Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.
24 Mar 2016 in National Assembly:
Shukrani, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hiyo nafasi ya muda mdogo japo nilikuwa nataka kuwa na muda wa kutosha. Ukweli ni kwamba tungetaka sana kupitisha Mswada huu. Kwa wakati ujao, tungetaka tuwekewe sehemu nyingine inayoonyesha kuwa katika majimbo na zile sehemu ambazo pesa zinakusanywa, ni kiwango kipi cha pesa kimekusanywa ili wakati wanapewa pesa zingine, tuangalie ni vipi tutawapa pesa kwa sababu saa hivi tunatoa pesa ambazo hatuelewi zitatumika vipi. Upande wa unyunyizaji wa maji katika mashamba ningeomba tuweze kusimamia sekta hii iendelee katika Galana kwa sababu ni moja kati ya sehemu ambazo zinaweza kulisha nchi hii.
view
22 Mar 2016 in National Assembly:
Shukrani Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, natoa pongezi kwa Kiongozi wa Walio Wengi kwa kutuletea Mswada huu ambao haugusii jinsia moja tu. Kwa sasa, inaweza kuonekana kana kwamba tunatetea haki ya wanawake pekee. Lakini, tutakuwa tunajitayarisha kwa wakati wowote ikiwa itatokea kuwe na upungufu katika jinsia ya kiume katika mabunge yajayo. Hivyo, watakuwa na sheria inayoweza kuwasimamia na kutoa haki katika nyanja mbali mbali katika maeneo tofauti tofauti yanayosimamiwa na mambo yanayotokana na kuchaguliwa. Mswada huu umekuja kwa wakati unaofaa. Hii ni kwa sababu tusipoupitisha, tutakuwa tumeenda kinyume na Katiba yetu. Hii inaweza kutuletea matatizo. Bunge hili ...
view
22 Mar 2016 in National Assembly:
Kwa hivyo, hatuko kwa kutoa peke yake. Ni nipe, nikupe! Shukrani, Mhe. Naibu Spika.
view
12 Nov 2015 in National Assembly:
Shukrani Naibu Spika kwa kunipa nafasi niweze kuuchangia Mswada huu ambao umekuja kwa wakati unaofaa. Itakuwa bora kwa Bunge kuutilia maanani na kuupitisha haraka iwezekanavyo ili mwananchi aweze kuona faida ya utamaduni wake. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
12 Nov 2015 in National Assembly:
Ukiangalia maisha ya sasa, vile ambavyo vijana wetu wanavyolelewa na vile wanavyoishi, utakuta kwamba tumepoteza hadhi zetu kama Waafrika na kama Wakenya. Mambo mengi ya kitamaduni tumeyaacha na hii imetuingiza katika matatizo makubwa haswa katika upande wa mavazi na vyakula. Mababu zetu wameishi maisha marefu zaidi kuliko sisi kwa sababu waliegemea vyakula vya kitamaduni na matibabu ya kitamaduni. Mavazi yetu ya kitamaduni tumeyawacha kiwango cha kwamba hata katika Bunge letu, tumeshindwa kujionyesha tumetoka katika asilia gani. Wakati umefika wa Bunge kutenga siku maalum ambayo tunaweza kuvaa kitamaduni ili tuonyeshe vizazi vyetu ni kipi kilicho bora katika utamaduni wetu. Kupitia Mswada ...
view
12 Nov 2015 in National Assembly:
lazima kinywaji kile kiweko. Je, leo tunaambiwa tulete makreti ya Tusker . Huo sio utamaduni. Turudini katika utamaduni wetu na tuyavae mavazi yetu ili na sisi tuhesabike katika ulimwengu kuliko vile ilivyo leo. Mpaka hapa ndani ya Bunge ni lazima ujifunge tai na uvae sketi ndio uhesabike kwamba wewe ni Mbunge. Haifai! Tuukuze utamaduni wetu na turudi katika makavadhi yetu. Kupitia Mswada huu, tutaweza kuyalinda yale makaya na kuyakuza mpaka hata watalii wakija, waweze kuyatembelea ili waone utamaduni wetu na wauelewe. Pia, tutakuwa tunawapatia watoto wetu nafasi ya kupata utao na mwongozo kulingana na utamaduni wetu, kinyume na vile ilivyo ...
view
11 Nov 2015 in National Assembly:
Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ninampongeza Daktari Susan kwa Hoja hii ambayo ameileta kwa wakati unaofaa. Tukiangalia hali ilivyo nyanjani panapotokea ajali, tunakuta ni hali ya kusikitisha sana. Tutafaidika tutakapowapatia vijana wetu elimu maalum inayosimamia mambo ya ajali. Kwa mfano, pale kwangu Kwale, kulitokea ajali ambapo mama mmoja ambaye alikuwa ameumia uti wa mgongo--- Kwa vile watu hawakuwa na ujuzi wa kuokoa majeruhi, huyo mama, mwishowe alipoteza maisha yake. Kwa hivyo, hii isiwe tu katika hali ya kuelimisha watu peke The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report ...
view
11 Nov 2015 in National Assembly:
yake. Inatakikana tuwe na magari na vifaa vya kuende unyo kwa unyo panapotokea ajali. Pia, inafaa tuwe na watu wanaojua kuvitumia vifaa hivyo. Tunatoa heko kwa Mama Margaret Kenyatta. Ametuletea zile kiliniki za rununu au
view
11 Nov 2015 in National Assembly:
ambazo zina kila kitu ndani. Lakini hakuna watu ambao wanaujuzi wa kuvitumia. Kwa hivyo, hayo magari pia yamesimama. Wakati tutaweza kuleta hii elimu na zile ambalanzi tulizo nazo ziweze kuwekwa vifaa maalum mle ndani, tutaweza kuwahudumia wagonjwa kabla hawajafika katika hospitali.
view
11 Nov 2015 in National Assembly:
Ninamshukuru Mhe. Dkt. Susana Musyoka kwa kuileta Hoja hii. Asante.
view