Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 180.

  • 15 Feb 2017 in National Assembly: Shukrani Mhe. Spika. Nachukua fursa hi kwanza kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Kenya kwa kuona umuhimu wa kumteua mama kuwa Mwenyekiti wa Tume inayosimamia ugavi wa rasilimali. Kusema ukweli, hii Kamati ambayo ilimhoji huyu mama waliona ni mama ambaye ana utaalamu na elimu ambayo kati ya wengi na waume walikuwa, akaibuka kwamba ndiye mjuzi kushinda wale wengine wote – kielimu na kiutaalamu. Ameweza kutumikia Serikali na jamii ndani na nje ya nchi. Ni mama ambaye katika wadhifa wake, atasimamia rasilimali zetu na kuona ugavi wa haki na wa usawa katika nchi nzima. Tukiangalia nchi nzima, pia nitoe wito kwake ... view
  • 8 Feb 2017 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Mswada huu ambao ni wa maana sana. Ninalo ombi kwa Waheshimiwa Wabunge kwamba tusikimbie tu kuupitisha Mswada huu bila kurudi nyuma kuufanyia ukarabati kidogo. Kweli tunatetea haki ipatikane upande wetu sisi wanawake, lakini ifahamike kwamba hata sisi wanawake tunachangia hizi shida zingine. Ukiangalia mavazi ambayo tunavaa, yatamfanya huyo mwanamme agutuke nafsi yake. view
  • 8 Feb 2017 in National Assembly: Je, atakuwa amekosea huyo au la? We are provoking problems. Kwa hivyo, katika hii sheria, tuende nayo kwa utaratibu tuweze kurekebisha mpaka katika Katiba. Kwa sababu wakati tunasema mtu anaruhusiwa kuvaa anavyotaka, lakini mtu avae nusu uchi, uwe unategemea nini? Uwe unategemea ufuatwe kwa macho na kwa vitendo. Kwa hiyvo, Mswada huu ni wa maana sana na utaweza kulinda haki zetu pande zote mbili; wanawake na wanaume. Ningependa kusema kuwa hicho kipengele kinachosema kwamba watu wanaweza kujadiliana ili kesi iondolewe, ningeomba wakati mwafaka ukifika tukiondoe. Wanaopatikana na hatia wanafaa kuadhibiwa hata kwa adhabu ya kifo kwa sababu watakuwa wamemharibia mtoto ... view
  • 26 Oct 2016 in National Assembly: Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua fursa hii kuupinga huu Mswada wa rafiki yangu Chepkong’a . Kwanza ninatoa mwito kwa wananchi wa Kenya nikianza na vijana, walemavu na akina mama, Mswada huu siyo wa mwanamke bali ni wa kutuweka katika hali ya usawa wa kijinsia. Leo ni sisi akina mama ndio tunalia, kesho itakuwa wanaume, kesho kutwa vijana na walemavu. Kwa hivyo, akina mama wa Kenya wanalilia Mswada huu kwa sababu mama ndiye mzazi wa kila mtu. Mhe. Chepkong’a na timu yake wanafaa waelewe kwamba ni huyu mama, kijana na mlemavu ndio wamewafanya wachaguliwe kuja hapa Bunge. Walemavu, akina ... view
  • 26 Oct 2016 in National Assembly: Tukifanya hivyo, tutaweza kuokoa hili Bunge lizifedheheke. Tuepukeni fedheha. Huu Mswada ninaupinga vilivyo. Wakenya waungane na sisi tuupinge pamoja. Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 27 Jul 2016 in National Assembly: Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Mheshimiwa usitie wasiwasi. Utapata nafasi maana Kwale na pahali unakotoka ni tofauti. Tena wewe ni mwanaume na mimi ni mwanamke. Kwa hivyo tuko tofauti. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini kwa wakati ambapo tupo katika mashaka makubwa kumaanisha ingefaa ije mapema zaidi ya hivi. Pia, ninampongeza Mhe. Mwadime kwa sababu maji ni uhai. Wakati tunazungumzia maji yaenezwe katika shule zetu, pasiwe kwamba ni shule chache. Haya maji yanahitajika sana haswa tukiangalia hali iliyo katika shule zetu na nikizungumzia sehemu za kwetu. Katika sehemu za Kinangop, Matuga na Lunga Lunga, kuna ... view
  • 22 Jun 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada huu ambao umekuja wakati mzuri. Nasema hivyo kwa sababu utaweza kutufafanulia barabara ambazo zitasimamiwa na Serikali kuu na zile za serikali za kaunti. Hapo awali, kumekuwa na mvutano ambao umesababisha madhara. Kwa mfano, katika eneo langu la Kwale, barabara ni mbovu kabisa. Zaidi ya machungu ni pale ambapo Serikali kuu ilipoamua kutuwekea barabara lami, magavana walienda kortini kuzuia barabara hizo ziziwekwe lami. view
  • 22 Jun 2016 in National Assembly: Kama Wabunge, Mswada huu utatupa mwangaza kutekeleza majukumu yetu ya kuangalia jinsi hela inatumika pande zote mbili - Serikali kuu na serikali za kaunti - kinyume na vile magavana wanavyofikiria kwamba sisi hatupaswi kuchunguza matumizi ya pesa katika kaunti. Mhe. Spika, ni jambo la kusikitisha. Ilifikia kiwango kwamba barabara zetu zilizorota kwa sababu ya mvutano. Tumekuwa tukitetea barabara nyingi zisimamiwe na Wabunge. Kuna mfano mzuri wa matumizi mabaya ya pesa pale ambapo magavana waliamua kuchukua hospitali zote na hivi leo, hospitali hazina madawa. Kunguni tele na watu wanalala watano na wengine wanalala chini. Hivi sasa, wamepewa nafasi ya kusimamia barabara ... view
  • 22 Jun 2016 in National Assembly: kupitia Ndavaya. Hivi sasa, magari yote kutoka Tanzania yanatumia barabara hiyo kwa sababu yanapopitia feri, inachukua siku tatu au nne ndio gari liweze kuvukishwa. Barabara ya Samburu- Kinango-Lungalunga imerahisisha usafiri. Kwa upande wa utalii, barabara hiyo ya Samburu- Kinango-Lungalunga-Kwale inafaa kuwekwa lami wakati huu. Hii ni kwa sababu imekuwa nyimbo tangu enzi ya Rais Mstaafu Daniel Arap Moi. Kila wakati tunaambiwa kwamba lami itawekwa, lakini hatujawahi kuiona. Sasa hivi, tunategemea barabara hiyo kwa utalii. Ikiwekwa lami, itatufungulia utalii ambao umezoroteka katika Kaunti yetu ya Kwale. view
  • 22 Jun 2016 in National Assembly: Barabara iliyo katika eneo la Lungalunga inayoenda Shimoni ni barabara nyingine muhimu. Hivi leo, tunataka bandari ijengwe haraka lakini ikiwa barabara kutoka Kanana hadi Shimoni haitawekwa lami, basi hakutakuwa na maana. Mvua inaponyesha, barabara hiyo haipitiki. Barabara ya kwenda Vanga pia haipitiki mvua inaponyesha. Sehemu hizi ni nzuri sana katika kukuza utalii katika eneo letu la Kwale. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu utatuonyesha mwelekeo ambao utatekeleza mahitaji muhimu ya mwananchi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus