All parliamentary appearances
Entries 141 to 150 of 10403.
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
iliyowasilishwa Mezani mwa Bunge la Taifa Jumanne, tarehe ishirini na tisa Oktoba mwaka huu, na kuidhinisha toleo la Kiswahili la Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa, na vilevile kuamua kwamba Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kwa lugha ya Kiswahili zianze kutumika mwanzoni mwa Kipindi cha Nne cha Bunge la Kumi na Mbili. Kanuni za Kudumu ni Standing Orders, Mr. Speaker. Nimesema “Kanuni za Kudumu”. I am just trying to keep abreast.
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Mhe. Spika, nimekuja hapa nikiwa nimejihami vilivyo. Niko na Kamusi ya Kiswahili sanifu ambayo naomba nimpe Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ili ajisaidie nacho nikiendelea na mchango. Najua hatanielewa.
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Kama Bunge la Taifa tumeamua kwamba itakuwa bora tukianza kutumia Kiswahili na Kanuni zetu ziwe kwa Kiswahili. Itatusaidia kuangalia kwamba mambo yatakayo kuja mbele yetu yatatekelezwa kwa haki.
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Mhe. Spika, niko na Kamusi nyingine ambayo nitampelekea ndugu yangu, Kiongozi wa Walio Wachache Bungeni. Nachukua nafasi hii kuwashukuru wale walio jumuika katika kazi hii. Ni kazi iliyofanywa kwa miezi sita. Kuna wafanyikazi wetu hapa waliofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba shughuli hii inafaulu. Pia, nashukuru Ofisi yako Bw. Spika kwa sababu wewe ndiye uliyetenga rasilimali za kuhakikisha kwamba tutakuwa Bunge la pili duniani kuwa na Kanuni za Kudumu zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Wafanyikazi hawa waliweza kutembelea Bunge la Taifa jirani la Tanzania ambalo lina Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili. Ni wao peke yao waliokuwa na ...
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Kiswahili ni lugha maskini. Kwa mfano, jina “ Speaker’’ tunalitoa na kuliita “Spika” badala ya kutafuta neno la Kiswahili litakalotoa tafsiri ya moja kwa moja.
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninawaelewa. Ni vigumu kuelewa lugha ya Kiswahili. Nilivyosema, Kiswahili ni lugha maskini. Kuna misamiati ambayo haipatikani kwa Kiswahili. Ni lazima uazime kutoka kwa lugha ya Kiingereza na utoe, kwa mfano neno " Speaker" ambalo ni la Kiingereza . Tukitafsiri " Speaker" kama "Msemaji" huko ni kupotoka; hicho si Kiswahili sanifu. Tukijaribu kutafsiri, tutapata shida kiasi. Kama ujuavyo, katika Bunge la Kitaifa, tuna Waswahili wa kutosha. Kwa mfano, kuna ndugu yangu niliyeketi naye hapa, ambaye ninashauriana naye. Anaitwa Mhe. Mwashetani. Kuna Waswahili wazuri Bungeni. Tuko na Mhe. Ali, Mjumbe Ali Wario, Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ambaye amejifunza Kiswahili ...
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Aliniambia la! Tutaitafsiri na kusema ni “Nyumba ya maana au ya kifahari” Hivyo ndivyo nitakavyosema. Kuna mambo kadhaa ambayo yataendelea kuwatatiza Wabunge kuyaelewa kikamilifu. Kwa mfano ukiangalia “ Petition ” kwa kawaida tungesema ni “Ombi” Lakini tafsiri yake si “Ombi”
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Nataka nimshukuru Mhe. Millie kwa sababu ameniletea maji. Ameona ninajikaza. Kwa hivyo, ni vyema tuipitishe Hoja hii. Nawaomba Wabunge wenzangu kwamba, katika hali ya
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
samahani, katika hali ya uzalendo, tuchukue nafasi hii leo na tuipitishe Hoja hii haraka ili tuweze kuwasiliana na Wakenya wenzetu kwa urahisi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
-
30 Oct 2019 in National Assembly:
Kwa haya, Mhe. Spika, naomba kuwasilisha hii Hoja na niombe Mhe. Ali Wario awe mwafiki wangu. Ahsante sana, Mhe. Spika.
view