Mwandawiro JD Mghanga

Born

November 1959

Post

22812-00400 Nairobi

Telephone

0722316588

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 169.

  • 25 Jul 2007 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kuniona na kunipa nafasi niunge mkono Hoja hii kwa dhati sana. Kwa sababu sina wakati wa kutosha, nitasema kwa mukhtasari. Mawazo yote ambayo yamesemwa na Waziri Msaidizi hapa ni yale ya kuitazama nchi kupitia mfumo wa ubepari. Tunajua sekta ya binafsi inapata faida sana kutoka na kuimarika kwa uchumi. Ingawa uchumi wetu unakuwa kwa haraka sana lakini nafasi za kazi haziongezeki. Sekta ya umma au ya Serikali ina jukumu la kuwapa wananchi wake nafasi za kazi. Kwa hivyo, Hoja hii ambayo inasinikiza sekta ya Serikali iajiri walimu, waguuzi na wanafanya kazi wengi ... view
  • 25 Jul 2007 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi kuunga mkono hii Hoja ambayo ni ya muhimu sana katika nchi yetu na dunia ya leo. Ningependa kuchukua fursa hii kumpa hongera Bw. Ahenda kwa kuleta Hoja hii wakati huu. Hii ni Hoja iliyofaa kuja katika Bunge hili zamani na tungeokoa maisha mengi ambayo labda yameenda kwa sababu ya kuwa na sheria ambayo ina ruhusu hukumu ya kifo. view
  • 25 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, sababu ya kwanza ambayo imeelezwa na muhimu ni kuwa hukumu ya kifo ni kinyume cha Katiba ya nchi yetu. Sheria inasema kwamba Katiba ndio msingi wa sheria zote. Kwa hivyo, hatufai kuwa na sheria yoyote ambayo inaruhusu hukumu ya kifo kwa sababu inaenda kinyume cha Katiba. Pili, maisha ni haki ya msingi ya binadamu. Tukisema kwamba tunaheshimu haki za binadamu, haki ya msingi kabisa ni haki ya maisha. Kwa hivyo, hukumu ya kifo inavunja haki ya kimsingi ya binadamu na ni muhimu tuiondoe. Tatu, tunajua kwamba binadamu si wakamilifu. Nimekaa gerezani Kamiti mwaka wa 1985 ... view
  • 24 Jul 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. The Minister knows very well - and everybody knows very well - that if you want to sack somebody who is under you, you can use all types of excuses. So, is it in order for the Minister to ask these poor people to appeal before they are reinstated? view
  • 19 Jul 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. Is it in order for successful Ministers of Local Government to continue pretending that they are bringing order in urban areas while they are allowing slums to mushroom everyday? What kind of order are they bringing? view
  • 17 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mabeberu wa Marekani na Uingereza kuilazimisha nchi hii kuwa na sheria ya kibeberu ya ugaidi. Bunge hili limekataa jambo hilo. Jambo hili liko dhidi ya Waislamu. Je, hii ni njama ya kujaribu kuitekeleza hiyo sheria, ambayo haijapitishwa hapa, kwa mlango wa nyuma? Sheikh Mohamed amefanya kosa gani ambalo linasababisha arudishwe Uingereza? view
  • 12 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Spika, tatizo la watu kujeruhiwa hata kuuawa na wanyama wa porini kama vile nyoka, ndovu, simba na fisi ni halisi na linaendelea sana, hasa katika Wilaya ya Taita-Taveta. Je, Wizara ina mipango gani halisi ya kuwafidia watu mara moja wakati wamekumbwa na tatizo kama hilo? Hesabu ya Kshs200,000 hazitoshi kumfidia binadamu ambaye amejeruhiwa na mnyama ama kuuawa? view
  • 12 Jul 2007 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Tangu jana tumekuwa tukipelekwa kizungumkuti na Wizara hii ikisema kuhusu sera au Mswada ambao utaletwa mbele ya Bunge hili. Swali langu lilikuwa halisi. Hivi sasa Wizara ina mipango gani ya kufidia wale watu ambao wamejeruhiwa au kuuawa hata kabla ya sisi kuijadili sera anayoizungumzia? view
  • 11 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Spika, ninashangaa! Huyu Waziri anatoka Mkoa wa Pwani na anaelewa sana kwamba katika mbuga ya wanyama pori ya Tsavo kuna wanyama pori wengi. Watu wa eneo kama Taita-Taveta hawafaidi chochote na huku kando nyama hii inauzwa katika mahoteli. Je tutaendelea kuwaambia watu wetu wachunge hizo kanga ili kutosheleza mahitaji ya mabepari wakati hawapati chochote? view
  • 11 Jul 2007 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Bunge haliwezi kuwa linapotezewa wakati. Tuko na Mawaziri na Mawaziri Wasaidizi. Ikiwa Waziri Msaidizi yuko hapa na hawezi kujibu Swali, ni wazi kwamba wanapoteza wakati wa Bunge! view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus