Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 180.

  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Hoja hii isiwe tu ndani ya Bunge la kitaifa bali iwe ni sheria mwafaka ambayo itaweza kuiokoa nchi hii. Kabla ya kupitisha Katiba ya Kenya, 2010, tulikuwa na serikali za mitaa. Wakati huo mazingira yalikuwa na nafuu na usafi. Tunazipatia serikali za kaunti pesa nyingi kupitia kwa magavana lakini yasikitisha kwamba kila unapopita wasikia harufu ya uvundo na waona takataka. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hawa tunawaelewa. Ni wale ambao wanawapiga akinamama magongo. Kwa hivyo, hajali afya ya mama. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Ninamshukuru sana Mhe. Ottichilo kwa kuileta Hoja hii. Ni lazima tusimame na afya na mazingira yetu sio kwa kuzungumzia tu bali kwa vitendo pia. Tuitenge siku ambayo itakuwa maalum kwetu sisi sote kwa maana mazingira si jukumu la sehemu moja ama la watu fulani bali ni jukumu letu sisi sote. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Katika utamaduni wa Kiafrika, mama ndiye anayelinda mazingira, kuanzia mzee ndani ya nyumba akioga. Mama ndiye anayehakikisha usafi wa mzee akivaa. Kuna pesa ambazo zimepangiwa kupelekwa kwenye serikali za kaunti kutekeleza majukumu ya usafi wa mazingira na wameshindwa. Ni jukumu letu kama Bunge la kitaifa kuona kwamba pesa hizo zimepatiwa akinamama wawakilishi wa maeneo Bunge. Usafi utaweza kuonekana katika kaunti zetu na kila mahali mtakapopita, mtafurahia mazingira mazuri. Kwa mfano, mazingira ambayo hayana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: takataka, upandaji wa miti na urembo kama vile kupanda maua katika bustani zetu. Hilo ni jukumu ambalo likiachiwa akinamama mtashangaa vile ambavyo Kenya hii itabadilika. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Ninampongeza Rais wetu. Hivi juzi nilikuwa kwenye msafara wake kwenda Ujerumani. Alikaa na wafanyibiashara na wawekezaji ambao wengi wao walikuwa wamelenga kuja Kenya kuhifadhi mazingira kupitia shughuli za kuzoa na kubadilisha takataka ziwe mbolea na umeme. Rais amelitilia jambo hilo maanani. Ni kwa nini sisi kama Bunge tusimuunge mkono Rais wetu na tuweke sheria dhidi ya ukiukaji wa sera ya kulinda mazingira ili watu hao wachukuliwe hatua mwafaka? Hiyo itakuwa hukumu ambayo itaweza kuwafunza watu wetu kulinda mazingira. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Nilitembelea nchi ya Zimbabwe. Usishangae kwa sababu ukipakuliwa chakula katika barabara za Zimbabwe, utakula na hakuna madhara utapata maana kuna usafi wa hali ya juu. Kwa nini Kenya isiwe kama Zimbabwe? Wale ni Wafrika kama sisi. Kwa nini tusiweze kulinda mazingira yetu? Tulipokuwa tukisoma, kila siku ya Ijumaa ilikuwa ni siku ya mazingira katika shule. Hayo mambo yote yametupiliwa mbali. Tujiulizeni ni kitu gani tumekosea ili tuweze kurekebisha na kuyalinda mazingira yetu. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ingia mlango wetu wa Kenya. Nikizungumza hivyo, ninamaanisha wakati unapotoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Moi na kuingia Mombasa. Utakutana na uvundo. Kuna maradhi ambayo hizi sasa yameikumba kaunti ya Mombasa. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeyajali mazingira bali watu wanajali mifuko yao. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Twende katika Kaunti ya kwale. Hapo awali kulikuwa kusafi sana. Hivi sasa kila mahali kuna makaratasi na kinyesi. Wakati umefika Bunge la Taifa lisimame kindete kuokoa mazingira, afya na nchi yetu kwa jumla bila kujali ni nani; tusimame kwa umoja tuamue. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Mhe. Ottichilo, tunaunga mkono siku ya Alhamisi itengwe kulinda mazingira. Sisi sote tuingie kiwanjani na mitaani tusafishe mji wetu. Pia, tuwape nafasi wawekezaji ambao wako tayari kushirikiana na Wakenya kubadilisha zile taka zote ziwe ni vitu vya manufaa. Tukifanya hivyo, tutaleta ajira kwa vijana wetu ambao wanalia hawana kazi. Tukitoa hiyo nafasi bila kuweka vikwazo vingi na kuleta ufisadi, tutaweza kuyaokoa mazingira yetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus