Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1951 to 1960 of 2123.

  • 9 Apr 2019 in Senate: Pia tukiangalia ukulima katika eneo la Mombasa, bado hakuna jambo lolote linalofanyika. Sehemu zingine watu wanapewa ruzuku za mbegu, mbolea na pembejeo nyingine lakini mpaka sasa katika eneo la Pwani au Mombasa, hakuna jambo lolote la ukulima ambalo linafanyika. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: Kwa hivyo tunaiomba Serikali ifanye juhudi kubwa ili kuinua uchumi kwa sababu katika eneo la Pwani, Kwale ina uwezo wa kulisha Pwani nzima kwa jumla. Tana River na Kilifi pia zina uwezo mkubwa wa kuweza kulisha Pwani lakini utapata kwamba hivi sasa wanajitahidi ili waweze kuzuia baa la njaa ambalo limezuka kutokana na kuchelewa kwa mvua. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: Hotuba ya Rais ilikuwa na mambo mengine mazuri na mengine mabaya ambayo tungependa Serikali irekebishe. Tunaona ya kwamba iwapo hatutakuwa makini tutapata matatizo makubwa siku za usoni kwa sababu wale wote ambao wanakosa nafasi za kazi, na wanaoathirika na madawa ya kulevya katika miji yetu kule Mombasa na kwingineko, watakosa nafasi ya kujiendeleza kimaisha. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ninaunga mkono Hotuba ya Rais. Nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja hii. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 21 Mar 2019 in Senate: Madam Temporary Speaker, I was surprised by the learned Senate Majority Leader canvassing an issue which is actively before a tribunal where he represents one of the parties in that matter. Is he in order to canvass an issue which is before a tribunal here? view
  • 21 Mar 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Statement ya Sen. Malalah kuhusu vita dhidi ya ufisadi. Ni lazima tupambane na ufisadi kwa sababu ufisadi umekuwa donda sugu katika nchi yetu. Kila mwaka tumekuwa tukilalamika kuhusu ufisadi lakini hatujaona matokeo yoyote ya vita dhidi ya ufisadi. Tumekuwa na taasisi kadhaa za kupambana na ufisadi kama vile Kenya Anti-Corruption Commission (KACC) na EACC lakini hatujaona matokeo ya kazi zake. Mwaka huu, kidogo kazi imeanza kufanywa. Kama ilivyo kawaida, lazima wanasiasa walete siasa mahali ambapo hakuna siasa. Yeyote anayetuhumiwa kwa ufisadi ana haki ya kwenda mahakamani na mahakama ina ... view
  • 21 Mar 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Nimesimama kuambatana na Kifungu 47(1) za Kanuni za Bunge la Seneti kutoa taarifa hii kuhusu hali ya uchumi wa Kaunti ya Mombasa na Kaunti njirani za Kilifi, Kwale, Taita Taveta, Makueni, Kajiado na Machakos. Bi. Spika wa Muda, kaunti hizi ziko katika Ukanda wa Kasakazini au Northern Corridor ya barabara ya Afrika. Ukanda huu unaanzia katika Bandari ya Mombasa na kuelekea mpaka Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura, Goma na Juba katika nchi jirani ya Congo na Sudan Kusini mtawalia. Kwa hivyo, ukanda huu ni muhimu kwa biashara na makazi ya watu. view
  • 21 Mar 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 21 Mar 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, Bandari ya Mombasa ni kiungo muhimu katika uchumi wa kaunti za Pwani hususan Mombasa. Asilimia kubwa ya watu wa Pwani wanategemea Bandari ya Mombasa kwa njia moja au nyingine. Hivyo basi, mama mboga anatarajia mfanyikazi wa bandari kununua mboga zake jioni. Dereva wa lori anatarajia kubeba makasha kutoka Bandari ya Mombasa na wauzamaji barabarani pia wanapata biashara kutokana na bandari hiyo. Bi. Spika wa Muda, mchakato huu wote unaleta mapato kwa kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Taita Taveta, Kajiado, Makueni na Machakos. Iwapo biashara bandarini itapungua, mapato ya kaunti hizi yataathirika kwa sababu kaunti hizi zinategemea ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus