29 Sep 2020 in Senate:
On a point of Order, Madam Deputy Speaker.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Madam Deputy Speaker, the apology read by Sen. Kwamboka does not include her full name as stated by the Communication from the Chair. She said, “I Beatrice and I Kwamboka.” The name should be cited the same way it was read in the Report and in the Communication from the Chair.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya vifaa vya matibabu. Kwanza, ninajiunga na Maseneta wezangu kupongeza Kamati kwa kazi nzuri iliyoifanya ya kuzuri kaunti kadha wa kadha ili walete ripoti hii.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Nilibahatika kuandamana na Kamati katika ziara yao ya Kaunti ya Mombasa, Kilifi na Tana River. Tulizuru Mombasa kwa arifa ya siku moja. Tulipozuru Coast General Teaching and Referral Hospital, ambapo vifaa vingi vilikua vimewekwa, Kamati iliridhika na matumizi ya vifaa vile. Vifaa katika hospitali hiyo vilikua vinatumika vilivyo.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, najiunga na wenzangu kusisitiza kwamba vifaa hivi vimetumika vizuri katika Kaunti Ya Mombasa. Mradi huu umesaidia sana Kaunti ya Mombasa kukimu mahitaji ya vifaa maalum vinavyo hitajika kuhudumia wananchi.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Mradi wa MES ulikuwa na lengo nzuri sana. Tulipoenda Tana River, tuliona kuwa vifaa vingine vilikuwa pale kama vile Computerized Tornography (CT) scan na X-Ray. Vifaa vinatumika ingawa kuna uhaba wa wataalamu. Kwa mfano, X-Ray na CT scan zao zilikuwa ni lazima kupelekwa Mombasa kusomwa na kurejeshwa Tana River ili watu waweze kuhudumiwa.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Mradi huu ulikuwa na malengo mazuri sana. Lakini utekelezaji wake ndio uliyoleta mtafaruku, sinitofahamu na ufujaji wa pesa. Jambo la kwanza hakukufanywa utafiti wa kujua mahitaji ya kila kaunti. Ingekuwa ni jambo bora kama tungejua mahitaji ya vifaa vya kila kaunti ili viwe na manufaa kwa watu wetu. Mrundiko wa masanduku ya vifaa katika stoo za kaunti zetu hauna faida kwa watu wetu ikiwa vifaa hivyo havitumiki vilivyo.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, utaona pia kuwa kaunti nyingi hazikuwa zimejitayarisha. Kwa mfano, mashini za dialysis zinahitaji maji safi. Hospiali nyingi nchini hazina maji safi na kutosha kuwahudumia wananchi wetu. Ni kweli kaunti nyingi hazikua zimejitayarisha kupokea vifaa hivi.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Kaunti ambazo zinaona mbele zimefaidika na vifaa hivi. Kaunti ambazo bado ziko katika fikra ya kurudi nyuma hazijafaidika na vifaa hivi. Hatukuweza kupata value formoney katika kaunti nyingi ambazo vifaa hivi vimepelekwa.
view
29 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, pia nilibahatika kuzuru Kaunti ya Meru na Kamati ya COVID-19. Tuliona kwamba vifaa vya ICU walivyopewa vilikua bado katika stoo miaka mitatu iliyopita. Hawajaweza kujenga ICU kuweza kutumia vifaa hivo. Tulizuru Kaunti ya Kilifi. Vifaa vya ICU havijatumika kwa muda wa miaka mitatu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view