Mwandawiro JD Mghanga

Born

November 1959

Post

22812-00400 Nairobi

Telephone

0722316588

All parliamentary appearances

Entries 151 to 160 of 169.

  • 26 Apr 2006 in National Assembly: Bw. Spika, Swali hili ni muhimu sana, na ni lazima lipewe uzito unaostahili. Hivi ninavyozungumza, kuna watu zaidi ya 30 katika mtaa wa Dandora ambao wamekufa mikononi mwa polisi. Je, Serikali inafanya nini kurekebisha hali hii ambapo wananchi wanazidi kupoteza maisha yao mikononi mwa polisi, akizingatia matukio ya mtaa wa Dandora? view
  • 26 Apr 2006 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Spika. view
  • 26 Apr 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ni jukumu la Serikali, hasa Mawaziri, kuhakikisha kwamba kuna umoja wa kitaifa kila pahali. Vile inavyoonekana, umoja wa kitaifa haukuzingatiwa na Wizara ya Afya. Walizingatia maslahi yao ya kibinafsi. Ni makosa sana kufanya hivyo. Je, Wizara ya Afya ina mipango gani ya kuhakikisha kwamba hakuna ukabila wakati inaajiri watu na kwamba, inazingatia umoja wa kitaifa? view
  • 26 Apr 2006 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza nataka kumpongeza Bw. Kimeto kwa kuwasilisha Hoja hii muhimu sana. Hoja hii ina lengo la kutafuta sera halisi za kukabiliana na swala la kutatua usafiri katika nchi hii. Sera ni mipango halisi. Katika karne hii ya 21, ni muhimu kuwa na sera halisi ambazo zinaonekana wazi kitaifa na kimataifa. Inafaa ijulikane kwa kila Mkenya kuwa Serikali hii inalenga kufanya nini kutatua swala la usafiri katika nchi hii. Tukiangalia matatizo ambayo tuko nayo ya usafiri, ni wazi kabisa kuna umuhimu wa sera. Ukiangalia msongamano wa magari katika miji, hasa Mji wa Nairobi, ... view
  • 25 Apr 2006 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 25 Apr 2006 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 25 Apr 2006 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Spika. Uvamizi wa wadudu waharibifu pia umetokea katika sehemu za Wundanyi na nyanda za chini za Wilaya ya Taita-Taveta kwa jumla, na kusababisha upungufu mkubwa sana, na haswa wa mbegu. Je, Waziri Msaidizi anaweza kueleza ni lini mbegu alizoahidi zitatolewa kwa wakulima? Je, ni lini atawapelekea wakulima mbegu hizo? Mvua inaendelea kunyesha na mbegu bado zinahitajika. view
  • 19 Apr 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ninampongeza sana Mbunge ambaye ameliuliza Swali hili. Hii ni kwa sababu mwaka mmoja na nusu, niliuliza Swali kama hili na sikupata jibu halisi. Inaonekana kwamba hakuna mipango halisi ya kukabiliana na tatizo la mitaa ya mabanda katika nchi hii. Je, Waziri ana mipango gani ya kuhusisha Wizara mbalimbali, hasa Wizara ya Fedha, ili atenge pesa za kuboresha mitaa ya mabanda? Zaidi ya robo tatu ya watu wa Nairobi wanaishi katika mitaa ya mabanda. view
  • 19 Apr 2006 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. Swala la usalama ni swali nyeti sana. Waziri Msaidizi anasema kwamba Wizara inajitahidi kuhakikisha kwamba kuna usalama nchini. Kunawezaje kuwa na usalama ikiwa Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi wa CID hawafanyi kazi pamoja? Kabla hamjatatua jambo hilo usalama utadumishwa namna gani? view
  • 19 Apr 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili nichangie huu mjadala nyeti kuhusu usalama. Huu ni mjadala nyeti sana kwa sababu tumewapoteza ndugu zetu tuliokaa nao hapa. Nataka kupendekeza kwamba watu ambao wako upande huo, hasa Mawaziri ambao wanaandika Bajeti na kuleta hapa, wana jukumu kubwa zaidi la kuangalia hayo maneno. Hatuwezi kuwa tunalalamika kila wakati katika Bunge hili. Wengine lazima waonyeshe njia kwa sababu wamepewa mamlaka ya kuwa huko. Tunajua kwamba vyombo vya usalama ni lazima vifanye kazi kwa umoja. Vinapaswa kuzingatia nidhamu zote zinazohusika. Hivi ninavyozungumza, katika Kikosi cha Polisi, inajulikana kwamba Kamishina wa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus