11 Nov 2020 in Senate:
Kwa mfano, Ofisi ya Rais itakuwa na fursa ya kuchagua Waziri Mkuu na kumfuta wakati wowote wanapotaka. Hizo ni nguvu zaidi ambazo zitaongezwa kwa Ofisi hiyo kuliko vile ilivyo sasa kwa sababu hakuna nafasi ya Waziri Mkuu kwenye Katiba. Sisi katika Seneti lazima tuangalie mapungufu tuliyonayo na jinsi tutaongeza nguvu zetu ili Seneti itakayofuata iwe na nguvu na mamlaka zaidi ya kutekeleza kazi yake ya kutetea ugazuti katika nchi yetu ya Kenya. Wanapendekeza kuongeza Maseneta wengine 47 wa jinsia ya pili. Sio kwamba tunaongezewa nguvu; ni kupewa idadi ya watu ambayo haitasaidia popote katika kutetea ugatuzi katika nchi yetu. Kwa ...
view
11 Nov 2020 in Senate:
Bi. Naibu Spika, kwa kumalizia, wabunge waliochaguliwa hapo mbeleni kwa viti tofauti katika Bunge wamefanya kazi kubwa kupeleka mbele miswada inayo husu akina mama kuliko wale tunao sasa. Huo ndio mjadala tunataka kuangalia. Ni njia gani tutatumia kusukuma mbele mjadala wa akina mama, ili haki zao na za watoto wetu wa kike zilindwe? Vili vile, pia bibi zetu wapate haki sawa katika Katiba yetu. Mjadala si kwa nini awe mume ama mke, mjadala ni vipi tutaweza kuongeza nguvu za Seneti ili liheshimike inavyo takikana.
view
11 Nov 2020 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika.
view
11 Nov 2020 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kupinga Mswada huu wa kubadilisha vikao vya Bunge kutoka Jumanne, Jumatano na Alhamisi mpaka Jumanne ambayo ni siku moja kwa wiki. Nimekuwa hapa kutoka jana na Ripoti muhimu ya kamati yangu. Jana nilikaa hapa kuanzia saa nane unusu mpaka saa kumi na mbili unusu tulipoahirisha kikao. Sikuweza kupewa fursa ya kuweza kuendeleza hiyo Ripoti. Leo vile vile, nimekuwa hapa kutoka saa nane na nusu mpaka saa hii, saa kumi na mbili, na sijaweza kupata fursa ya kuendeleza Ripoti yangu. Bi Spika wa Muda, hii inamaanisha kwamba wakati ambao tuko nao ...
view
10 Nov 2020 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I beg to lay the following Paper on the Table of the Senate, today, Tuesday, 10th November, 2020- Report of the Sessional Committee on Delegated Legislation on the Crops (Tea Industry) Regulations, 2020, Legal Notice No. 97 of 2020. I thank you.
view
10 Nov 2020 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I wish to give notice of the following Motion- THAT, the Senate adopts the Report of the Sessional Committee on Delegated Legislation on the Crops (Tea Industry) Regulations, 2020- Legal Notice No. 97 of 2020, laid on the Table of the Senate on Tuesday, 10th November, 2020 and that pursuant to Section 18 of the Statutory Instruments Act and Standing Orders No. 221(4)(b) and 221(5)(b), annuls in its entirety, the Crops (Tea Industry) Regulations, 2020 - Legal Notice No. 97 of 2020. I thank you, Mr. Speaker, Sir.
view
10 Nov 2020 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Shiyonga. Ni jambo la kutamausha kuwa Waziri Magoha alimkejeli na kumtusi afisa wa elimu katika eneo la Rift Valley kwa njia ambayo haikuwa sawa kulingana na maadili ya bindadamu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
10 Nov 2020 in Senate:
Sifa kubwa ya kiongozi ni kwamba lazima awe mtu wa kuheshimu sheria na binadamu wengine, lakini kitendo Prof. Magoha alifanya kinakiuka maadili hayo. Sote tuna mapungufu katika utendakazi wetu, na itakuwa si sawa kwa kiongozi yeyote kumuita mwenzake mjinga ama mpumbavu akiwa hadharani penye kila mtu anaweza kuona. Hayati Julius Nyerere alisema kwamba mtu mpumbavu amezaliwa mpumbavu. Yaani, kwa Kiingereza, he is a fool. Mjinga ni yule ambaye hana ufahamu wa jambo fulani. Kwa hivyo, akifahamishwa, ule ujinga huwa unaondoka. Bi. Naibu Spika, kama kulikuwa na jambo ambalo Waziri aliona kuwa kuna na upungufu kwa yule afisa wa elimu, angemwita ...
view