27 Feb 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, mambo kama haya yanaendelea kutokea katika sehemu tofauti. Ukiangalia hata hapa Nairobi, watoto wengi ambao wanarandaranda wanachukuliwa kama wahalifu, ilhali ni jukumu la Serikali ya Kaunti kuhakikisha kwamba wanapata makao, chakula na nguo, ili waishi kama binadamu wengine. Jambo kama hili ni lazima lichunguzwe na tuhakikishe kwamba wale ambao walihusika na huu unyama wanapewa adhabu ya kutosha. Asante, Bw. Naibu Spika.
view
27 Feb 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati kuhusu shida zinazowakumba wakulima wa mahindi. Kwanza, ninapongeza Kamati iliyoongozwa na Seneta (Prof.) Kamar na Seneta Wetangula kwa kazi nzuri iliyoifanya kuhakikisha kwamba dhambi zote ambazo wakulima wa mahindi walitendea katika eneo la kasikazini ya ponde la ufa na kwingineko nchini Kenya yameaangaliwa na kutolewa suluhisho. Hii Ripoti ya mahindi inatukumbusha mambo ya sukari katika eneo la pwani. Kiwanda cha Sukari cha Ramisi kilikuwa kiwanda cha kwanza kusaga sukari katika miaka ya 1950. Jambo la kusikitisha ni kwamba sukari ililetwa kwa wingi kama yalivyoletwa mahindi mwaka jana ...
view
27 Feb 2019 in Senate:
kushugulikia maswala ya ukulima ni za ili wakulima wasiwe watu wa kuombaomba milele na milele katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika, nikimalizia, ningependa kusema kwamba Ripoti hii inaweza kutumika katika sekta zingine zozote ambazo zinahusika na ukulima. Kwa mfano, kuna sekta ya sukari ambayo imelemaa kwa muda mrefu. Vile vile kuna sekta za kahawa, majani chai na zingine ambazo zimeshindwa kujiinua na kujinasua katika lindi la ufisadi ambalo linaendelea kwa sasa. Asante sana, Bw. Naibu Spika.
view
14 Feb 2019 in Senate:
Madam Temporary Chairperson, I second.
view
14 Feb 2019 in Senate:
Madam Temporary Chairperson, I second.
view
27 Nov 2018 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, on a point of order.
view
7 Nov 2018 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi hili kuhusu kahawa, chai na macadamia. Kule Pwani mazao makubwa ni korosho na nazi. Mazao haya mawili yamewekwa katika kaburi la sahau. Tulikuwa na mtambo wa korosho kule Kilifi kwa Sen. Madzayo, lakini mtambo huo umekuwa mahame sasa. Hakuna yeyote ambaye anachukua fursa hiyo kuweza kufufua mtambo ule. Vile vile, kule Kwale ambako ndugu yangu, Sen. Boy, anatoka, kulikuwa na mtambo wa Bixa, yaani ile mirangi ambayo inatumika kuweka rangi kwenye chakula ama bidhaa zingine tofauti. Tunaunga mkono ombi hili kwa sababu wakulima wengi katika eneo la Pwani wanapata shida ya ...
view
6 Nov 2018 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa Data . Kwanza, naipongeza Kamati ya---
view
6 Nov 2018 in Senate:
Bw. Naibu Spika “Data” ni Kiswahili. Angalia Kamusi ya---
view
6 Nov 2018 in Senate:
Naam, Bw. Naibu Spika. Nina uhakika.
view