Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 180.

  • 28 Oct 2015 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika, nimesimama kulipinga tengenezo badilisho hili ambalo Mhe. Korir amependekeza. Nalipinga kwa sababu hatutaki kuwa tunakaa tukingoja maafa yatokee ili tuyashughulikie. Tunataka tuzuie maafa. Kama itakuwa silaha zifuatiliwe popote zilipo, ni lazima kuwe kumewekwa mikakati. Polisi, jeshi ama kitengo chochote kile cha usalama kinapaswa kuwa na mikakati ya kufuatilia mahali ambako silaha ziko. Hatutaki kungojea mpaka shida itokee ndiyo tuanze kutapatapa. Nina imani kwamba tukiingiza pesa katika hali ambayo imepangiwa na kusitokee mambo ya ufisadi, tutaweza kuokoa maisha ya Wakenya mahali popote walipo, kuliko vile ambavyo hali iko. Hivi sasa, pesa zinatumika lakini haieleweki zinatufaidi vipi, ilhali watu ... view
  • 28 Oct 2015 in National Assembly: ambalo litabadilisha sheria ambayo itatusaidia kuzuia maafa. Tupitishe tengenezo badilisho la kutumika wakati ambapo maafa yametokea. Tukizingatia hali tuliyo nayo katika nchi hii, ni lazima tusimame kidete, kama Waheshimiwa, tutunge sheria ambazo zitamuokoa mwananchi awe salama pahali popote alipo. view
  • 28 Oct 2015 in National Assembly: Kuna watu wengi--- view
  • 28 Oct 2015 in National Assembly: Naendelea Mhe. Naibu Spika. Unaweza kusikia kuwa kuna polisi mahala fulani ambaye amepigwa na kunyang’anywa bunduki--- view
  • 28 Oct 2015 in National Assembly: Niko hapo, Mhe. Naibu Spika. Nalipinga tengenezo badilisho hili. Utapata askari wa polisi amepigwa na kunyang’anywa bunduki. Je, ikiwa bunduki hiyo haitafuatiliwa, tutajua pale itakapoangukia? Kwa hivyo, ni lazima tuwe na mikakati ya kusuluhisha mambo haya. Kwa hayo machache, nalipinga tengenezo badilisho hili. view
  • 14 Oct 2015 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono huu Mswada kwa hicho kipengele ambacho kimeletwa na Mhe. Emanikor kwa sababu tumeonyesha wazi kwamba hili Bunge linasimamia kufadhili Katiba yetu na kukubaliana na yote tuliyopitisha. Lakini pia tutaweza kujitenganisha na wale ambao wanataka kufanya mambo yao wakati sisi tunaendesha mambo yetu katika Bunge hususan kama walivyozungumza Waheshimiwa wenzangu. Wakati ule wa nyuma tuliweza kuona wakituletea nguruwe na hali inajulikana wazi kwamba nguruwe si halali kwa Mwislamu. Walitutia katika hali ambayo haikuturidhisha kama Waislamu katika Bunge na hata Kenya nzima. Kwa hivyo, ninaunga mkono. view
  • 5 Aug 2015 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu kuhusu kubadilisha tarehe ya uchaguzi. Bunge hili linatunga sheria na ni lazima tufahamu kwamba sheria inakata mbele na nyuma kama msumeno. Kwa hivyo, haiwezekani tuliunda sheria ambayo inasema kwamba MCAs na kila anayechaguliwa, awe ni Mbunge, Seneta au Rais, atatumikia kipindi cha miaka mitano na leo, tunataka kuibadilisha. Kwa nini leo iwe hao watu watatu watapunguziwa muda wao na MCAs waachiwe muda wao? Mswada huu unatuletea uwiano ili tuweze kuweka hali ya uchaguzi iwe sawa kwa kila mtu. Pili, ikiwa tutakuwa na uchaguzi katika mwezi wa nane, kwanza, tutakuwa ... view
  • 5 Aug 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, ni vizuri uchaguzi ufanyike katika mwezi wa kumi ma mbili. Kwa mfano, kwetu pwani, kuna wengi ambao walichukua kura zao katika sehemu za bara kwa sababu bara ndiyo kwao. Decemba huwa wamejipanga kurudi kwao ili wapige kura. Huo ndio wakati ambao wanaweza kupata ruhusa ya kurudi katika maeneo yao na waweze kupigiwa au kupiga kura. Kwa hivyo, naunga mkono pendekezo kwamba uchaguzi ufanywa mwezi wa Desemba. Hii haimaanishi kwamba Wabunge watakuwa wameongezewa mshahara. Kusema ukweli, tulichaguliwa na sheria inayosema tutatumika kwa miaka mitano. Kwa hivyo, tukitumika mpaka mwezi wa nane, inamaanisha hata haki yetu itakuwa imekiukwa. Je, kwani ... view
  • 29 Jul 2015 in National Assembly: Shukrani,Mhe. Naibu Spika. Nimesimama kuunga mkono na kumpongeza Mhe. Waluke kwa kuileta Hoja, ambayo inagusia usalama wetu kikamilifu. Serikali huwaajiri watu na kuwapa mafunzo maalum lakini baada ya muda mfupi, watu hao wanaacha kazi na kwenda kuhudumu kwingineko. Hali hii imechangia ukosefu wa usalama nchini, kwa sababu maafisa wanaobakia kwenye kikosi ni wale ambao hawajapata mafunzo yanayohitajika kwenye vitengo tofauti. Kwa mfano, ukiangazia kundi la Recce katika idara ya polisi, utaona kwamba ni maafisa wachache sana ambao hupata mafunzo maalumu. Tunapowahitaji, inakuwa vigumu kupatikana kwa sababu wako katika kambi moja pekee. Kama mafunzo hayo yangesambazwa kwa kila pembe miongozi mwa ... view
  • 29 Jul 2015 in National Assembly: Katika kitengo cha polisi miaka ya nyuma Makamu wa Rais akiwa ni Mhe. Moody Awori, ilitokea kwamba kutakuwa na usimamizi maalum ambao utaweza kubadilisha maisha ya kitengo cha magereza na hata polisi wa kawaida. Lakini, ukiangalia zile nyumba ambazo zilijengwa, nyingi ziko Nairobi na miji mikubwa. Kadhalika, hazimfaidi anayepaswa. Nyingi zimechukuliwa na wale maafisa walio na mishahara mikubwa na katika ngazi za juu. Ofisa anayetumikia katika ngazi ya chini anakuwa mtu anayenyanyasika kimaisha. Ninaunga mkono Hoja hii ikiwa na ukarabati ambao umeletwa na Mheshimiwa mwenzetu. Shukrani Mhe. Naibu Spika. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus