Mwandawiro JD Mghanga

Born

November 1959

Post

22812-00400 Nairobi

Telephone

0722316588

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 169.

  • 9 May 2007 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi kuchangia Mswada huu kuhusu ajira. Kwa kuanza tu ningesema kwamba huu Mswada tumeusubiri kwa miaka mingi sana, kwa sababu sheria nyingi za nguvu kazi ni sheria ambazo zimekuwa za kikoloni. Ingawa Waziri amechelewa katika kuleta Mswada huu Bungeni, haidhuru ni bora kuchelewa kuliko kutokuja. Mambo haya na sheria hii inahusu haki za wafanyakazi; lakini katika mfumo wa ubepari. Kwa hivyo, kutoka mwanzoni, mimi naelewa kabisa kwamba, sio kwamba sheria hii itamkomboa mfanyakazi. Hii ni sheria ambayo itampatia mfanyakazi uwezo wa kupambania haki zake zaidi. Sheria zilizokuwa hapo mwanzoni, zile ... view
  • 11 Apr 2007 in National Assembly: Bw. Spika, Swali hili ni muhimu sana na si la kupuuzwa. Wakati makampuni yanajenga barabara huwa yanajenga kambi. Je, Wizara hii imechukua hatua gani ya kuyashawishi makampuni hayo kuzipatia jamii husika kambi hizo kutumia kama vyuo vya ufundi ama vituo vinginevyo? Wizara hii inafanya nini? Haitoshi kusema tu kwamba watu wayashawishi makampuni hayo. view
  • 11 Apr 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 11 Apr 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 11 Apr 2007 in National Assembly: Mr. Speaker, Sir, is it in order for the Assistant Minister to fail to answer my question simply because I asked it in Kiswahili? I asked him what the Ministry is doing to persuade those construction companies to hand over the camps to the local communities. I asked him that in Kiswahili. view
  • 11 Apr 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, asante sana kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii muhimu sana kuhusu kilimo cha korosho na vita dhidi ya ufisadi. Ninasimama kuunga mkono kabisa Hoja hii. Hii ni kwa sababu baadhi ya watu wangu wa Eneo la Uwakilishi Bungeni la Wundanyi walifanya kazi katika kiwanda hicho kabla hakijanunuliwa na watu binafsi. Wengi wao wanaishi maisha ya shida katika mji wa Kilifi. Bw. Naibu Spika, tukiwa katika Bunge hili hatuwezi kujua ni upande gani wa Serikali au Upinzani. Hii ni kwa sababu hata Mawaziri na Wasaidizi wao hulalamika na kunung'unika kama sisi wa Upinzani. Ikiwa Serikali inaona kuna ... view
  • 10 Apr 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, suala hili limedumu kwa muda mrefu sana. Wakenya wamekuwa na hofu kwamba Serikali ya Kenya inafuata maagizo ya Marekani na marafiki wake walioko Somalia na kwingineko. Je, Waziri anaweza kutueleza alitumia vigezo gani kujua kwamba hawa watu walikuwa wakimbizi au ni raia wa Kenya? Tuna mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi! view
  • 5 Apr 2007 in National Assembly: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. I think we have to be serious in this House. There are many promises which have been made to various constituencies, including Wundanyi Constituency and they have not been fulfilled. Now, the Minister has promised the Member for Mumias Constituency that this project will be implemented in the next financial year. Are we sure that, that promise will be fulfilled? view
  • 5 Apr 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, mimi naomba kumuuliza Waziri kwa ufupi kwamba, katika hayo marekebisho kwa wafanyakazi wa Serikali, je marekebisho hayo yanalenga kupunguza wafanyakazi na kuongeza ukosefu wa kazi ama ni marekebisho ambayo itawapa uwezo wa kutoa huduma bora zaidi na kuwapeleka mahali ambapo wanahitajika? Nchi hii ina ukosefu wa kazi na hatuhitaji marekebisho ambayo yatapunguza kazi. view
  • 3 Apr 2007 in National Assembly: Mr. Speaker, Sir, I beg to ask the Minister of State for Administration and National Security the following Question by Private Notice. (a) Why was Mr. Abdulmalik Mohammed handed over to the USA security forces by Kenyan forces? (b) How many other people have been handed over to the USA by the Kenyan security forces for interrogation outside the country? (c) What is the health and security status of those Kenyans under the custody of USA Government? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus