Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 2061 to 2070 of 2095.

  • 5 Jun 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, naondoa neno ‘Super Senator’. Nasema Sen. Sakaja ambaye ni Seneta wa Kaunti ya Nairobi. Ni Seneta wa jiji kuu kama vile mimi, Seneta wa Kaunti ya Mombasa na Seneta wa Kaunti ya Kisumu. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, nakubaliana nawe na ninaondoa hiyo. Sina haja ya kuomba msamaha kwa sababu ni jambo ambalo ni zuri kwake. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika. Kwa hivyo, ninasema kwamba maswala yale ambayo yanawakumba ndungu zetu wanaoishi katika vitongoji duni ni maswala ambayo lazima tuyaangalie na tuhakikishe Sheria imetumika sawa sawa katika sehemu zote za Jamhuri ya Kenya. Tumeona kwamba maswala ya ubakaji katika maeneo yale ni maswala ya kawaida. Mimba zisizopangwa na uwaviaji mimba kiholela ni mambo ambayo yanatokea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, ndugu yetu Seneta wa Laikipia angetumia msemo “usipoziba ufa, utajenga ukuta.” Huo ndio ungekuwa msemo mwafaka kwa kumalizia hotuba yake. view
  • 29 May 2018 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, the Committee is not ready to move the Bill. view
  • 29 May 2018 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, we were supposed to have a meeting this morning but it aborted due to lack of quorum. The Chairperson of the Committee is unwell. Only two Senators were in attendance. Therefore, the meeting did not take place. view
  • 29 May 2018 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ya kuunga mkono Hoya ya Sen. (Dr.) Gertrude Musuruve. Kwanza kabisa, Kiswahili ni lugha ya taifa kulingana na Katiba. Ni haki ya watoto wetu wenye ulemavu wa maskio kufunzwa kwa lugha ya Kiswahili. Hiyo ni haki yao ya Kikatiba. Sisi kama Bunge la Seneti tunapaswa kuwahakikishia kwamba haki hiyo inatimizwa. Jambo la pili ni kwamba ukosefu wa mtaala wa Kiswahili kwa wale ambao wana ulemavu wa maskio ina maana kwamba tunawanyima haki yao ya kikatiba kufunzwa kwa lugha ambayo wanaitaka. Katika sehemu nyingi katika Jamhuri ya Kenya, watu wanazungumza Kiswahili kama lugha ... view
  • 17 May 2018 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia mjadala wa kuahirishwa kwa Bunge la Seneti ili tuhudhurie Legislative Summit mjini Mombasa katika Kaunti ya Mombasa. Kama Seneta wa jiji la Mombasa, Kaunti ya Mombasa, nachukua fursa hii kwanza kuwakaribisha nyote katika mji wa Mombasa wakati wa view
  • 17 May 2018 in Senate: Not at all, Madam Temporary Speaker. view
  • 17 May 2018 in Senate: Bi Spika wa Muda, ni lazima tuweze kuzisaidia hizi bunge za kaunti ili wale Wabunge waweze kuchukua majukumu yao kikamilifu; ya kuweza kuangalia raslimali zinazokwenda kule zinafuatiliwa kikamilifu. Tumeona kwamba katika kaunti nyingi Wabunge wale wako tayari kusafiri nje ama safari zingine katika Jamhuri lakini kukaa ndani na kuweza kuuliza maswali magumu yale ambayo yatakikana kuulizwa inakuwa changamoto. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus