21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, jambo lingine ambalo ningependa kuchangia ni kuhusu bandari huru ambayo inatarajiwa kuwepo baadaye. Bandari hii isije ikavamiwa na makabaila au waporaji ambao wanangojea tu wakati Waziri atakapotangaza, wao watakuwa tayari kuwanyima wenzao haki zao. Ninamwomba Waziri ahakikishe kwamba Mswada huu umeangaliwa kikamilifu.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, jambo la nne ni kuhusu mabaharia. Kama ujuavyo, vijana wetu wengi wameomba kazi na wameingia katika shughuli za ubaharia. Wengi wao wanatupwa majini kama wameingia kwa meli bila ruhusa. Ninamwomba Waziri, vile vile, aangalie kwa ukamilifu ili vijana hawa watendewe haki. Na kama ni ajira, wapewe ajira ya haki. Mara nyingi, meli hizi zinatia nanga katika bandari ya Mombasa na zinatafuta watu wa kufanya kazi kutoka nje na vijana wetu wako hapo na wanaomba ajira.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, jambo la mwisho ni kuhusu umilikaji wa ardhi na maji yetu. Hivi sasa tunaona meli nyingi zinaingia na kufanya vile zitakavyo katika sehemu ya nchi yetu. Ninamwomba Waziri aangalie kuwa nchi yetu inalindwa kutoka ufuo wa baharini Kilindini hadi Lamu. Ni meli ngapi zinaingia hapo kuvua samaki? Tuna njia gani ya kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya nchi inahifadhiwa na kuwa meli yoyote inayoingia humu nchini haipewi kibali cha kuvua samaki inavyotaka, kubeba mali wanavyotaka na kuuza wanavyotaka ilhali watu wa Kenya wanapata taabu?
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, huo ndio mchango wangu kuhusu Mswada huu. Ni matumaini yangu kuwa Waziri ataweka maanani maoni yangu hasa nikiangalia kuwa kampuni nyingi ambazo ziko hapa hivi sasa zinamilikiwa na mafedhuli wa nchi za nje. Tukiangalia watu wanaosafirisha mizigo humu nchini, watu wa Kenya hawajahusishwa kumiliki ama kuwa na hisa katika kampuni hizi za kusafirisha mizigo. Kampuni hizi zimeandikishwa humu nchini na zimekubaliwa kusafirisha mizigo. Ninaomba wakati huu tusikubali kamwe kampuni za meli ambazo zimeandikishwa nje ya nchi hii kuhusika katika usafirishaji wa mizigo humu nchini.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Tujiepushe na janga ambalo tumeliona kwa Wataliano kule Malindi ambapo hata vioski vya kawaida vimekuwa ni vyao. Mkenya akienda kutafuta kioski huko Italia ama Ulaya hatakipata. Lakini humu nchini tumeruhusu mtu yeyote kufanya atakavyo. Ninamwomba Waziri azingatie mambo haya na kuhakikisha kwamba Mswada huu umerekebishwa.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, yangu yamekamilika. Ninaunga mkono Mswada huu.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Naomba, tafadhali, kuzungumzia tu lile jambo lililoletwa na Bw. Jirongo la kubadilisha orodha ya majina. Hao ng'ombe wote wakiibwa wanapelekwa Taita. Wote! Na wamejazana huko! Sisi tunajiuliza: Tuanze kuwaiba na sisi pia? Kwa hivyo, naomba, tafadhali, mfikirie: Kama hoo ng'ombe wote wakiibwa huko juu wanaletwa Taita na wamejazana huko na hakuna mtu yeyote anayeshughulika kuwafuata huko, kwa nini Ja nuary 21, 2009 PARLIAMENTAR Y DEBATES
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
asked the Minister for Higher Education, Science and Technology when he will elevate Mariwenyi Campus to a constituent college of a public university, or to a fully fledged university.
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I would like to thank the Assistant Minister for that answer. Due to the distance from Juja and where the campus is, could he give a specific date as to when it will start functioning independently?
view
20 Jan 2009 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, now that the Assistant Minister says that the campus will start functioning independently from tomorrow, what measures have been put in place, from yesterday to today, to enable it function independently?
view