Mwandawiro JD Mghanga

Born

November 1959

Post

22812-00400 Nairobi

Telephone

0722316588

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 169.

  • 5 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, pasipoti ya Kenya ni lazima iheshimiwe na ichukuliwe kwa uzito unaofaa bila kujali ni mtu gani ambaye anaibeba. Wasomali ni Wakenya. Ikiwa Msomali wa Kenya ambaye ana pasipoti ya Kenya akienda Tanzania anakamatwa na Serikali 2304 PARLIAMENTARY DEBATES July 5, 2007 haiwezi kumlinda, lazima Serikali ichukue msimamo. Je, Waziri anachukua hatua gani ili kuhakikisha kwamba Jamhuri ya Tanzania inahesimu pasipoti ya Kenya, iwe imebebwa na Msomali au mtu gani? Hatutaki watu wetu wabaguliwe na hali hatuwabagui Watanzania ambao wako katika nchi yetu. view
  • 5 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, Mbunge wa Magarini ameeleza kwamba wakati Mhe. Rais alipozuru sehemu yake, aliahidi kwamba hii barabara itawekwa lami. Waziri amemjibu na akasema kwamba halifahamu jambo hilo. Je, Waziri anaweza kwenda kuuliza ili afahamu jambo hilo na akifahamu atekeleze vile Rais aliagiza? view
  • 4 Jul 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. I am also very worried that we are not having Assistant Ministers answering Questions. We have heard about Assistant Ministers' rebellion. In fact, as we speak, some of them are out there, whereas, they can be able to answer Questions like this one. Is this a sign of a rebellion by the Assistant Ministers? view
  • 3 Jul 2007 in National Assembly: Jambo la Nidhamu, Bw. Spika. Mbunge ambaye ameuliza hili Swali anasema kwamba ana hakika kabisa kwamba huu mradi haufanyi kazi, naye Waziri Msaidizi anatueleza kwamba unafanya kazi. Tutamwamini nani? Hawa Mawaziri wanapokea habari kutoka kwa watu wengine mashinani, ilhali hawajafika huko. Tutamwamini nani? view
  • 3 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Spika, kutokana na umaskini miongoni mwa wazazi, baadhi ya wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Nne hawapati vyeti vyao kwa sababu huwa hawajamaliza kulipa karo. Je, Wizara inafanya nini kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata vyeti vyao baada ya kumaliza masomo yao ya Kidato cha Nne? Je, wanafanya nini kuhakikisha kwamba ule mrundiko wa maelfu ya vyeti katika shule za upili umepewa wanafunzi waliomaliza masomo yao ya Kidato cha Nne ili watafute kazi au waendelee na masomo katika vyuo vikuu vya na vyuo vingine hapana nchini? view
  • 27 Jun 2007 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Hoja hii muhimu ya Bajeti. Tangu mwanzo kitu ambacho kimenipendeza zaidi katika hii Bajeti ni kwamba inategemea kidogo sana pesa kutoka kwa wafadhili. Nafikiri tukiwa na huo mwenendo wa kuhakikisha kwamba Bajeti yetu inategemea rasilmali zetu za ndani, nafikiri hapo tutakuwa tunaendelea vizuri sana kwa sababu uchumi wetu hauwezi kuyumbishwa yumbishwa na siasa kutoka kwa wafadhili kutoka nchi za nje. Ni muhimu kwa Serikali, Bunge na Wakenya kwa jumla kutoa sauti kali kabisa kwamba hili deni kubwa ambalo tunabebeshwa na wabeberu iondoke. Serikali yoyote ya Magharibi ambayo ... view
  • 27 Jun 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo, sina budi kuunga mkono. view
  • 27 Jun 2007 in National Assembly: Bw. Spika, inaonekana wazi kwamba tunaimarisha utamaduni wa ufisadi. Ufisadi umetendeka na tunaonyesha Wakenya kwamba mtu anaweza kupasua ardhi ya umma na baadaye akigawa kidogo, tunamhurumia na kuacha ufisadi uliotendeka. Je, huu ni utamaduni wa kumaliza ufisadi? Je, Serikali inakubali kuendeleza utamaduni wa ufisadi? view
  • 26 Jun 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. Given the importance of the Question and that the hon. Member who was to ask it comes from Coast Province, could I ask it on his behalf now that we have very similar problems with regard to this matter and also that the Minister is ready to answer it? view
  • 22 May 2007 in National Assembly: asked the Minister of State for Defence:- (a) whether he is aware that Messrs: Edward Njenge Mwanyika, John Njeru Munene, Joseph Nguku, Silvester Ngatia Kaniaru, and Isack Mutheni Mirongo, who were soldiers serving in the Kenya Army, were unlawfully dismissed from service at Kahawa Barracks in August 2006; and, (b) if he could order their reinstatement. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus