Onesmas Kimani Ngunjiri

Parties & Coalitions

Telephone

0725371937

All parliamentary appearances

Entries 141 to 150 of 192.

  • 16 Dec 2015 in National Assembly: Naelewa kwamba Mswada huu pia utapelekwa kwa Bunge la Seneti na urudishwe hapa na, hivyo basi, tukakuwa na nafasi ya kuuzungumzia zaidi. Ningetaka tu kuwaunga mkono wenzangu waliozungumzia mambo ya kuhifadhi misitu. Katika Serikali ya Rais mstaafu mzee Moi, nilikuwa mwenyeketi wa KANU katika Wilaya ya Nakuru. Wakati huo, misitu yote ilikuwa imefungwa ili watu waweze kulima ndani. Niliweza kunyenyekea kwake na nikajua kitu kimoja. Hakuna wakati juhudi za kuhifadhi misitu zitafaulu bila ya kuwahusisha wananchi. Hapo mbeleni, uharibifu wa misitu ulikuwepo kwa sababu wananchi walifurushwa kutoka kwa misitu. view
  • 16 Dec 2015 in National Assembly: Misitu haiwezi kulindwa kwa njia ya haki bila kuwahusisha wananchi. Ni lazima wafahamu kwamba misitu in mali yao na ni muhimu kuichunga. Siku hiyo nilipata nafasi hiyo na nikawa mtu wa kwanza - kabla nichaguliwe kuwa Mbunge - kurudisha mambo ya kulima ndani ya misitu. Imetufaidi sana kwa sababu Serikali haikuwa na pesa za kupanda miti na kulimia katika misitu. Wananchi wakihusishwa, itakuwa ni jambo rahisi sana. Hata sasa ni rahisi kwa sababu wananchi watapewa sehemu fulani ambako watalima. Kawaida, msitu hufukuza wakulima baada ya miaka mitatu kwa sababu miti ikifika miaka mitatu, hauwezi kupanda kitu kingine ndani. Kwa hivyo, ... view
  • 16 Dec 2015 in National Assembly: Naunga mkono Mswada huu kwa sababu yale tunayoyazungumzia leo hii ni mambo nyeti ambayo tunastahili kusukuma ili yapite. Baada ya wananchi kulima na kupanda miti bila kulipwa, kuna mambo machache ambayo yataleta mabadiliko. Hii ni kwa sababu baada ya wananchi kuilinda miti hiyo, kuna shida ambazo zinawapata. Kuna watu kutoka Nairobi ambao hupewa vibali vinavyowaruhusu kuikata miti hiyo. Wananchi hao hawapewi hata kuni kutokana na mabaki baada ya miti kupasuliwa mbao licha ya kwamba wao ndio walioipanda miti hiyo. Uhusiano wa wakazi na misitu unaanza kuharibikia hapo. Wananchi wakikosa imani na kuona kwamba hawahusishwi kwenye juhudi za kuhifadhi misitu, uharibifu ... view
  • 16 Dec 2015 in National Assembly: Sisi kama Wajumbe tunahitaji kuziendeleza juhudi za kuwafunza wananchi ili wapate kufahamu kwamba hakuna utajiri mkubwa kama misitu. Tukiichunga misitu yetu kwa njia nzuri, tunaweza kuweka nyuki na watatusaidia. Kule kwetu Nakuru, tunapanda pareto ambayo inawawezesha wananchi kupata kiasi kizuri cha pesa kila wiki kutokana na mazao yao. view
  • 16 Dec 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, Mhe. Naibu Spika wa Muda, nimeshukuru. Kama ulivyosema, Mswada huu utapelekwa kwenye Bunge la Seneti alafu urudishwe hapa tena, na tutaendelea kuuangazia. view
  • 16 Dec 2015 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono. view
  • 30 Sep 2015 in National Assembly: Ninashukuru, Naibu Spika wa Muda--- view
  • 30 Sep 2015 in National Assembly: I am sorry. I thought you had finished. view
  • 30 Sep 2015 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru. Yangu yatakuwa machache kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ya Ardhi. Ningependa kumshukuru Mwenyekiti wangu kwa kazi nzuri ambayo amefanya kwa Kamati yetu. Kamati ya Ardhi inafanya mambo yote ambayo inaweza kufanya kuhakikisha kwamba mjadala kama huu kuhusu shamba la Muri umetimia na mambo haya yamemalizikika. Lakini, ningetaka kuweka wazi ili kila mtu aelewe na Serikali ielewe kuwa baada ya Kamati ya Ardhi kumaliza mambo haya yote, shida nyingi zinatokea baada ya sisi kutoa maoni yetu. Shida hutokea baada ya kuanza kuwapatia cheti cha mashamba yao. Hapo ndio watu huingilia na kuuharibu mpangilio ... view
  • 4 Aug 2015 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, nasimama kuunga mkono hii sheria ambayo itabadilisha mjadala huu kwa sababu ni muhimu sana. Watu wengi wameumia kwa miaka mingi. Kwa hivyo ninaunga mkono kwa kusema marekebisho haya ni ya maana na ninamshukuru mwenye kuipendekeza. Wananchi wameumia hata sisi tumekuwa kwa kampuni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus