4 Nov 2020 in Senate:
iwasilishe ripoti yake kwa muda mfupi utakao wezekana kwa sababu ni jambo ambalo linaathiri wengi hasa watu wanaofanya kazi za bandari.
view
4 Nov 2020 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Sen. Malalah kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19. Ni masikitiko makubwa kwamba nchi yetu imeendelea kuona mkurupuko wa visa zaidi vya COVID-19 vinavyosababisha vifo. Nikizungumzia Kaunti ya Mombasa ninapotoka, ni jambo la kusikitisha kuwa karibu kila siku kwa muda wa siku 10 nimekuwa nikishuhudia visa vya watu wanaofariki ambao wengine ni watu walio karibu na mimi. Nikizungumzia wiki iliyopita, siku ya Jumamosi, diwani wa zamani wa eneo la Majengo anayeitwa Said Mathias alifariki. Bunge la Kaunti ya Mombasa limefungwa sasa kwa sababu kulipatikana visa nane vya maambukizi ya COVID-19. ...
view
4 Nov 2020 in Senate:
Bwana Spika wa Muda, hapo nyuma kidogo tuliweza kuteteleka na tukawacha kufuata yale maagiza ambayo yametolewa. Kwa mfano, tuliruhusu watu kukutana kiholela, kutembea mijini bila barakoa na kutotumia kitakasa. Hivi Sasa, hali ambayo inatokea katika maeneo ya burudani na sehemu zingine ni kuwa watu wanaendelea kusongamana kwa wingi bila kuchukua tahadhari zozote. Ni masikitiko kwamba hali imekuwa hivi na hatuwezi kuendelea kulalamika kuhusu hali hii bila ya kuchukua hatua mwafaka. Bw. Spika wa Muda, nimefurahi kwamba leo Rais ameweza kurejesha amri ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri. Lakini hiyo haitoshi. Hii kwa sababu bila ya ...
view
3 Nov 2020 in Senate:
Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyosomwa na Mhe. Spika. Kwanza niruhusu niwape kongole Spika pamoja na Seneti nzima kwa uamuzi wao wa kwenda mahakamani kutetea haki ya kikatiba ya Seneti. Vilevile nawapa kongole mawakili wote ambao walihusika katika kesi hii tukiongozwa na Mhe. Orengo, Mhe. Omogeni, Mhe. Sen. Mutula Kilonzo Jnr. na wale wengine wote ambao tulikuwa nyuma tukitoa mawazo na usaidizi wa aina nyingine. Nilikuwa na Sen. Omogeni wakati kesi ilipokuwa inazungumzwa. Kwa hakika alizungumza kwa ujasiri mkubwa akisaidiana na wakili Bi. Mercy Thanji ambaye yuko katika Idara ya Sheria katika Bunge letu la ...
view
3 Nov 2020 in Senate:
Wakati huu ambapo tunapongeza Mahakama kuna Majaji 40 ambao wamechaguliwa na Tume ya Kuajiri Mahakimu ambao Mhe. Rais amekataa kuwatangaza rasmi na kuwaapisha kama Majaji. Kitendo hicho kinahujumu Katiba kwasababu JudicialService Commission (JSC) ikipendekeza Majaji waajiriwe, inapendekeza kwasababu imewafanyia ukaguzi na kila kinachotakiwa kufanywa kuhakikisha kwamba wale Majaji wameweza kuchaguliwa. Hatuwezi kupigania uhuru wa Seneti au Seneti iweze kupata nguvu zaidi wakati mahakama inaendelea kuhujumiwa na Rais.
view
3 Nov 2020 in Senate:
Kamati ya Haki, Maswala ya Sheria na Haki za Kibinadamu ya Seneti iliweza kumuita nafikiri Mwanasheria Mkuu kuja kuzungumzia swala hilo, na mpaka sasa hatujaweza kupata utatuzi kuhusiana na suala la kuajiriwa kwa Majaji 41.
view
3 Nov 2020 in Senate:
Majuzi tu mmoja wa Majaji ambao walikuwa wamependekezwa alifariki dunia, na hivyo ndivyo ndoto yake ya kuwa Jaji katika Mahakama Kuu ya Kenya ilididimia. Tunapozungumzia taasisi za kikatiba ni lazima tuhakiskishe kwamba taasisi hizo zinafanya kazi kulingana na sheria. Hatuwezi kuwa na taasisi ambazo hazina mamlaka kikatiba na vilevile tunategemea kwamba zinaweza kufanya kazi vile wananchi wanavyotaka.
view
3 Nov 2020 in Senate:
Tunapozungumzia BBI, lazima uwezo wa Seneti kujadili maswala ya ugavi wa rasilmali uendelee kuwepo. Vilevile, Seneti ipewe nafasi ya kukagua nafasi zote za ajira The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
3 Nov 2020 in Senate:
katika Serikali ili kuhakikisha kuna usawa na Checks and balances katika Katiba yetu ambayo tumeitumia kutoka mwaka 2010.
view