Sara Paulata Korere

Parties & Coalitions

Telephone

0727027937

All parliamentary appearances

Entries 291 to 300 of 416.

  • 24 Aug 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, naomba unilinde dhidi ya hawa mabwenyenye. view
  • 24 Aug 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, naomba unilinde tafadhali. view
  • 24 Aug 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, nataka kuwafahamisha Wabunge wenzangu kwamba nimezoea kelele hata nilikotoka lakini mimi husema ninayotaka kusema. view
  • 24 Aug 2016 in National Assembly: Nasikitika kwa sababu leo nimeketi upande mbaya wa Jumba hili, lakini nitaendelea. view
  • 24 Aug 2016 in National Assembly: Siwezi kuketi chini! Kwendeni huko! view
  • 24 Aug 2016 in National Assembly: Itashika huyu kwanza. view
  • 18 Aug 2016 in National Assembly: Nashukuru, Naibu Spika. Ni kitu cha maana kwamba katika Mswada huu, tumeeleza jinsi ujenzi wa barabara utakavyotekelezwa. Imekuwa taabu kubwa sana hasa kuhusu jinsi ambavyo serikali za kaunti zinajenga barabara. Kwa hivyo, nataka kupongeza Kamati iliyowasilisha Mswada huu. Ni matumaini yetu makubwa kwamba mahali kulikosahaulika kutakuwa na mabadiliko hivi karibuni. Nashukuru. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Shukrani Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti iliyo mbele. Imechangiwa na Kamati ya Pamoja na Uwiano wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mwenyekiti wangu katika Kamati. Ninampongeza. Ni muhimu kuzingatia kwamba, katika Kipengele cha 97, wamezungumzia maswala ya jinsi ya kufurusha watu ambao wamekaa kwa ardhi isiyo yao kihalali. Hili limekuwa swala nyeti sana katika nchi ya Kenya tukizingatia matukio ya mara kwa mara ambapo tumeona wananchi wakifurushwa katika sehemu tofauti tofauti Kenya. Tumeshuhudia dhuluma ambayo wananchi wanapitia wakati wanafurushwa kutoka kwa ardhi. Mara kwa mara, wanaomiliki ardhi hii huambiwa kuwa si yao. Mara nyingi, utapata hii ni ardhi ya ... view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika, ukitazama Ripoti hii ambayo imefanywa na Kamati ya Pamoja, utazingatia kwamba wamebainisha wasiwasi majukumu ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi na Wizara ya Ardhi. Kwa wakati uliopita, tumeshuhudia mizozo kati ya hizi idara mbili ambayo imeathiri utendakazi wao. Kwa hivyo, kupitia Ripoti iliyo mbele yetu, ni matumaini yangu makubwa kuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Wizara ya Ardhi na Tume ya Kitaifa ya Ardhi watatekeleza majukumu yao bila mizozo. Hii Ripoti imengojewa sana na Wakenya, hasa tukizingatia ya kwamba jamii nyingi zimengoja kuona vile tutasuluhisha dhuluma za kihistoria ambazo zimewakumba. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus