Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1321 to 1330 of 1994.

  • 24 Nov 2020 in Senate: To date, 26 years later, the victims of the MV Mtongwe Ferry disaster have never been compensated. The proposed handing over of the KFS to KPA violates Article 186 and Schedule 4 (2) of the Constitution of Kenya, which provides that ferry services are functions of county government and should be transferred to the County Government of Mombasa. The Kenya Ports Authority Act gives KPA a specific mandate of managing the ports in Kenya, but does not extend this mandate to managing the operations of ferries. Over the years, the management and operation of KFS has deteriorated, largely because of ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Madam Temporary Speaker, is the Nominated Senator for Wajir in order to cast aspersions on a Committee of this House? view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Najiunga na wenzangu kumpa kongole Sen. Sakaja, Seneta wa Nairobi, kwa Ripoti ya ufasaha na utendakazi ambayo ameweza kuitoa. Ningependa kushauri kuwa, wale ambao wametoa ardhilhali wakati wamepeleka mashtaka mahakamani, wangeshauriwa kuondoa mashtaka yale mahakamani kwa muda. Kwa Kiingereza wanasema: Withdraw the proceedings, amaby o inakupa fursa ya kuleta mashtaka yale kortini baadaye wakati utaona kwamba labda juhudi za Kamati ya Seneti hazikuweza kufua dafu. Watakapoondoa mashtaka yale Kortini, wataweza kupata fursa baada ya muda, iwapo Kamati haikuweza kutoa mwafaka mzuri wakaweza kufuatilia maswala yale kule kule mahakamani, ambapo alikuwa ameenda ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Rais kwa Bunge zote mbili iliyosomwa wiki iliyopita. Kwanza ningempongeza Rais kwa Hotuba yake ambayo iligusia mambo mengi na ambayo alieleza kwa ufasaha zaidi. Vile The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Nov 2020 in Senate: vile, ningependa kumpa kongole kwa zile ripoti nne ambazo aliweza kutoa katika Bunge kama inavyosema Katiba yetu. Hii ni mara ya tatu katika Bunge hili kwa Mhe. Rais kuja kuhutubia Bunge. Kila anapokuja kuhutubia Bunge huwa anatoa ratiba ya zile kazi ambazo Serikali yake imeweza kufanya kwa muda huo mpaka pale hali ilipofika kufikia sasa. Bi Spika wa Muda, nitagusia mambo matano ambayo Rais ameweza kuzungumzia katika Hotuba yake. Kwanza kabisa nitaanza na swala la usalama. Rais alieleza kuwa swala la usalama wa nchi ni mzuri sana na hakuna jambo lolote ambalo linaweza kuchukuliwa kama la kutishia kama usalama wa ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Bi Spika wa Muda, jambo la tatu ni swala la vita dhidi ya ufisadi. Ufisadi umerejea tena upya katika nchi yetu. Tukiangalia matumizi za pesa za COVID-19 na utoaji wa zabuni katika Kenya Medical Supplies Authority (KEMSA), yote haya ni maswala ambayo yako wazi, ambapo Rais angeweza kuyazungumzia kwa ufasaha zaidi. Bi Spika wa Muda, hapo nyuma, Rais alikuwa ametoa ilani ya siku 21 kwa Directorate of Criminal Investigations (DCI) na Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) kuhakikisha kwamba wale ambao wamekula pesa za KEMSA ambazo zilinuiwa kusaidia katika vita dhidi ya COVID-19 katika nchi yetu ya Kenya washtakikwe na wapelekwe ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: katika enzi za chama kimoja na wapinzani kupigwa na wengine kuumizwa kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa. Hili swala la uhusiano na nchi za nje, lazima Serikali yetu iliingalie. Wale wanapigwa Tanzania ni kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa. Hawapigwi kwa sababu wameweza kuvunja sheria. Bi Spika wa Muda, nikiongezea, kuna kisa ambacho mtu aliuliwa hivi juzi kwa sababu alipigwa na wanajeshi kule Tanzania na ana familia yake katika eneo la Mombasa. Ilikuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mtu amepoteza maisha katika mikono ya Serikali na hakuna jambo lolote ambalo ataweza kufanya kulingana na sheria zao. Swala la ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Bi Spika wa Muda, tumeona kwamba kumekuwa na hatua fulani ya Serikali kuingilia majukumu ambayo yanatakikana kufanywa na Serikali zote za kaunti katika Jamhuri hii yetu. Nashukuru kwa kunipa fursa hii ya kuweza kuchangia Hotuba ya Rais. Kabla sijamaliza, nilisikitishwa kwamba dadangu, Sen. (Dr.) Zani ambaye babake alikuwa ni mwalimu wa Kiswahili, ameweza kuchangia Hotuba hii ya Rais kwa lugha ya Kiingereza. view
  • 11 Nov 2020 in Senate: Thank you, Madam Deputy Speaker. I stand pursuant to Standing Order No.51 (1) (b) of the Senate Standing Orders to make a Statement relating to the activities of the Sessional Committee on Delegated Legislation from 6th May, 2020 to 4th November, 2020. The Sessional Committee on Delegated Legislation is established under Standing Order No.221 of the Senate Standing Orders. The Committee is mandated to scrutinize statutory instruments laid before the House to ensure that they are consistent with the provisions of the Statutory Instruments Act, 2013. During the review period, the Committee held 64 meetings, during which we considered 25 ... view
  • 11 Nov 2020 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, tukubaliane kwamba ripoti iliyotolewa na Kamati ya Sheria na Haki za Kibinadamu inafaa kuungwa mkono. Tunafaa kujua jinsi tutakavyosongeza mjadala huu mbele. Kuna msemo wa Kiswahili kuwa “wingi si hoja”. Seneti inaweza kuongezewa Maseneta hadi 290 lakini hatutakuwa tumesaidia kwa yale ambayo Seneti inafaa kufanya kwa sababu haitakuwa na uwezo wowote. Tunafaa kuwa na Seneti iliyo na mamlaka kama vile wengine katika taasisi tofauti tofauti wameongezewa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus