4 Feb 2009 in National Assembly:
4692 PARLIAMENTARY DEBATES February 4, 2009
view
4 Feb 2009 in National Assembly:
have promised our people that the road will be tarmacked and yet it has never been tarmacked. We want a statement from the Assistant Minister.
view
29 Jan 2009 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, is the Assistant Minister telling this House that a project of that magnitude could be undertaken without a proper feasibility study? Is this not one of the projects that will end up being a white elephant project in Taita?
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, ninaomba kutoa maoni yangu kuhusu Mswada huu ambao umeletwa na Waziri. Yangu ni machache.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Kwanza, ninamwomba Waziri aangalie kampuni za meli ambazo zimeandikishwa humu nchini kwa maana nyingi zao zinasafirisha mizigo. Ninamwomba Waziri aangalie kampuni za meli katika nchi jirani ya Tanzania. Hamna kampuni ya meli inayoruhusiwa kuwa na kampuni nyingine ndogo ndogo za kusafirisha mizigo bila kuwahusisha wenyeji. Ukiangalia katika nchi yetu ya Kenya, utaona kwamba kampuni nyingi za meli zinasafirisha mizigo ndani na nje ya nchi. Je, wananchi wameachwa wapi? Hamna lolote wananchi wanafaidika kutoka kwa kampuni hizi ambazo zinasafirisha mizigo ndani ya nchi.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, Mswada huu haujafafanuliwa wazi wazi. Haibainiki kama Waziri aliuangalia kwa undani. Kama Mswada huu unaweza kurekebishwa, kampuni hizi za meli kubwa kubwa ambazo zina makao yao nje ya nchi hii na mengine humu nchini hazitaruhusiwa kusafirisha mizigo nje ya nchi. Ninamwomba Waziri aangalie jambo hilo.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Jambo la pili, Bw. Spika, ni kuwa kuna kampuni ambazo zinashughulikia meli hapa nchini. Kwa Kizungu, tunaziita shipping agents . Ukiangalia, utaona kwamba zinapewa riba fulani na kampuni za meli. Pia, kampuni hizi uamua kiasi cha pesa ambazo wanalipa kampuni za humu nchini. Ikiwa wataamua kulipa theluthi thelathini, hiyo ndio kodi nchi yetu itapata. Kwa hivyo, inatunyima kodi kwa sababu wakiamua hawatalipa, itakuwa hivyo. Kwa Kizungu, tunaiita transfer pricing . Ninamwomba Bw. Waziri aangalie jambo hili kwa ukamilifu.
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Spika, tumeambiwa kuwa bandari ya Lamu itakuwepo. Hela zinatafutwa ama zipo? Je, watu wa Lamu wamehusishwa na jambo hili? Ni jambo la kufadhaisha moyo kuona vile ilivyofanywa Kilindini. Watu wa Changamwe, Wajomvu na Wadigo walinyimwa haki zao. Je, tunataka kuchukua msimamo huo huo na watu wa Lamu? Je, Pwani itakuwa "inalaliwa" mpaka lini? Ninamwomba Waziri
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
4330 PARLIAMENTARY DEBATES January 21, 2009
view
21 Jan 2009 in National Assembly:
aangalie jambo hili ili ndugu zetu wa Lamu wahusishwe kikamilifu. Kama itabidi Serikali kuchukua ardhi ya watu fulani, basi, walipwe riadha na iwe ya haki na sawa.
view