5 Jun 2018 in National Assembly:
Kiongozi wa nchi hakuacha nyuma magonjwa yanayotukumba. Kama vile mnakumbuka, alisema kwamba ugonjwa wa malaria ni janga ambalo lilikuwa linaumiza Wakenya sana. Serikali imechukua hatua na kuona hilo limepungua. Vile vile aliongea juu ya akina mama kujifungua bure. Alitaja kuwa kiasi cha Ksh5.2bilioni kilitumika na kitaendelea kutumika kuona akina mama wanajifungua bure. Hilo ni jambo la busara hasa kwa wanasiasa kwa sababu tunapenda wapiga kura. Kama hatushughulikii wapiga kura, basi tutaumia. Wakati afya ya wapiga kura inadumishwa ni jambo la kuvutia na kupewa kipaumbele.
view

Nakumbuka kiongozi wa nchi aliongea juu ya barabara. Alitaja kuwa Serikali imetenga kiwango cha pesa cha kutengeneza kilomita 10,000 ya barabara. Alisimama mbele yetu akasema tayari wamekamilisha kilomita 3,000. La kuvutia ni wakati aliongea juu ya barabara kutoka Isiolo na kuunganisha nchi yetu na Ethiopia. Kama vile mwenzangu, Mhe. Jonah Mburu, kutoka Lari ametaja, kuna umuhimu mkuu wa kuona nchi ya Kenya inaungana na maeneo mengine ya Africa ndiyo maendeleo, hasa ya biashara na uchumi, yaweze kuenea na kuchukua nafasi iliyochukuliwa na ulimwengu wote.

Ni vizuri kukumbuka kwamba kiongozi wa nchi alitaja maneno yanayohusu utalii. Mungu anapenda Kenya yetu kwa vile hata kama tumeumia kisiasa, alisema tumepiga hatua asilimia 20 kiutalii na inaonekana tukichukua huo mwelekeo wa kuwa na uwiano na kushikamana, tutaenda mbele haraka.

Sitasahau kutamatisha kwa kusema ufisadi uliingia katika Hotuba ya Rais. Alisema asilimia kumi ya pesa imerudishwa na itaendelea kurudishwa tukiiga mwigo wa kupigana na ufisadi.

Nashukuru na naunga mkono Hotuba ya Rais.