Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1431 to 1440 of 1994.

  • 24 Jun 2020 in Senate: Swala hili limeangaziwa pia katika katiba. Katika Kifungu cha 66, kinachozungumzia matumizi ya ardhi na rasilimali. Kifungo hicho kinapeana mwongozo wa matumizi ya ardhi au chochote kilichoko katika ardhi ile kwa masuala ya usalama, usalama wa uma, ‘ public order’, ‘public morality’, ‘public health’ na vile matumizi ya ardhi ile. Imesemekana hapa kwamba Bunge litaweka sheria ya kuhakikisha kwamba uwekezaji katika mali kama hizi zinafaidisha wakaazi au wenyeji na uchumi wao katika maeneo yale. view
  • 24 Jun 2020 in Senate: Bi. Naibu Spika, Bunge ilikuwa itowe sheria kuhakikisha kwamba rasilimali kama hizi; dhahabu, bahari na madini yeyote mengine ambayo yako, yatakuwa yanafaidisha jamii zilizoko sehemu zile pamoja na uchumi wao. Wakati huu, watu wa Kaunti ya Nandi, Migiori na Taita Taveta wanalalamika. Zamani, wakati Hayati Mzee Jomo Kenyatta alipotembea Taita, aliwaambia Wataita ambao ni shemeji zake Seneta wa view
  • 24 Jun 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Jun 2020 in Senate: Kaunti ya Nairobi, Sen. Sakaja, kwamba Wataita wamekalia uchumi. Wakati huo, alimaanisha kwamba kuna madini mengi katika eneo la Taita ambazo Wataita hawajaweza kutafuta na kuhakikisha kwamba yanasaidia uchumi wa eneo hilo. view
  • 24 Jun 2020 in Senate: Arifa hii ni muhimu sana kwa sababu inagusia sehemu zote za nchi hata maeneo ambayo haina rasilimali za madini. Kuna rasilimali za aina mingi kama; mifugo au wanyama pori ambazo zinaweza kusaidia kuinua hali ya uchumi wa wananchi pamoja na kaunti ambazo zinahusika. Kamati husika lazima iangalie swala hili kwa undani Zaidi ili kuhakikisha kwamba haturejei hapa tena kuzungumzia swala hili ambalo limekuwa donda sugu kabla ya uhuru wa nchi hii. Kabla ya kupata Uhuru, tulikuwa tunapigania rasilimali. Waliokuwa katika maeneo ya White Highlands, walikuwa wanapigania mashamba ambayo ni rasilimali yao. Wapwani tulikuwa tunapigania uchumi wetu ili tuweze kuimarika na ... view
  • 24 Jun 2020 in Senate: Bi. Naibu Spika, asante sana kwa kunipa fursa. view
  • 23 Jun 2020 in Senate: Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Arifa iliyoulizwa na Seneta wa Taita/Taveta kuhusiana na pesa zinazotolewa kwa maswala ya kupambana na ugonjwa wa Korona. Bi. Naibu Spika, wiki mbili zilizopita, tulibahatika pamoja na Kamati ya COVID- 19 kusafiri Kaunti ya Isiolo kwa minajili ya kuona jinsi wamejitayarisha kupambana na janga hili. Jambo la kusikitisha ni kwamba hata Ofisi ya Gavana ilikuwa haina nafasi ya kuweza kutu pokea kama Maseneta ambao tulikuwa huko hususani kuanaglia ile miradi ya kaunti kuhusiana na maswala ya Korona. Bi. Naibu Spika, tulipelekwa katika police pavilion ambayo ndugu yetu Sen. Linturi alikuwa akitembelea ... view
  • 23 Jun 2020 in Senate: vinanunuliwa, wananchi wanapewa barakoa na kadhalika. Hizi zote ni vitu za kuonyesha tu, lakini kwa ukweli hakuna jambo lolote linatendeka. view
  • 23 Jun 2020 in Senate: Tulizuru hiyo Intensive Care Unit (ICU) . Tulionyeshwa vitanda ambavyo vilisemekana vilinunuliwa vipya. Yasemekana vingine ni automatic, ukibofia, kinainuka. Daktari mmoja alibofia karibu mara sita ilihali kitanda hiki hakikuinuka. Sisi tulikuwa palepale. view
  • 23 Jun 2020 in Senate: Bi. Naibu Spika, ufujaji wa pesa ni jambo ambalo liko wazi. Jana maafisa wa Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists Union (KMPDU) walikuwa wanalalamika ya kwamba kaunti tano hazijalipa mishahara ya madaktari pamoja na wahudumu wa afya wakati huu tunapambambana na Korona. Ni vipi tutaweza kupambana na Korona ikiwa wafanyikazi hawalipwi mishahara? Daktari anafanya kazi katika hali ambayo ni ngumu. Anajihatarisha maisha yake na ya familia yake. Kwa mfano, anapewa barakoa moja. Hiyo ndiyo anaenda nayo nyumbani jioni. Kesho asubuhi anapewa ya pili. Bi. Naibu Spika, hili ni swala ambalo Kamati hii inaweze kuchunguza kwa undani na kuhakikisha pesa hazifujwi. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus