12 Mar 2019 in Senate:
Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view
12 Mar 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I have heard you say that Kiswahili is the language of Mombasa. It is a national language used in this Senate, the National Assembly and all other places. It is, therefore, the national language in Kenya.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I was just clarifying.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa kanuni za kaunti, ama kwa Kiingereza, The County Statutory InstrumentsBill, 2018 . Mswada huu umekuja wakati mwafaka kwa sababu kaunti nyingi hazijapitisha mwongozo wa vipi watachapisha kanuni ambazo zinatumika kutekeleza sheria ambazo wanapitisha katika mabunge ya kaunti. Kwa hivyo, Mswada huu utasaidia kuwapa mwongozo zile serikali au mabunge ya kaunti kuhakikisha kwamba ni njia gani watatumia kupitisha kanuni ambazo zitatumika kutekeleza sheria zinazopitishwa.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, mara nyingi mambo yote hayawekwi katika miswada ya sheria; ila ni baadhi ya mambo tu yale muhimu yanayowekwa katika miswada ya sheria. Watekelezaji wa sheria hizi au kile kitengo cha utekelezaji, yaani the executive wanapewa fursa na sheria kutunga kanuni ambazo zinasaidia kutekeleza zile sheria zilizopitishwa. Kwa hivyo, sheria hii ni kigezo muhimu cha kuendeleza na kuzipa fursa serikali za kaunti kuhakikisha kwamba wanapitisha miswada; na vile vile kwamba miswada yenyewe inapitishiwa kanuni ya kuitekeleza.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, sheria hii pia inajumuisha kaunti zote katika Jamhuri ya Kenya. kwa hivyo, kila kaunti ambayo haijapitisha mwongozo kama huu itapata fursa ya kutumia mwongozo huu ili kupitisha zile kanuni ambazo wanataka kupitisha ili kuendeleza kazi zao. Mara nyingi, kanuni hizi hutumika katika kukusanya ushuru au leseni kadha wa kadha ambazo zinatumika katika serikali za kaunti. Kwa hivyo, bila kanuni hizi, inakuwa vigumu kwa serikali za kaunti kukusanya fedha za kutekeleza miradi wanayoendeleza katika kaunti zao.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Bi. Spika Wa Muda, sheria hii inatoa mwongozo kwa Executive na kuwapa uwezo wa kutunga kanuni; lakini lazima kanuni zitakazotungwa ziambatane na ile sheria iliyopitishwa. Haiwezekani kwamba sheria inazungumza tofauti na kanuni ambazo zinapitishwa na wale watekelezaji zinakuwa tofauti. Kwa hivyo, sheria inatoa mwongozo kwamba lazima kanuni zote zitakazotengenezwa zilingane na ile sheria iliyopitishwa.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Vile vile, Bi. Spika wa Muda, uwezo uliopewa serikali za kaunti, yaani Executive, wa kutunga kanuni kanuni hizi, sio uwezo ambao hauna vigezo. Huu ni uwezo ambao lazima utekelezwe kulingana na vile sheria inavyosema. Kwa hivyo, iwapo watakwenda kinyume na zile sheria, zile kanuni ambazo watakuwa wametengeneza hazitakuwa na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Mar 2019 in Senate:
maana yoyote kwa sababu zinapinga sheria ambazo ziko. Kupitisha kanuni hizi itasaidia kuyapa mabunge ya kaunti uwezo wa kuangalia ama kudhibiti uwezo wa serikali za kaunti katika kupitisha kanuni ambazo labda zinawaathiri wananchi katika eneo lile. Inasemekana kwamba sheria hii inaipa bunge la kaunti lile jukumu la kuangalia na kuangazia kazi zinazofanywa na kitengo cha utekelezaji, yaani executive kuhakikisha kwamba kanuni wanazopitisha zinaambatana na sheria.
view