Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 180.

  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pongezi kwa Mhe. Ottichilo. view
  • 14 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninampongeza Rais kwa Hotuba yake iliyokuwa na mwelekeo katika uongozi bora wa nchi yetu. Sisi sote tuko hapa kuwawakilisha wananchi wetu. Ninampongeza kwa sababu Hotuba hii ilizungumzia mambo muhimu katika maisha ya mwananchi kule nyanjani. Kuna watu wachache ambao wanasema barabara hazijaenea. Ningependa kuzungumzia upande wa Kwale. Hata hivi tunavyozungumza, barabara ya Lunga Lunga kuanzia Msambweni inarekebishwa. Barabara hii ilizungumziwa na Rais. Kuna zabuni ambazo ziko tayari na mwezi ujao Rais mwenyewe anaenda kuanzisha mradi wetu wa barabara ya Kinango kuelekea Lunga Lunga ambayo itawekwa lami. Kwa hivyo, upande wa barabara, tunaweza kusema kuwa ... view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu ambao umeweza kufika wakati ambao Wakenya wanateseka. Wakenya hukaa wakiwa na vipeni vyao hususan kina mama ambao wameamka na biashara ndogo. Wanatafuta mahali pa kuwekeza vipeni vyao vidogo ili waweze kupata mkopo waendeleze biashara. Lakini unakuta katika zile benki zetu tunazozitegemea za Serikali, ni vigumu kupata mkopo kwa sababu wanahitajika udhamana wa hali ya juu. Wanapokimbilia hizi benki ndogo ambazo zinabuniwa za kisasa zenye riba ya chini, inafika wakati wanarudi kujuta kama hivi sasa tunalia Chase Bank na Imperial Bank zimefungwa. view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: Katika eneo Bunge langu, kuna mwekezaji ambaye alikuwa ameamua kushirikiana na wananchi katika upande wa baharini ili waweze kuanzisha mradi ambao ungekuwa ni historia katika Afrika wa Well Shark ambao kwa Kiswahili tunamwita Papa Shilingi. Pesa ziliwekwa katika Imperial Bank. Leo hatuelewi kama Imperial Bank itaweza kufufuka ama itakuwa ni vipi. Kwa hivyo, Mswada huu umeletwa kwa wakati unaofaa lakini tunajiuliza Benki Kuu ya Kenya iko wapi wakati benki hizi zinakuja kutapeli wananchi? Banki kuu ya Kenya ndio macho ya mwananchi na Serikali. Mbona wakuu wa Benki Kuu wamenyamaza wakati watu wanatapeliwa? Hakuna hatua ambayo inachukuliwa kwa wale wanaotapeli wananchi. ... view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: Pia, tungependa Bunge hili, kupitia Kamati yetu ambayo inahusika na mambo ya fedha, ihakikishe kuwa Benki Kuu ya Kenya na Waziri wametuelezea ile pyramid scheme ambayo iliwatapeli Wakenya fedha ilienda wapi. Kule Kwale, kina mama na wazee wengi walikufa kwa kiwewe baada ya ile pyramid scheme kuanguka. Tunafaa kujua kufikia leo pesa hizo ziko wapi na ni lini wananchi wetu watarudishiwa pesa zao. Watu walikimbia kuweka pesa kwa wingi kila siku na kila uchao wakifikiria kwamba wakati umefika wa kujinasua katika matatizo waliyo nayo ya kiuchumi. Kumbe walipeleka pesa zao katika midomo ya papa na zilimezwa na mpaka leo hatujui ... view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: Huu Mswada umekuja wakati unaofaa. Bunge hili litaweza kuwanasua wananchi wa nchi hii kutokana na hawa matapeli na hizi benki. Tutaweza kusaidia mwananchi kuona benki zetu, kwa mfano Kenya Commercial Bank (KCB), Cooperative Bank na National Bank, na zitaweka riba sawa. Sijui kama tunaweza kujiuliza ni akina nani ambao huunda zile benki ndio waweze The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: kututapeli. Hili ni swali tunaloliacha mikononi mwa Benki Kuu ya Kenya iweze kutujibu na kuchukua hatua inayofaa ili mwananchi aweze kupata haki yake. Kuna ulanguzi ambao unaendeshwa na zile benki ambazo zinaundwa na zina sauti tamu ya kuwavutia mwananchi ili waende kutapeliwa. view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: Ningeomba kupitia kwako, Mhe. Spika wa Muda, niweze kutoa hizo dakika zangu mbili or tatu ambazo zimebaki kwa Mhe. Mwanyoha ambaye amekaa sana hapa ndani. view
  • 13 Apr 2016 in National Assembly: Ahsante. view
  • 30 Mar 2016 in National Assembly: Shukran, Naibu Spika wa Muda. Ninaiunga mkono Hoja hii inayogusia maisha ya wananchi wetu kule nyanjani. Wakati umefika wa kutambua haki za binadamu. Ni makosa sana kuwa vijana wetu wanapotaka kujisajili kule nyanjani wanaambiwa hawawezi kujisajili kuwa wapigaji kura kwa sababu hawana vitambulisho, bali wana stakabadhi za kungojea vitambulisho. Kuwa na kitambulisho ni haki yetu. Pia, kujiandikisha kama mpiga kura ni haki yetu. Ingekuwa bora kama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka na wizara inayohusika na mambo ya vitambulisho wangeweza kukaa pamoja na kuwa na uwiano kwamba wakati vijana wanapopewa vitambulisho ama stakabadhi za kungojea vitambulisho, waweze kujiandikisha kama wapigaji ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus