Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 421 to 430 of 604.

  • 2 May 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba nami nichukue nafasi hii kutoa mchango wangu juu ya Hotuba ya Rais. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba yake aliyoitoa hapa Bungeni. Ni Hotuba ambayo iliangazia mengi kuhusu maendeleo ya nchi hii. Nikimshukuru Rais kwa yote aliyosema, hata hivyo nina mambo mawili au matatu ambayo naomba yapewe kipaombele. Kwanza ni kuhusu uchumi wetu. Hali ya uchumi wetu unaendelea kuzoroteka. Lakini Rais hakutaja kipengele chochote kuhusu mikakati inayowekwa na Serikali ili kuboresha maisha ya wananchi. Hivi sasa, wananchi wameadhirika sana. Ningependa kuona mikakati ambayo itawasaidia wananchi wasiadhirike zaidi kuliko walivyoadhirika sasa. view
  • 2 May 2012 in National Assembly: Mheshimiwa Rais aligusia ukarabati wa barabara. Alisema kuwa Serikali itaendelea kuzingatia sera za kuboresha barabara hapa nchini na hasa sehemu ambazo zina manufaa zaidi. Swali langu ni hili: Ni sehemu zipi ambazo hazina manufaa? Hata kule tulikuwa tunaambiwa zamani hakukuwa na manufaa na ambapo kulikuwa kumeachwa nyuma kimaendeleo, sasa mafuta yamepatikana. Barabara za huko ni mbaya sana. Hamna barabara zozote ambazo zimekarabatiwa ama kuwekwa lami. Je, hayo mafuta mtayatoa namna gani kutoka kaunti hiyo? Barabara nyingi katika Mkoa wa Pwani ni mbaya sana. Kwa mfano, barabara ya kutoka Voi kwenda Mwatate/Wundanyi ni mbaya sana. Imepewa kampuni ambayo imeshindwa kufanya kazi ... view
  • 2 May 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, Rais alisema anataka usawa wa nchi. Ninamuunga mkono hapa. Tunataka usawa na umoja wa nchi. Wananchi wote washirikiane, kazi ziwe zinapeanwa kwa usawa. Juzi, tuliambiwa kuwa ukabila umekita mizizi katika vyuo vikuu. Watu wa jamii fulani ndio wameajriwa sana. Huu ni ukweli kwa sababu hivi juzi Waziri wa Uchukuzi analiunda Bodi ya Kenya Ports Authority (KPA). Aliweka watu wa jamii moja. Tunaenda wapi kama Waziri anaweza kuweka watu kutoka jamii moja katika Bodi ya KPA jamii moja? Je, watu wa Pwani hawana mtu hata mmoja ambaye amesomea uanasheria? Hawana mtu anayetosha kuwa katika bodi hiyo? ... view
  • 2 May 2012 in National Assembly: Tunataka kujua kwa nini pesa za mbuga ya Tsavo zinachukuliwa na Serikali kuu. Wale watu ambao wako katika maeneo ya mbuga, ni faida gani wanayoipata. Wao ndio wanashughulika kuangalia kuwa wale wanyama wanawalinda vilivyo. Na Bw. Spika wa Muda, nashukuru kuwa katika eneo la Bunge unaloakilisha, tunapakana nawe. Hawa wanyama pia wanakuadhiri. Nina furaha kuwa tutakuwa na Serikali ya Ugatuzi. Huu ugatuzi hautakuwa na maana kama wananchi wenyewe ikiwa hawatafaidika na rasilimali zao. Namshukuru mwenzangu, mhe. Mbunge alitangulia kabla yangu. Amegusia jambo la madini kuwa hivi sasa zile sera zilizoko za ugawaji wa fedha za madini hazisaidii wenyeji. Lililoko hivi ... view
  • 2 May 2012 in National Assembly: Ninashukuru Waziri yuko hapa. Ninatoa mchango wangu uje uone ile reli jinsi mlivyoiacha. Ni mali ya umma na ni mali ya Serikali lakini hakuna mtu ambaye anaiangalia. Imeachwa, watu wafanye wanavyotaka kufanya, wabebe hivyo vyuma na waende waviyeyushe ili wafanye navyo shughuli nyingine. Je, ni nani anayehusika? Hii ni reli ambayo inaweza kutumika kuunganisha Kenya na Tanzania ili tuokoe uchumi wetu. Nikimalizia, jambo la kusikitisha ni kuwa tuna vyuo vikuu vingi ambavyo vimeanzishwa. Lakini katika Mkoa wa Pwani, hatuna hata kimoja ambacho kimesajiliwa sawasawa. Tunazo zile zinaitwa “ constituent colleges” lakini hatuna chuo hata kimoja ambacho kimepewa mamlaka yote katika ... view
  • 19 Apr 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba nitoe mchango wangu kulingana na makadirio ya ziada ambayo yamewasilishwa na Waziri wa Fedha. Bw. Naibu Spika wa Muda, nikiunga mkono Hoja hii, namuomba Waziri wa Fedha kusikiliza ushauri wetu kwa makini. Hii ni kwa sababu ana masikio lakini hataki kusikiliza ushauri wetu. Shida yao kubwa ni kuwa hawazingatii ushauri wowote. Tafadhali Bw. Waziri, fungua masikio yako leo. Bw. Naibu Spika wa Muda, Kamati ya Bunge ambayo inahusika na makadirio ilimshauri Waziri na kumuelekeza vile ambavyo ilionelea makadirio hayo ya fedha view
  • 14 Mar 2012 in National Assembly: Mhe Naibu Spika, natoa shukrani kwa kunipatia muda pia kutoa maoni yangu kwa mjadala huu. Maadamu umeamua kuwa unaufunga, naomba niseme mawili au matatu kwa heshima yako. view
  • 14 Mar 2012 in National Assembly: Naunga mkono uteuzi wa huyu kijana, Boniface Korobe, ili aweko katika halmashauri hii ya maeneo ya uwakilishi bungeni, ili naye apate kutumia taaluma yake ile Mungu amemjaalia na aweze kupeana huduma. view
  • 14 Mar 2012 in National Assembly: Mhe Naibu Spika, CDF imefaidi maeneo mengi sana ya ubunge katika nchi yote nzima; ukiangalia miradi mingi iliyotekelezwa, imetekelezwa na CDF. Hii ni fund ambayo, kusema kweli, imeeneza maendeleo nchi nzima. Shida amayo tunaiona hivi sasa ni kuwa hawa ndugu zetu ambao tunawachagua, ama tuwanapatia mamlaka ya kuweza kutuhudumia wameanza kuzembea kazi. Tunaomba kuwa huu uzembe ukome kwa sababu unafanya ombi lako la fedha lisitekelezwe mara moja; wakitaka stakabadhi hizi, unazipeleka; mara zimepotea; huzipati na miradi mingi katika maeneo mengi ya ubunge inakwama kwa sababu ya uzembe wa hawa maafisa. Naomba kwamba huu uzembe uishe ama upungue. view
  • 14 Mar 2012 in National Assembly: La mwisho, Mhe Naibu Spika, ni kuwa wengi wametoa maoni kuwa tukienda katika ugatuzi, fund hii ipelekwe kwa magavana. Maoni yangu ni tofauti; naomba fund hii ibaki pale ilipo ili Wabunge wapate kuishughulikia na wakamilishe miradi ambayo tunaihitaji hapa nchini. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus