Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1971 to 1980 of 1994.

  • 18 Apr 2018 in Senate: Asante sana, Bwana Spika kwa kunipa fursa hii kujiunga na Wakenya wengine na wakaazi wa Murang’a kuomboleza kifo cha hayati Matiba. Sisi watu wa Pwani, tulimtambua Matiba kama mwekezaji mkubwa katika biashara ya utalii katika eneo la Pwani. Vile vile, alikuwa rafiki mkubwa wa Pwani kwa sababu wakati alipokuwa akiwaania kiti cha Kenya Football Federation (KFF) kama mwenyekiti, Pwani ndio ilimuunga mkono wa kwanza ndiyo nchi nzima ikafuata badaaye. Kwa hivyo, tunamtambua hayati Matiba kama kiongozi ambaye alikuwa akiwapa kipaumbele Wakenya ambao hawakubahatika kijamii, aidha kimasomo, kibiashara na katika hali zingine za kijamii. Kifo cha Matiba pia kinatukumbusha wale wengine ... view
  • 28 Mar 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, nimesimama kuunga mkono Hoja ya Sen. Orengo na kuwapongeza viongozi wetu,vinara wawili; Mhe. Rais Uhuru Kenyatta na Mhe. Raila Amollo Odinga. Viongozi hawa walikuwa mahasimu wajadi lakini juzi, siku tukufu ya Ijumaa, walikuja pamoja, wakakumbatiana, wakapeana mikono na wakashusha hali mbaya ya siasa ambayo iliyokuwepo katika nchi yetu ya Kenya. Ilhali, yapo mengi ambayo bado yana takikana kufanywa kwa sababu ukabila, ufisadina mambo mengi ambayo waliyazungumzia bado yako. Ni lazima tushirikiane kama Bunge la Seneti na nchi kwa jumla kuhakikisha kwamba yametatuliwa. Jambo moja ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba hatuna kitu cha kutuunganisha pamoja sisi kama Wakenya ... view
  • 27 Mar 2018 in Senate: Yes, Mr. Deputy Speaker, Sir, it is fine with me. view
  • 21 Mar 2018 in Senate: Asante, Bwana Spika wa muda. Ripoti iko sawa isipokuwa mapendekezo yake ndio yalikuwa yanatatiza waheshimiwa Maseneta. Ripoti hii inaeleza kwamba wa kwanza katika majadiliano alikuwa ni Sen. Isack Kipkemboi Melly ambaye alipata alama 78. Ripoti hii inatilia maanani uzoefu wake wa awali. Kwa kizungu inaitwa view
  • 21 Mar 2018 in Senate: Kwa Kiswahili tunasema ‘uzoefu wa awali.’ Kwa hivyo, uzoefu wake wa awali ulitiliwa maanani kwamba alikuwa amefanya kazi kama msimamizai wa maswala ya wanafunzi katika chuo kikuu na pia amekuwa Seneta kwa wa miaka mitano. Ijapokuwa ripoti inasema kuwa ana uzoefu wa awali wa miaka kumi kwa mambo ya fedha ilivyotakikana na Section 5 (2) (b), aliweza kuwashinda wenzake kwa alama tatu. Kwa hivyo, inaonekana kwamba huyu ni mwerevu. Tunaweza kumuita kwa kiingereza genius kulingana na mahojiano yaliyofanyika. Bwana, Spika wa muda, naunga mkono kwamba tubadilishe majina ya Sen. Isack Kipkemboi Melly na Bi. Margaret Sawe wakubaliwe kama washindani kwa ... view
  • 15 Mar 2018 in Senate: Asante sana, Bwana Spika. Swala la SGR ni nyeti sana kwa sababu linaathiri watu kutoka Mombasa mpaka labda Naivasha wakati itakamilika. Ijapokuwa SGR kwa sasa inafanya kazi, kuna baadhi ya watu ambao wameathirika kutoka sehemu ya Mombasa 001 mpaka 020 ambao hawajalipwa ridhaa kwa ardhi zao zilizochukuliwa kwa maswala ya SGR. Vile vile, kuna sehemu ya baharini kule Eneo Bunge la Changamwe ambapo mikoko na miti mingine ya thamani imeharibiwa na mpaka sasa, hakujakuwa na njia yoyote ya kurekebisha madhara kama yale ambayo yametokea kwa mazingira. Kwa hivyo, ninaunga mkono Petition ya watu wa Kajiado. Imekuja kwa wakati mwafaka kwa ... view
  • 15 Mar 2018 in Senate: Asante Bw. Spika. Neno ‘ halumbe’ ambalo Mhe. Seneta wa Makueni amelizungumzia ni ‘Halambe’ kwa lugha ya Kigiriama. Jina la Kiswahili hasa ni ‘halambe.’ Kama alivyotangulia kusema maana ya ‘halambe’ ni kuvuta pamoja. Harambee ilikuja kwa sababu ya matamshi. Kwa mfano, dada yangu pale, Sen. Kihika, anaweza kusema ‘hera’ badala ya ‘hela.’ view
  • 15 Mar 2018 in Senate: Bw. Spika, neno ‘Harambee’ linalotumika katika Coat of Arms halihusiani kamwe na ‘ambe’ambaye anasemekana ni Mungu katika sehemu zingine za dunia. Kwa hivyo nakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Haki, Maswala ya Sheria na Haki za Kibinadamu, kwamba ombi la ndugu Aluoch Polo Aluochier halina msingi na linafaa kutupiliwa mbali. Asante. view
  • 14 Mar 2018 in Senate: Asante sana, Bwana Spika. Swala la SGR ni nyeti sana kwa sababu linaathiri watu kutoka Mombasa mpaka labda Naivasha wakati itakamilika. Ijapokuwa SGR kwa sasa inafanya kazi, kuna baadhi ya watu ambao wameathirika kutoka sehemu ya Mombasa 001 mpaka 020 ambao hawajalipwa ridhaa kwa ardhi zao zilizochukuliwa kwa maswala ya SGR. Vile vile, kuna sehemu ya baharini kule Eneo Bunge la Changamwe ambapo mikoko na miti mingine ya thamani imeharibiwa na mpaka sasa, hakujakuwa na njia yoyote ya kurekebisha madhara kama yale ambayo yametokea kwa mazingira. Kwa hivyo, ninaunga mkono Petition ya watu wa Kajiado. Imekuja kwa wakati mwafaka kwa ... view
  • 14 Mar 2018 in Senate: Asante Bw. Spika. Neno ‘ halumbe’ ambalo Mhe. Seneta wa Makueni amelizungumzia ni ‘Halambe’ kwa lugha ya Kigiriama. Jina la Kiswahili hasa ni ‘halambe.’ Kama alivyotangulia kusema maana ya ‘halambe’ ni kuvuta pamoja. Harambee ilikuja kwa sababu ya matamshi. Kwa mfano, dada yangu pale, Sen. Kihika, anaweza kusema ‘hera’ badala ya ‘hela.’ view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus