Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1871 to 1880 of 1994.

  • 12 Mar 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, Mswada huu pia unatoa mwongozo wa vipi zile kanuni zitatengezwa hadi ziwe sheria. Kuna kifungu ambacho kinasema kwamba lazima ichapishwe katika gazeti rasmi la Serikali, na vile vile katika magazeti rasmi ya kaunti. Vile vile, inatoa fursa kwa wananchi ama washikadau wote katika kitengo kile ambacho kimekusudiwa kwenda kutoa mwongozo au kutoa maoni yao. Kwa mfano, ikiwa wanatunga kanuni za kudhibiti biashara ya boda boda, itakuwa ni lazima watoe fursa kwa washikadau wote – waendesha boda boda na wengineo – kutoa maoni yao kulingana na kanuni zilozotungwa. view
  • 12 Mar 2019 in Senate: Vile vile, Bi. Spika wa Muda, kanuni hizi zinazotungwa lazima zipelekwe katika bunge la kaunti ili zichunguzwe kabla ya kupitishwa. Kwa hivyo, hiyo pia inatoa fursa ya kuhakikisha kwamba kanuni zile zinazotungwa na utekelezaji wake zinaambatana na sheria, na zimepitishwa na bunge la kaunti ile. view
  • 12 Mar 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, Mswada huu pia unatoa mwongozo kwamba kanuni zitakazopitishwa zitabatilishwa baada ya miaka kumi kutoka ile tarehe ambayo zimepitishwa. Tunaona kwamba kaunti nyingi zina kanuni za kutoka wakati wa Mwingereza. Kanuni zile zimetumika kutoka wakati wa Serikali ya ukoloni. Ukiangalia katika kaunti nyingi, kanuni zote zinazohusiana na ujenzi wa majumba zilitengezwa wakati wa ukoloni. Kwa hivyo, sheria hii inatoa mwongozo kwamba zile kanuni zinakufa baada ya kila miaka kumi. Pia, sheria hii inapendekeza kwamba zikifa, lazima aidha ziongezewe muda, na muda utakaoongezwa hautazidi miezi kumi na miwili; ama kanuni zingine mpya zipitishwe kuhakikisha kwamba zinaambatana na sheria. ... view
  • 12 Mar 2019 in Senate: Swala lingine, Bi. Spika wa Muda, ni kwamba Kifungu cha 16 kinasema kwamba lazima kila kanuni itakayopitishwa na kukubaliwa iwekwe katika gazeti rasmi la Serikali, yaani Kenya Gazette na vile vile county gazette . Pia, lazima zipewe namba maalum; kwa mfano, No.001/1/2019. Huo ni mfano wa zile namba zitakazopeanwa katika hizi kanuni za kaunti ili ziwe rahisi kuzipambanua zinahusiana na jambo lipi, na ile inahusiana na jambo lipi. view
  • 12 Mar 2019 in Senate: Vile vile, sheria hii inasema kwamba kama kunatengenezwa kanuni fulani kuhusiana na swala fulani; kwa mfano, iwapo wanatengeneza kanuni kuhusiana na swala la kahawa, kanuni zile zitahusika na kahawa peke yake na hazitatumika kudhibiti maswala ya boda boda ama mambo mengine ambayo yanaweza kutokea. Kwa hivyo kila kanuni itakayotengezwa inahusisha sehemu fulani tu ya lile swala ambalo linadhibitiwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 Mar 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kusema ukweli Mswada huu umekuja wakati mwafaka, na ni lazima tuunge mkono kwa sababu ni njia moja ya kusaidia serikali za kaunti kuweza kupata mapato ya kusaidia kuendesha kazi zao. Vile vile, kanuni ambazo zitaleta maswala ya kifedha – yaani zinazipa serikali za kaunti fursa ya kukusanya kodi – ni lazima ziwe na kodi maalum; kodi ya chini na juu. Kwa Kizungu yaani ni minimum na view
  • 12 Mar 2019 in Senate: charges ambazo zitakuwa zinalipishwa. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, Mswada huu ni mzuri sana, na umeletwa wakati mwafaka ambapo mabunge mengi ya kaunti hayana sheria kama hii. Nawaomba ndugu zangu, Maseneta wote, waunge mkono Mswada huu kwa sababu utaleta manufaa Zaidi kwa serikali zetu za kaunti. view
  • 12 Mar 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. view
  • 27 Feb 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa kuchangia Ombi ambalo limeletwa na Seneta wa Nakuru, Sen. Kihika. Lilikuwa ni jambo la aibu na la kuvunja moyo sana kuona watoto zaidi ya 40 wakilalamika kwamba wametupwa msituni na maafisa wa Kaunti ya Nakuru. Ningependa kuwapongeza wakaazi wa eneo ambalo watoto walitupwa kwa ubinadamu wao. Waliwapokea wale watoto, wakawapa chakula na kuwasaidia kwa usafiri kurudi Nakuru. view
  • 27 Feb 2019 in Senate: Jambo kama hili halifai kufanyika wakati huu wa sasa baaada ya kupitisha sheria mpya ya watoto, yaani Children Act, ambayo ilipitishwa kutoka Mwaka wa 2005. Inafaa vyombo vya usalama vichukue hatua mara moja kuhakikisha kwamba wale ambao walifanya huu unyama wameshitakiwa, kufungwa na kupoteza kazi zao katika Kaunti ya Nakuru. Hii ni kwa sababu jambo hili linatia dosari na doa Serikali ya Kaunti ya Nakuru. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus