Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 180.

  • 22 Jun 2016 in National Assembly: La ziada ni barabara ambazo zimejengwa kupitia China Road na mashirika tofauti. Wakati umefika upanuzi wa barabara hizo uweke nafasi ya watu wa boda boda . Ajali nyingi za view
  • 22 Jun 2016 in National Assembly: zimetokana na barabara nyembamba na hawajatengewa sehemu zao za kupita. Magari yetu yana michoro kwa sababu zile pikipiki zikipita, zinakwangura gari na ukisema umshtaki, utakuwa unamwonea kwa sababu si makosa yake maana anahitaji kutumia barabara hiyo. Mswada huu utatusaidia. Natumai hakutakuwa na ufisadi katika mpangilio wa ujenzi wa hizo barabara. Ufisadi umetuharibia mipangilio mingi ambayo inasimamiwa na Serikali kuu kumwondolea mwananchi tatizo katika usafiri katika nyanja zote. Kwa hayo, naunga mkono Mswada huu. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Mswada huu utaokoa nchi yetu kutokana na walaguzi ambao wametuharibia mimea yetu ama mbegu ambazo zilikuwa tegemeo la mwananchi tangu abu na abu. Maradhi ambayo yanakumba nchi hii hivi sasa ni maradhi ambayo wakati wa wazee wetu hayakuwa. Kwa mfano, kuna saratani. Saratani na ugonjwa wa Kifua Kikuu ni maradhi ambayo yalikuwa yakishika milango fulani lakini sasa yamekuwa maradhi ambayo yanashika watu ovyo ovyo. Hii inatokana na yale madawa yanayotumika katika kuchanganya mbegu ambazo zinaletwa na wenzetu ambao wanasema kwamba wameelimika zaidi kushida Waafrika. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: Mswada huu utalinda mbegu na mimea yetu, na kulinda tamaduni na desturi zetu kama Waafrika wa Kenya. Miti na mimea ilikuwa ni ya dawa, chakula na kivuli. Hivi sasa, ile mimea tunayoletewa kwa kisingizio kwamba ndiyo mimea bora, imeharibu mazingira. Kwa mfano, huko Kwale, katika sehemu ya Marere, wakati sisi tulipokuwa wachanga, Mto Marere ulikuwa haukauki maji. Lakini, wakati ulipopandwa miti iliyoko sasa hivi, ilikuwa chanzo cha ule mto kukauka mpaka leo. Kuna shida kubwa ya maji katika maeneo yetu. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: Mswada huu utatusaidia kuikuza mimea yetu na kuipatia mapato kwa kuwa tutakuwa tunaelewa mmea huu ni wa aina gani na unaweza kutibu nini ama unaweza kuleta lishe ya aina The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: gani. Katika miaka ya sabini, kule kwetu Shimba Hills, kulikuwa na mzee ambaye alizindua mti ambao ulikuwa ukitibu saratani. Hatukujua ni vipi ilitokea kwa sababu wananchi walishtukia watu wamewasili kwa magari makubwa na kuikata ile miti yote, wakaibeba na kuenda nayo. Wakazi wa sehemu hiyo hawajui ilikopelekwa miti ile. Hakuna faida ambayo huyo mzee na Serikali ilipata. Si ajabu kuwa mti huo unatengeneza madawa ambayo tunauziwa kwa bei ghali na ilhali huo mti ulitoka nchini kwetu. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: Kuna masuala ya vyakula. Ni kweli, Serikali yetu, kupitia Bunge, iliweza kuzuia vile vyakula ambavyo vinatokana na mchanganyiko wa madawa. Ni haki vile vyakula vizuiliwe kwa sababu vimeua hadhi ya vyakula vyetu vya kitamaduni. Ninakumbuka nyanya yangu alifariki akiwa na umri wa miaka 126. Alikuwa anaona na kula nyama na mahindi kwa sababu alikuwa na meno yote. Mtoto wa miaka 35 leo, hata meno yameisha mdomoni kwa sababu ya vyakula ambavyo tunakula. Vyakula vyote viko ndani ya mkebe na vina madawa ambayo hatuyaelewi yametokana na nini. Hii ni hatari kubwa kwa afya zetu. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: Ninaunga mkono Mswada huu kwa maana utalinda hali ya mazingira, utamaduni na mimea yetu. Mswada huu utatusaidia kufanya utafiti kwa maana vyuo vyetu vinatumia rasilimali iliyo katika nchi yetu kukuza taaluma katika kitengo cha kilimo na kulinda mazingira. Ninafurahi na kushukuru kwa sababu tumepata Mswada huu ambao utaweza kuokoa nchi yetu. view
  • 27 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili niweze kuichangia Hoja hii yenye nia ya kuleta usafi kwenya mazingira yetu. Ninaiunga mkono Hoja hii. Kwanza, nampongeza sana Mhe. Ottichilo kwa sababu ni mwanamazingira ambaye huzungumza kuhusu mazingira na anataka kuona vitendo ambavyo vitarekebisha hali ilivyo katika nchi yetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus