21 Aug 2007 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nitoe maoni machache kuhusu hii Hoja ya Wizara ya Maji na Unyunyizaji Maji Mashamba. Kwanza, nitaungana na wenzangu kuipa pongezi Wizara hii kwa kazi inayoifanya katika taifa lote. Lakini, kule Wundanyi, hatujaona mkono wowote wa Wizara hii. Mbali na kuleta Maswali mengi katika hii Bunge kuhusu Ngilinyi dam, Kakimwaisa Water Project na mradi wa Kishushe, pia kuenda kwa Wizara na barua nyingi ili kuwakumbusha na kumkumbusha Waziri hapa, na hata Waziri kuahidi katika hii Bunge, hakuna hata ahadi moja ambayo imetekelezwa na Wizara hii katika sehemu ya uwakilishi ...
view
15 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Spika, karibu miji yote mikubwa ya Kenya ina chuo kikuu ndani yake ama karibu sana. Je, mji wa Mombasa umekosa kitu gani mpaka sasa hakuna chuo kikuu? Ni mpango gani ambao umefanywa kuanzisha chuo kikuu Mombasa mara moja?
view
15 Aug 2007 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Nimeuliza kuhusu chuo kikuu, na siyo sehemu ya chuo kikuu!
view
15 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, swala hili kuhusu watu wanaopewa kandarasi za barabara ni muhimu na la kitaifa. Nimeshindwa kuelewa uhusiano uliopo kati ya Wizara na wanakandarasi wa barabara. Kandarasi nyingi zinapewa watu ambao hawafanyi kazi. Kwa mfano, barabara ya Thika ambayo Mhandisi Toro anaitumia anapoenda katika eneo lake la uwakilishi la Bunge, imejengwa kwa mwaka mzima ingawa ni kazi ndogo. Kuna barabara nyingine ambayo ilipewa kandarasi kutoka Musau-Windanyi-Verunga; barabara ya Bura. Sehemu ya Mulondo imejengwa na slab na imebomoka kabisa. Wizara inajua jambo hilo lakini haifanyi lolote. Je, wana uhusiano gani na wanakandarasi? Kwa nini mnawaogopa?
view
8 Aug 2007 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono Hoja hii. Hoja hii inaangazia tatizo lenyewe. Lakini swala la msingi ni kuondoa huu mfumo wa ubepari. Nchi hii ni tajiri kabisa. Inaweza kupatia kila mtu elimu ya bure katika shule za upili. Lengo la Serikali hii sasa--- Elimu inaongeza pengo kati ya watoto matajiri na watoto maskini. Tusipobadilisha jambo hilo, hata tukiongeza huu mfuko, tatizo hilo litaendelea. Kwa hivyo, naunga Hoja hii mkono kwa sababu inaonyesha tatizo hilo. Tatizo la msingi ni kupambana August 8, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3031 na sera ya ubepari ambayo imekuwako tangu ...
view
8 Aug 2007 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mimi naomba kuunga mkono hii Hoja ya maana sana. Nasikitika ya kwamba Waziri ya Mipango na Maendeleo na Waziri wa Fedha hawako hapa. Pia, wataalamu kutoka Wizara wa Mipango na Maendeleo na ile ya Fedha hawako hapa. Hii Hoja inalenga kusaili sera za kiuchumi za nchi hii. Imeletwa na mtu August 8, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3035 ambaye alikuwa Waziri wa Mipango na Maendeleo katika nchi hii. Vile vile, imewasilishwa na Dr. Awiti ambaye ni mtaalamu wa maswala ya kiuchumi. Dr. Awiti ana historia kali ya mapambano ya kukomboa hii nchi ili tupate maisha ...
view
25 Jul 2007 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir. Is it in order for the so-called General to purport----
view
25 Jul 2007 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I withdraw and apologise. But for the purpose of this House, the General is sitting on this side and is trying to answer on behalf of the Minister!
view
25 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, wakati ambapo tunazungumza kuhusu plastiki na uchafuzi wa mazingira, kuna tatizo lingine ambalo linaambatana nalo. Tatizo hilo ni mikebe ya plastiki. Kuna bia, soda na bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi ambazo zimepakiwa ndani ya mikebe. Je, Serikali inashughulikia vipi swala hilo, tukizingatia uchafuzi wa mazingira?
view
25 Jul 2007 in National Assembly:
Thank you, Mr. Temporary Deputy, Speaker Sir. First of all, I would like to thank hon. Members for their very enthusiastic contributions to this very important Motion. Indeed, it is a noble idea for any Kenyan leader, including myself, to have unemployed Kenyans recruited in the public or private sector. However, I wish to reply. My response details measures under implementation to create employment and solve the unemployment problem on a sustainable basis. My response urges against passing the Motion moved by the hon. Member. Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir, Kenya has a potential to make rapid progress in employment ...
view