29 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, wakati mwingine tunashindwa kuelewa ni nani hasa ambaye ana jukumu la kukarabati barabara hapa nchini. Kwa mfano, kuna barabara ya kutoka Wundanyi hadi Werugha. Barabara hii ilijengwa na kampuni ya Victory lakini imeharibika. Tunaambiwa kwamba itakarabatiwa, lakini hakuna jambo linaloendelea. Wakati huu watu wa Werugha wameulizwa na Mkuu wa Wilaya na chifu wakusanye mawe ili wairekebishe barabara hiyo. Je, ni nani hasa ambaye anahusika na ukarabati wa barabara ya Wundanyi kwenda Werugha?
view
29 Aug 2007 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika.
view
29 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nampongeza aliyewasilisha Hoja hii. Sehemu za nchi kame ama nusu-kame zina uwezo mkubwa sana. Kile ambacho hatuna ni mipango halisi na utekelezaji wa mipango hiyo. Katika Taita Taveta, kuna chemchemi za Mzima Springs. Ni maji ambayo yanatoka Mlima Kilimanjaro. Tuna madini mengi sana. Tuna mbuga za wanyama pori. Lakini bado Serikali haijatekeleza mipango hiyo. Maji yanatoka sehemu ya Taita Taveta na kumwagika baharini. Sehemu za nyando za chini za Taita Taveta ni nchi kame. Madini ambayo yanaweza kuleta mabilioni ya pesa yako kwa wingi. Lakini hayo mabilioni hayaingii kwa kodi ya wananchi. Yanaenda kutumika kiholela. ...
view
29 Aug 2007 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nami nichangie kidogo kuhusu Hoja hii ya kuongezea pesa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni. Mwanzo, naomba kuunga mkono kwa sababu Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni inachangia sana kiuchumi. Biashara nyingi ambazo zinapatikana katika sehemu ya Uganda na Kanda ya Maziwa Makuu na sehemu zote ambazo ziko karibu na ng'ambo, nyuma yake kuna sera za Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni. Hilo linadhiirika wazi wakati unapotembea nje na kukutana na mabalozi ambao wanakusanya habari na kutupatia. Kwa hivyo, pamoja na hayo, naunga mkono sera ya ...
view
29 Aug 2007 in National Assembly:
na tuwe na vyuo vingi zaidi. Tunaweza kuzipatia nchi zingine kama Burundi, Rwanda, Djibouti, Somalia na hata Sudan scholarships . Hata kama tuna matatizo yetu, tufanye kama Cuba. Wakati tunaendelea kujenga, tunaendelea kutoa. 3576 PARLIAMENTARY DEBATES August 29, 2007 Bw. Naibu Spika wa Muda, baada ya kusema hivyo, nashukuru kwamba watu wamesema tukichagua ubalozi, tusizingatie tu maslahi ya wanasiasa peke yake. Mimi nasikitika kusema kwamba mtu ambaye amestaafu kama Rais, na anapata pension kubwa mno - pesa nyingi kabisa - na ambaye hana matatizo, eti sasa amekuwa mwanadiplomasia wa amani huko Sudan. Tukiangalia rekodi yake ya kuunga mkono udikteta--- Na ...
view
29 Aug 2007 in National Assembly:
wa Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT). Lakini hao ni mabalozi. Kuna akina Shadrack Guto. Hadi sasa, anatumiwa kama Balozi katika Afrika Kusini. Anaheshimiwa sana kwa mambo mengi ya kidiplomasia. Anatumwa hata na Rais Mbeki. Ukienda Namibia na kusini mwa Afrika, Wakenya wengi ndio wanafanya hivyo. Kuna Wakenya wengi ambao ni lazima tuwatambue na kuwapa nafasi kama hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi nafurahi sana na kuipongeza Wizara hii ya Mashauri ya Nchi za Kigeni kwa kufanya uhusiano, hasa na Cuba, kuwa mzuri. Hilo ni jambo nzuri sana kwa sababu nchi ya Cuba ina heshima sana kwa ...
view
28 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, Waziri Msaidizi amesema ya kwamba Serikali haina pesa za kutumiwa na kamati hizi za amani. Lakini Serikali inatekeleza mipango ambayo inahatarisha amani hapa nchini. Wanabuni wilaya bila kuweka mipaka maalum. Ninasikia kuna mpango wa kubuni wilaya mpya kutoka Wilaya ya Taita Taveta ambapo mipaka haijulikani itakuwa wapi. Jambo hili linaleta migogoro na migongano. Bw. Naibu Spika, je, Serikali itapata wapi pesa za kupambana na migogoro inayozusha kwa kubuni wilaya bila kuwa na mipaka maalum?
view
28 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuanza lini hasa? Tarehe gani?
view
22 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, jana nilisema ya kwamba siku hizi kuna taasisi nyingi ambazo zinasimamia maji hadi hatuelewi kazi ya Wizara ya Maji na Unyunyizaji ni August 22, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3339 nini. Je, kulingana na huu mchanganyiko wa taasisi nyingi, Wizara ya Maji na Unyunyizaji inafanya kazi gani au inarushwa hapa na pale na wafadhili?
view
22 Aug 2007 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Swali langu lilikuwa linamuuliza Waziri Msaidizi: Kulingana na vile sasa kuna taasisi nyingi ambazo zinasimamia maji, je ni kazi gani hasa imebaki kwa Wizara ya Maji na Unyunyizaji?
view