All parliamentary appearances
Entries 21 to 30 of 1513.
-
6 Oct 2021 in National Assembly:
Ukweli ni kwamba Mkataba huu pia unatia imani ulimwengu mzima kuwa Kenya imefikia kiwango cha kuwezesha ndege kutoka Marekani kuja mpaka huku nchini bila tatizo lolote.
view
-
6 Oct 2021 in National Assembly:
Safari ndefu huanza na hatua chache na safari hii ni safari hakika ni ya kuungwa mkono. Tunaunga mkono Mkataba huu. Tunatakia uhusiano wetu wa Kenya na Serikali ya Marekani kuendelea kuwa na nguvu Zaidi.
view
-
6 Oct 2021 in National Assembly:
Naunga mkono.
view
-
6 Jul 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ni muhimu sisi kujua kuwa sasa hivi watu wengi wanawekwa kwa kikundi kimoja, kuwa kila mtu akitaka damu ni lazima itafutwe kutoka kwa ndugu zake ama majirani na marafiki wakati mtu ambaye ana cheti cha kuonyesha hivi, atakuwa na afueni kuwa amekuwa akitoa damu. Akifika atapatiwa nafasi ya kupata damu bila ya kuulizwa maswali mengi. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, watu wengine wanalipishwa pesa ili damu ipatiwe mgonjwa kwa sababu damu haipo. Hao wenye vyeti ni lazima wapendelewe kidogo. Kama damu ipo na wamekuwa wakitoa damu, ni vizuri. Kwa hivyo, nakubaliana na hilo.
view
-
30 Jun 2021 in National Assembly:
Mhe, Naibu Mwenye Kiti wa Muda, nilitaka tu kuunga mkono. Kuna umuhimu wa washika dau pamoja na umma kuhusishwa kwenye shughuli hizi ili wawe wanaelewa kinachoendelea wakati sheria zinapotengenezwa. Naam.
view
-
30 Jun 2021 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda, nakubaliana na marekebisho hayo. Hatutaki Serikali kuu ikae ikiotea miradi na kuamua kuwa miradi mikubwa inaweza kufanywa wakati wowote ule. Inafaa wananchi na umma wote wajue kuwa mradi fulani utafanywa na Serikali kuu.
view
-
30 Jun 2021 in National Assembly:
Mhe, Naibu Mwenye Kiti wa Muda, nilitaka tu kuunga mkono. Kuna umuhimu wa washika dau pamoja na umma kuhusishwa kwenye shughuli hizi ili wawe wanaelewa kinachoendelea wakati sheria zinapotengenezwa. Naam.
view
-
30 Jun 2021 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda, nakubaliana na marekebisho hayo. Hatutaki Serikali kuu ikae ikiotea miradi na kuamua kuwa miradi mikubwa inaweza kuiotea na kuifanya wakati wowote ule ili wananchi na wanauma wote wajue kuwa muradi ule utafanywa na Serikali kuu.
view
-
17 Jun 2021 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Chairlady, we have heard the sentiments of my colleagues. As we strive to make sure that Parliament is well funded, we usually consider certain things. I also want to remind Members that the figure you see there of Kshs6.6 billion does not involve Senate affairs only, but the Parliamentary Service Commission is also factored in as part of that. Of course, it is a small percentage which is not a lot of money. However, we will make sure that the budget allocation gets better in the next financial year after this coming financial year. Thank you.
view
-
16 Jun 2021 in National Assembly:
Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ya kuzungumzia mjadala huu ambao unahusu sheria ya ugavi wa pesa kwa maeneo 47 ya ugatuzi. Ukweli ni kuwa Wakenya walifurahia sana jambo hili la ugatuzi. Lakini vile muda unavyoenda, ikawa kuwa kwanza, pesa zikifika zinafujwa. Pili, pesa hazifiki kwa wakati unaofaa. Tatu, mara nyingine wanavuka mwaka na pesa zote hazijafika kwenye maeneo ya ugatuzi. Wenzangu wamezungumzia masuala ya wanakandarasi ambao wanadai serikali za ugatuzi kila mahali hapa nchini. Hata Serikali kuu pia inadaiwa kulingana na utendajikazi wa wanakandarasi na pesa kuchelewa kuwafikia. Kilio kipo kila mahali. Kilio kikubwa ...
view