchi yetu. Asante. view
  • 8 Oct 2020 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I beg to give notice of the following Motion– AWARE that the Sessional Committee on Delegated Legislation is established under Standing Order 221 of the Senate Standing Orders and is charged with the responsibility of scrutinizing statutory instruments laid before the House and that pursuant to Standing Order 221 (3) (b), the Committee is mandated to consider, in respect of any statutory instrument, whether the statutory instrument “ infringes on fundamental rights and freedoms of the public”; view
  • 8 Oct 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Oct 2020 in Senate: FURTHER AWARE that on 26th May, 2020, the Senate referred the Railway City Development Authority Order, 2020 to the Sessional Committee on Delegated Legislation; AWARE that the purpose of the State Corporation proposed in the Order is to provide for the coordinated planning, management, development and use of the Nairobi Railway Central Station and the surrounding land which has been designated as a special planning area; ACKNOWLEDGING that the Regulations touch on existing land rights, particularly with regard to the Kenya Railways Corporation, Kenya Railways Pension Scheme and private land owners in the designated area; NOTING that due to the ... view
  • 8 Oct 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kifungu Nambari 48(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge la Seneti kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Barabara na Uchukuzi kuhusu hali ya Barabara ya Nairobi- Mombasa hususan maeneo ya karibu na Dongo Kundu, mjini Mombasa. Kwenye Taarifa hiyo, Kamati inafaa kuangazia yafuatayo- (1) Kueleza sababu za sehemu ya Barabara ya Dongo Kundu iliyozinduliwa takriban mwaka mmoja na nusu uliopita kukarabatiwa mara kwa mara. (2) Kufafanua chanzo cha maporomoko ya udongo yaliyo shuhudiwa kwenye barabara hiyo zaidi ya mwezi mmoja uliyopita na kusababishwa kufungwa kwa sehemu za barabara hiyo, na ... view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa Bungeni na Kamati ya Afya. Kwanza naunga mkono mapendekezo ya Kamati ya Afya kuhusiana na kifo cha mamai katika Hospitali ya M.P. Shah. Visa vya Wakenya kufariki katika hali kama hiii vinaendelea kuongezeka kutokana na ajizi ama utepetevu katika hospitali zetu na pia madaktari ambao viapo vyao hawawezi kuvitekeleza kikamilifu. Imekuwa ni biashara kubwa kufungua hospitali, lakini huduma zinazotolewa mara nyingi huwa haziridhishi. Ndugu yangu, Seneta wa Makueni, amezungumzia kifo cha Mwalimu Walibora ambaye alikuwa mwalimu wa Kiswahili mwenye tajiriba kubwa. Maisha yake ilimalizika katika chumba cha wagonjwa mahututi ... view
  • 1 Oct 2020 in Senate: Asante Sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi ambalo limeletwa Bungeni na Bw. Nashon Ogana. Kwanza namuunga Bw. Ogana na wenzake mkono kwa kuwa na imani kwamba Bunge la Seneti litasaidia kutatua ombi lao. Imani hiyo imesababishwa na kwamba sisi kama Maseneta tunayaangazia matatizo kama haya kwa njia ya haraka na kutoa suluhisho mapema kuliko taasisi zingine ambazo zimewekwa na sheria za kutatua malalamiko kama haya. view
  • 1 Oct 2020 in Senate: Swala kama hili likipelekwa mahakamani, linaweza kuchukua zaidi ya miaka kumi kabla ya suluhisho kupatikana. Kamati husika litakalo angazia ombi hili ishughulike kwa haraka ili kuwe na suluhisho kwa muda mfupi iwezekanavyo. Hii ni kwa sababu mizozo ya mipaka kama hii husababisha watu kupoteza maisha, uharibifu wa mali, wizi wa mifugo na mali zingine za wananchi wa Kenya. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa karibu miaka 60 ya Uhuru hatujaweza kutatua matatizo madogo kama ya mipaka ambayo yako kote nchini. Kuna mizozo ya mipaka kati ya Kaunti Makueni na Taita Taveta, Taita Taveta na Kwale, Taita Taveta na Kajiado, Kisumu na ... view
  • 1 Oct 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, hatuna tume ya kitaifa inayoshughulikia mizozo ya mipaka. Njia pekee ya kuweza kutatua na kusuluhisha mizozo kama hii ni kupitia kwa Bunge la Seneti. Naomba kwamba katika uelekezi wako, uhakikishe kwamba kamati husika iangalie swala hili kwa haraka na kuweza kutoa mwongozo ili matatizo kama haya yasiweze kuendelea katika sehemu zingine katika Jamhuri yetu ya Kenya. view
  • 29 Sep 2020 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati. Kwanza, ningependa kusema kwamba sisi kama Maseneta ni Waheshimiwa na lazima tuendeshe mambo yetu tukiwa na heshima. Aidha tukiwa katika Bunge ama hata tukiwa nje ya Bunge, lazima maadili yetu tuyafuate kama Waheshimiwa. Pili ni kuwa ni jambo la kupendeza kwamba hawa Maseneta wawili, Sen. Kwamboka na Sen. Seneta, wameweza kuomba msamaha na wakajutia makosa yao. Kwa hivyo, ni sisi kama Bunge kukubali Ripoti ya Kamati ili waweze kusamehewa na warudi kwa miungano yao kama kawaida. Tumechaguliwa kuhudumu kwa miaka mitano. Kwa hivyo, ikiwa tutaanza kupigana wenyewe kwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus