19 Apr 2011 in National Assembly:
Bi Naibu Spika wa Muda, si mzaha kuongea juu ya Hoja hii kwa sababu ni jambo ambalo linahusu binadamu, wananchi wazalendo na shida walizonazo mashinani. Hata Wabunge walio katika Jumba hili, kunao wenye mali na wengine hawana. Pia, wao wanausikia uzito huu.
view
19 Apr 2011 in National Assembly:
Kwa hivyo, tuweke akili zetu pamoja, ili tutatue tatizo hili. Ukweli ni kwamba bei na gharama ya kununua mafuta imeenda juu na hali ya maisha imekuwa ngumu. Ukweli ni kwamba Waziri alijaribu kupunguza bei ya mafuta jana kwa shilingi mbili na tunajua jambo hili. Lakini ukweli ni kwamba ni sisi wenyewe katika Bunge hili tuliweka sheria za kutoa ushuru wakati wa kuongea juu ya makadirio ya fedha za Serikali. Makosa ni yetu wote katika Jumba hili. Wengine wasijifanye kwamba hawakufanya hilo kosa. Kwa hivyo, lililoko ni sisi wenyewe tukae, tutafakari na tuiangalie Bajeti tuliyoipitisha. Je, Bajeti tuliyoipitisha na nguvu tulizompa ...
view
19 Apr 2011 in National Assembly:
Bi Naibu Spika wa Muda, mimi najua vizuri sana. Ushuru wa juu wa mafuta unatumika kujenga barabara zetu. Mhe. Mbunge, ajiulize ni asilimia ngapi ya ushuru huo unaotumika kujenga barabara zetu.
view
19 Apr 2011 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika Wa Muda, asemayo mhe. Mbunge ni kweli. Lakini gharama ya kununua mafuta kutoka nje imepanda maradufu. Kwa nini sisi hatutaki kutumia kawi inayotokana na makaa. Nchi hii ina tani nyingi za makaa ya mawe ambayo yanaweza kutumika katika viwanda vyetu na kadhalika, badala ya kutumia mafuta. Ni kweli katika Bunge hili, kuna makabaila na mabaradhuli. Watu hawa hawajali maslahi ya wananchi. Watu hawa wanapatikana pande zote za Bunge hili; PNU au ODM. Watu hawa wanajulikana.
view
19 Apr 2011 in National Assembly:
Ni heri tujaribu kuwasaidia wananchi wetu, hasa wale wamekosa chakula. Ni lazima kama Bunge hili kutafakari mbinu maalum za kuweza kuwasaidia watu wetu. Lawama hazitasaidia wananchi wetu kupata unga na baadhi nyingi za kimsingi. Ni lazima tupate suluhu ya janga hili. Mhe. Mbunge amependekeza pesa ziongezwe kwa minajili ya kununua mbegu ili wakulima waweze kupanda, ili tuepukane na njaa siku zijazo. Jambo la pili ni kuhusu ukosefu wa chakula hapa nchi. Wananchi wa sehemu yangu wana chakula za kutosha. Maghala yetu yimejaa mahindi. Kwa hivyo, ningependa Serikali itenge pesa za kutosha za kuweza kununua mahindi kutoka kwa watu wetu. Wakati ...
view
19 Apr 2011 in National Assembly:
Kutoka Mji wa Kehancha hadi Mji wa Migori ni kilomita 28. Lakini watu wetu wanalipa nauli ya Kshs400.
view
23 Mar 2011 in National Assembly:
Bw. Spika, shukrani kwa kunipa nafasi hii ili nitoe usia wangu kuhusu Hotuba iliyotolewa na mhe. Rais kwenye kikao cha jana cha Bunge hili. Nikiitukuza Hotuba hii, kuna jambo moja au mambo mawili nitakayoyazungumzia. Rais alitupa mwongozo kwamba Bunge hili lina jukumu na kazi nzito ya kufanya haswa kupitisha Miswada kadhaa. Alitoa mifano ya Miswada kumi. Unapoiangalia Miswada hiyo, utaona kwamba mingine inarudiana. Miongoni mwa Miswada aliyotaja ni Mswada wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa. Mswada wa nane ni Mswada wa Tume ya Utoaji Haki. Hizo Tume mbili zinazonuiwa kubuniwa kupitia Miswada hii zingewekwa pamoja na kuwa Tume ...
view
23 Mar 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kwenye Katiba mpya, tunasema kwamba Kenya inaheshimu mikataba yote ambayo imefanywa na nchi nyingine pamoja nasi. Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki unasema kwamba mataifa yote wanachama wa Jumuia hiyo yatasoma Bajeti zao wakati mmoja, katika mwezi wa sita kila mwaka. Sisi, Kenya, tumeshaweka kidole na kukubaliana na kipengele hicho. Hivi sasa, mhe. Raila amekuwa akitueleza jinsi tulivyopiga hatua kwenya mambo ya kiuchumi. Tukisoma Bajeti yetu mwezi wa tatu na mataifa mengine wanachama yasome Bajeti zao mwezi wa sita, tutakuwa tumeutupilia mbali Mkataba wa Jumuia ya Umoja wa Afrika Mashariki. Je, itakuwaje? Hilo ni suala ...
view
23 Mar 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia barabara vile ziko Kenya hii, na hiyo imepitishwa barabara zinalimwa, na tunajivunia. Tumepiga hatua. Barabara zimelimwa na hospitali zimejengwa. Lakini sasa nauliza: Mimi kwangu kuna nini? Barabara hizi zimelimwa wapi? Uhuru ni nini? Ikiwa mimi ni mchochezi, basi turudi kizimbani. Serikali ya mseto imekuwa Serikali ya kusetiana. Hakuna mwendo mbele. Ombi langu ni kwamba vigogo hao waonyesha mfano bora, waongoze vizuri na wamewekwa hapo na Mungu. Ninataka waangalie wanyonge ili wasinyanyazwe na kukanyagwa, kwa sababu watakuja kujibu siku za kiama.
view
23 Mar 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu wa Spika, ninakubaliana sana na mawazo ambayo yalitolewa na mhe. Wetangâula, kwamba kuna vipengele ambavyo haviingiani. Ugatuzi utaleta shida. Sura ya nchi italeta shida kubwa; lakini tumepewa nafasi kama Wabunge kukaa na kufikia maafikiano fulani ili kuonyesha Kenya inaelekea wapi, hasa kulingana na mpango wa maendeleo wa mwaka wa 2030. Tunawajibu, sisi kama viongozi, kutoa uongozi.
view