11 Jun 2013 in National Assembly:
Pili, ni lazima Wabunge waelewe kwamba nchi yetu ya Kenya ina shida ya upungufu wa Kshs102 bilioni. Kwa sababu ya upungufu huo, hatukuweza kuyakidhi matakwa ya kila mtu. Kwa hivyo, tunawasihi ndugu zetu watuwie radhi na wakubaliane nasi kwa sababu tumejaribu sana.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Tatu, sababu iliyotufanya tusiongeze kiasi cha hela zilizotengewa serikali za kaunti ni kwamba hela hizo haziko. Pia, ukiangalia Ripoti ya Auditor-General, utaona The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
kwamba hata yeye hajui jinsi hela zitakavyotumika. Kwa hivyo, alitushauri tuzipatie serikali za kaunti kiasi hicho cha Kshs210 bilioni mwaka huu. Mwaka ujao, tutajua serikali za kaunti zilitumia hela hizo namna gani, na tutawaongeza kukiwa na haja ya kufanya hivyo.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Bw. Spika, hata Mamlaka ya Mpito haijui hela tunazotengea serikali za kaunti zitatumiwa namna gani. Mamlaka hiyo haijui bei za vitu. Haijulikani ni kitu gani kinatakiwa kufanywa. Kwa hivyo, wametushauri tuwapatie Magavana hela walipe mishahara ndiyo waanze kujiandaa kwa miradi watakayofanya. Mwaka ujao, tutaanza kuangalia iwapo kumekuwa na makosa ama la. Mwenyekiti wetu alijaribu sana kutusihi; alituuliza kama ingewezekana kwa serikali za kaunti kuongezewa pesa. Walisema hawakuwa na pesa ambazo wangetumia kwa maendeleo. Kwa ujasiri wa Mwenyekiti wetu, tulikubaliana kuwa hivi karibuni tumwite Waziri wa Fedha, magavana wote and hii Kamati ya Bajeti tuzungumzie vile mwaka ujao pesa zitagawanywa kwa ...
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Mwishowe, ningependa kusema tulitembea Kenya nzima na tulizungumza na wananchi. Na ningependa kukataa kata kata kwamba tulipoenda Kisumu kuna mtu lipiga Kamati yetu mawe. Ningependa kumalizia kwa kusema kwamba tulikaribishwa Kisumu na wananchi walizungumzia kwa ukali mambo ambayo yalikuwa yanawakera ya maendeleo. Walikuwa wanataka Bunge lihakikishe kwamba mwaka ujao, ikiwezekana, Wabunge waondoke Nairobi na kutembelea mashinani ili wananchi wawaambie vile wangependa pesa zao zigawe ili Kenya iwe na maendeleo ya usawa.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Kwa hayo machache, naunga mkono.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Ahsante, Bw. Spika. Nitaiunga mkono Hoja hii, nikitumia lugha ya mama ya Kiswahili.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Ahsante, Bw. Spika. Tafadhali, ndugu zangu, muniwie radhi. Tukiikuza lugha yetu ya Kiswahili, Kenya itakuwa nchi nzuri zaidi.
view
11 Jun 2013 in National Assembly:
Bw. Spika, kwanza, ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu, sisi, kama wanakamati wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, tuliketi pamoja tukakubaliana juu ya Ripoti hii. Hakuna mwanakamati hata mmoja aliyepinga masuala ambayo Mwenyekiti wetu ameyaangazia. Kwa hivyo, ninawasihi wanasiasa wasilete siasa kwa ugavi wa mali humu nchini, na haswa kuhusu masuala ya Bajeti. Kama kuna jambo ambalo walitaka kulizungumzia, wangekuja kwenye ile mikutano iliyoandaliwa washikadau kule mashinani. Wangezungumzia mambo hayo wakati huo. Kwa hivyo, haifai mtu yeyote kusema kwamba hatukufanya vile walivyotushauri tufanye.
view
6 Jun 2013 in National Assembly:
Hon. Speaker, I would like the Leader of Majority Party to explain something. In many countries in the western world and, indeed, in some of our African Countries, within the university campuses, you have governments which have set up security networks or police networks within the campuses which would stop any activity that is illegal within those universities. Some of those governments, other than our Government, have actually set up CCTVs everywhere in those universities so that when any crime takes place, the Government is able to know what happened and how it happened. Would the Leader of Majority Party ...
view