Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1341 to 1350 of 1994.

  • 10 Nov 2020 in Senate: Ningependa kuchangia Hoja ya Nidhamu ya Sen. Wambua kwamba, kuna Taarifa za Maseneta za kibinafsi na kuna zingine za Kamati ambazo tunafaa kuzipea kipaumbele. Mwenyekiti wa Kamati hawezi kukaa mpaka saa hii ambapo tunajadili Taarifa za kibinafsi. Mwenyekiti wa Kamati anaweza kuwa na Taarifa ya Kamati ambayo ni muhimu zaidi kuliko Taarifa ya kibinafsi. Wakati tunapanga ule wakati, tungezingatia jambo hilo kwa sababu zile Taarifa ambazo zinasomwa hapa, kwa mfano, nimekaa hapa kutoka saa nane unusu na niko na Ripoti ya Kamati na vilevile niko na Hoja ambayo nimepeana na mpaka hivi sasa, 5.30 p.m., sijapata fursa ya kuzungumzia Hoja ... view
  • 10 Nov 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kwa hivyo, nafasi hii ikipatikana, itakuwa ni wakati mzuri wa kuuliza maswali ya kiufundi ama ya kiteknolojia kuhusiana na hawa wakurugenzi wa Safaricom. Hiyo ni ili kuona kwamba mwananchi hapunjwi katika huduma wanazopata kutokana na mashirika haya. view
  • 10 Nov 2020 in Senate: Asante kwa kunipa fursa hiyo. view
  • 5 Nov 2020 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ambayo imeletwa na Seneta wa Lamu, Mhe. Anuar Loitiptip. Bw. Spika, juzi tulitamaushwa na ripoti zilizotoka kwenye vyombo vya habari ambazo zilikiwa zimezugumzwa na Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Usafiri na Miundo Msingi, Bi. Nancy Karigithu view
  • 5 Nov 2020 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. On 25th May, 2020, I sought a Statement on the shooting down of a Kenyan aircraft in Somalia. In the Statement, I requested the Committee on National Security, Defence and Foreign Relations to investigate the shooting down and maybe bring a report to the House. Mr. Speaker, Sir, to date, I have not had any engagement with the concerned Committee. To make matters worse, the International Air Transport Association (IATA) rules provides that a preliminary report be issued by the host country where the accident occurred and what measures they are taking to avoid future ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Asante, Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ombi ambalo limeletwa katika Bunge na Seneta wa Kaunti ya Vihiga, Sen. Khaniri. Utamaduni ama ustaarabu ndio chanzo cha utu na ubinadamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba kwa sasa tumeweza kuweka ustaarabu na utamaduni wetu nyuma kiasi ambacho vizazi vijavyo huenda vikapotea na vikawa havina mwelekeo. Kwa mfano, Mombasa ilikuwa ni kitovu cha ustaarabu wa Waswahili. Kule ndiko lugha ya Kiswahili ilianza kuzungumzwa na ikasambaa sehemu za bara. Ni masikitiko makubwa kwamba hata zile taasisi za zamani ambazo zilisaidia kukuza na kuendeleza utamaduni huu hazipo tena. Bi Naibu Spika, kaunti zote ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Bi. Naibu Spika, jengo la Fort Jesus katika Mji wa Mombasa ni la kale sana. Wanahistoria husema lilijengwa karne ya 15. Sasa hivi ni mahame na magofu. Hakuna watalii wa kutoka nje wanaozuru jumba hilo kwa sababu halijawahi kufanyiwa ukarabati wowote. Juzi ufuo wa bahari wa Mama Ngina ulifanyiwa ukarabati. Wakati walipokuwa wakifanya ukarabati huo, kulipatikana makaazi au mijengo ambayo ilijengwa karne ya 12. Ni lazima tutilie mkazo swala la kulinda na kuhifadhi tamaduni kwa sababu ya vizazi vijavyo. Bi. Naibu Spika, kila kabila au jamii yoyote ina tamaduni zake. Lazima tuheshimu tamaduni za jamii zingine kwa sababu ndio mwanzo ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kifungu cha 48 (1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti, kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Leba na Ustawi wa Jamii kuhusu kuteuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Bahari, KenyaMaritime Authority. Kwenye Taarifa hiyo, Kamati inafaa: (1) Kufafanua sifa zilizohitajika kwa mwombaji wa wadhifa huo wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Bahari. (2) Kuelezea idadi ya wakenya waliowasilisha maombi yao kwa wadhifa huo. (3) Kutoa ripoti kuhusu waliobobea kwenye mahojiano na waliowasilisha maombi ya kutwaa wadhifa huo. (4) Kuelezea sababu ya Waziri ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Bi. Naibu Spika, ningeongezea kwamba uteuzi huo umefanywa kinyume na sheria. Hii ni kwa sababu sheria inasema kwamba wa kwanza katika interview aweze kupewa wadhifa huo. Huyu mhusika alikuwa wa nne katika mahojiano ya kupewa wadhifa huo. Alikuwa hastahili kupewa wadhifa huo. view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Jambo lingine Bi. Naibu Spika ni kwamba alikuwa hana uwezo au tajiriba ya mtu ambaye ameweza kufanya kazi katika mazingara ya Bandari, yani Maritime Industry kwa muda unao stahili. Kuteuliwa kwake ni kinyume na sheria. Ningependa kwamba Kamati The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus