Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1891 to 1900 of 1994.

  • 6 Nov 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, nimefanya utafiti wa kutosha. Kwanza naipongeza Kamati ya Seneti iliyo kuja na Mswada huu ambao umekuja kwa wakati mwafaka kwa sababu tumeona kwamba kadiri tunavyoendelea, mambo yanayoibuka ni mengi. Jambo moja lililoibuka ni maendeleo katika maeneo ya teknolojia. Kwa hivyo, tunaweza kukusanya data nyingi za wananchi wa Kenya na taasisi nyinginezo na ipo haja ya kulinda data hiyo ili isitumiwe vibaya, kwa mfano, wanaweza kuitumia kwa uhalifu au mambo mengine ambayo haifai kijamii. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Jambo la pili ni kwamba Mswada huu pia unazingatia Kifungu Nambari 31 cha Katiba ya Kenya. Ni jukumu la Serikali au nchi kulinda data ya kibinafsi ya watu na kuangalia ni njia gani inaweza kukusanywa, kuwekwa na kuzingatia haki za watu. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, hapo nyuma tumeona kwamba data imetumika vibaya mpaka ikabidi wakurugenzi wa Face Book kwenda katika Bunge la Congress la Marekani kujieleza ni vipi watu ambao hawa kuruhusiwa walitumia data ya watu binafsi bila kuomba ruhusa kwa wahusika. Hili ni jambo ambalo liko wazi na ni lazima tuweke msingi wa kulinda data ya watu. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Nimepitia vipengele kadhaa katika Mswada huu na ninaona kwamba vyote vina jaribu kulinda haki za kibinadam. Kwa mfano, haki ya kuwa na siri au privacy kwa Kiingereza, katika data yako. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, Mswada huu unalinda wananchi wasifanyiwe ubaguzi wa kidini, kijinsia au kitabaka. Kifungu 13, kinalinda watu kutokana na data yao kutimika kuwabagua kibinadamu, kidini, kirangi, kikabila na vingenevyo. Hapo nyuma hasa jamii ya Waisilamu, wale wanaotoka sehemu za Kaskazini Mashariki mwa Kenya wamefanyiwa ubaguzi na wakakusanywa pamoja na kuchunguzwa ilhali wengi wao hawakuwa wahalifu. Mswada huu unaweza kusaidia sana kuhakikisha ya kwamba haki za kibinadamu zinalindwa katika nchi ya Kenya. Mswada huu unazingatia pakubwa data isitumike kwa njia ambayo si sawa. Katika Kifungu cha 14, wanasema kwamba data ichukuliwe ikizingatia usiri wa mtu anayechukuliwa na vile vile pia ... view
  • 6 Nov 2018 in Senate: kadi zinazotumika katika benki wakati kazi zile zingeweza kufanyika hapa nchini na wananchi wakaweza kupata ajira na mashirika yetu pia yakazidi kuendelea. Bw. Naibu Spika, hapo awali, data pia imetumika vibaya kwa wananchi kwa sababu watu wanapata zile data kutokana na mashirika mbalimbali na kuzitumia vibaya, kwa mfano, wakati wa kupiga kura, watu wanapata ujumbe au email za kueneza view
  • 6 Nov 2018 in Senate: nyingi ambazo hawakutarajia kwamba watu wale wataweza kupata habari ama view
  • 6 Nov 2018 in Senate: ya watu binafsi na kuitumia kwa mambo yao ya biashara. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu kwa sababu utaenda pakubwa kuhakikisha kwamba data za raia wa Kenya na mashirika kadha wa kadha zitalindwa na kuhakikisha kwamba kuna usalama na uwazi zinavyokusanywa. Bw. Naibu Spika, kuna vipengee vya kuwahukumu wale ambao watapatikana na hatia. Najiunga na Seneta wa Migori kusema kwamba ile hukumu ambayo imepeanwa ni nyepesi kwa sababu matatizo ambayo yatatokea wakati data itatumika vibaya ni makubwa kulingana na vile ambavyo yule ameiiba ataitumia. Kuna haja ya kulinda data ya watoto na wale ambao hawajafikia umri wa miaka 18 kwa ... view
  • 24 Oct 2018 in Senate: Madam Temporary Speaker, pursuant to Standing Order No. 48(1), I rise to seek a Statement from the Standing Committee on Education on the release of the Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE) certificates to students who have completed secondary school education in the country. In the Statement, the Committee should address the following- (1) State the number of certificates that have been released since the directive by the national Government to give a blanket waiver to candidates unable to clear their fees and have their certificates released. (2) Indicate how many certificates are pending release and out of these, how ... view
  • 24 Oct 2018 in Senate: seconded. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus