8 Jun 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, Waziri Msaidizi hajalihakikishia Bunge hili kwamba hakuna mfanyakazi atakayeachishwa kazi kwa sababu ya utumiaji wa mashine hizo. Yeye amesema tu kwamba kampuni hizo hazitawaachisha watu kazi. Je, Serikali itahakikisha vipi kwamba hakuna mfanyakazi atakayeachishwa kazi kutokana na kuletwa kwa mashine hizo?
view
7 Jun 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ikichukuliwa kwamba maofisa wa Wizara ya Maji na Unyunyizaji Maji Mashambani, wahandisi na hata masorovea wanadai pesa nyingi sana wakati wanatoa huduma kwa pesa za maeneo Bunge, je, Waziri, maofisa wako wanafaa kulipwa shillingi ngapi ikiwa wanafikiri kwamba pesa za maeneo Bunge si mradi wa Serikali? Kuna taratibu gani ya kuwalipa maofisa hao wakati wanafanya miradi ya pesa za maeneo Bunge?
view
31 May 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, Wizara ina mipango gani halisi ya kukarabati viwanja vyote vidogo vya ndege kote nchini kukiwemo kile cha Voi ambacho ni muhimu sana?
view
31 May 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika nimeuliza hivi: Je, Wizara ina mipango gani ya kukarabati viwanja vidogo vya ndege kote nchini kukiwemo kile cha Voi ambacho ni muhimu sana?
view
31 May 2006 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir. I think the Assistant Minister is further misleading the House. This is a very serious Question. In Taita Taveta, Mwatate and Voi Constituencies which face the same circumstances, teachers are getting hardship allowances. So, is it in order---
view
4 May 2006 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. If the House adjourns today, and I hope it does not, is it in order to request the Office of the President to reverse that situation since it is an emergency?
view
3 May 2006 in National Assembly:
Mr. Deputy Speaker, Sir, how does the Minister justify the existence of these regional authorities? What will the country lose by disbanding them and channelling funds for their purported activities to the relevant Government Ministries?
view
3 May 2006 in National Assembly:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika. Je, ni haki Waziri Msaidizi kulipotosha Bunge hili kwamba anatoa wataalam wa kusaidia jumuia katika miradi ya maji wakati wataalam wake wanadai hela nyingi sana?
view
3 May 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja hii. Ninaiunga mkono nia ya Hoja kikamilifu. Nia ya Hoja hii ni kujaribu kuhakikisha ya kwamba wananchi wetu wamefaidika kutokana na sekta ya kawi. Ikiwa bei ya mafuta ya taa imekaribia bei ya diseli, basi watu wengi wanaotumia mafuta taa wanaumia sana. Watu wengi hutumia mafuta taa sana katika matumizi ya kila siku. Hata hivyo, ni wenye magari ambao wanafaidika kutokana na bei ya juu ya mafuta. Hii ni kwa sababu bei ya diseli na petroli ni karibu sawa na ile ya mafuta ya taa. Nia ya ...
view
27 Apr 2006 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Waziri Msaidizi amesema kwamba atachukua hatua kukabiliana na suala hilo. Tumekuwa na Tume ya Ndung'u kuhusu hayo matatizo. Watu binafsi wamenyakua barabara na sehemu nyingine za matumizi ya umma. Je, mapendekezo ya Tume yatatekelezwa lini? Hiyo ndio hatua kamili!
view