27 Jun 2018 in National Assembly:
Kwa hivyo, nimeunga mkono kuondolewa kwa kipengele hicho ndio tukamilishe Ripoti hii muhimu ambayo nchi yetu ya Kenya huenda ikapoteza pesa nyingi.
view
27 Jun 2018 in National Assembly:
Asante sana. Naunga mkono.
view
5 Jun 2018 in National Assembly:
Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Hotuba ya kiongozi wa nchi.

Kwanza, ni kumshukuru kwa sababu aliheshimu Bunge kama eneo la kutafuta uwiano wa kimaendeleo katika Kenya yetu tuipendayo. Mengi yametajwa na Wabunge wakichangia Hoja hii ambayo nimesimama kuunga mkono. La muhimu ni kujua hata kama Kenya inaonekana iko na shida, kuna mengi yamepewa kibao mbele na kuhitimu hasa ile ya uwiano. Najua kama vile wengi wamechangia, nchi yetu ilipitia wingu mbaya sana na likaleta utengano kati ya Wakenya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.

Wakati viongozi, hasa Rais Uhuru Kenyatta na Mhe. Raila Odinga, waliketi na kukubaliana kuleta uwiano katika maendeleo, tulipata nafasi ya kuendelea vyema. Kwa hivyo, tunawashukuru. Ni vizuri sisi viongozi tuwaige ndiyo Kenya yetu iweze kupiga hatua za haraka kimaendeleo.

Lingine la kuvutia ni wakati kiongozi wa nchi aligusia pendekezo la viongozi kuunga mkono ugatuzi. Nchi yetu imeenda njia ya ugatuzi. Nakumbuka alisema ya kwamba kiwango kikubwa cha pesa cha Ksh372milioni kilitengwa cha kuleta usawa kwa ugatuzi katika kaunti ambazo zimewachwa nyuma. Hilo ni jambo la kuonyesha kwamba kiongozi wa nchi anapenda Kenya iendelee katika maeneo yote.