Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 180.

  • 29 Jul 2015 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninasimama kuuzungumzia Mswada huu. Ukiangalia zile hali ambazo tumekuwa nazo wakati wa nyuma kuhusu mambo ya kampuni ambazo zinaweza kupata zabuni tofauti tofauti katika maeneo yetu, utakuta kuwa kumekuwa na unyanyasaji mkubwa. Nikizungumzia upande wa akina mama na vijana, tukianzia hasa katika hali ya mtu kusajili kampuni yake, unakuta kuna sheria nyingi. Ofisi ambazo zinahusika haziko mahali ambapo yule mama ama kijana wa nyanjani anaweza kufika na kupata ile huduma. Pili, inabidi upitie mikononi mwa mawakili. Ukiangalia pesa ambazo wanadaiwa kulipa ili watengenezewe zile stakabadhi ambazo zinatakikana, inakuwa ni malipo ya hali ya juu ... view
  • 29 Jul 2015 in National Assembly: ama Ksh45,000. Je, huyu kijana au mama ambaye anataka kufanya biashara, atakuwa amezitoa wapi pesa hizo ikiwa yeye mwenyewe kwanza hata biashara yenyewe hana? Mswada huu pia utaweza kuturahisishia mambo kwa sababu utaweza kutuwekea mipangilio ambayo mtu ama vijana wakipata zabuni, benki inaweza kuwasimamia kufanya ile kazi kwa njia ya urahisi kuliko vile ilivyo saa hii. Hata vijana wanapopata hizi zabuni inabidi sisi Waheshimiwa tuanze kuenda juu na chini kuhakikisha hiki kikundi cha kina mama au vijana tumewatafutia pesa ili waweze kufanya ile biashara. Itakapokuwa sisi tumekamilisha huu mwongozo ambao tumeutoa kulingana na Mswada huu, tutaweza kuwa tumerahisisha namna ambayo ... view
  • 8 Jul 2015 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu na kumpongeza Mhe. Wamalwa kwa sababu umekuja kwa wakati unaofaa, tukiwa tumebaki na muda mfupi kwenda kutafuta kura tena. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu hali ilivyo sasa katika kila chama - na nitazungumzia upande wa chama changu ili nisizungumzie wengine - kila mwezi mshahara wetu unakatwa. Zile ofisi ambazo zimewekwa mashinani inambidi Mhe. Mwanyoha atoe pesa mfukoni mwake ili azilipie. Unashangaa hizo pesa ziko wapi. Hata kabla pesa hizo kuzungumziwa zaidi, ningetaka Mkaguzi Mkuu wa Fedha ajitokeze waziwazi kukagua matumizi ya pesa hizo kwa sababu hatuelewi. Hakuna wakati ... view
  • 8 Jul 2015 in National Assembly: fulani wakionekana wanashirikiana na upande wa pili, hao ni wasaliti na wanafaa kuadhibiwa. Kwa hivyo, huu Mswada utatusafishia hali ilivyo katika vyama vya kisiasa kwa wakati huu. Pia itatupatia nafasi tuzidi kuongeza vyama. Vyama vikiongezeka humu nchini, demokrasia itaeleweka. Kila mtu atatetea kile chama ambacho anakiona kina msimamo wa kuelekeza mapenzi na uwiano katika jamii zote. Vyama vingi tulivyonavyo leo, tukiwa nje, vinazungumzia uwiano wa jamii. Lakini vikikaa peke yao vinasema: “Ni sisi kama kabila ama nyumba hii.” Hatuwezi kukubaliana na kauli hiyo kwa sababu haielekezi Kenya katika mwelekeo ambao unafaa. Inaelekeza Kenya katika hali ambayo inaleta utata katika jamii. ... view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti hii ambayo imetolewa na Kamati ya Ardhi na pia kuipongeza kwa maana kwa muda tuliokua nao, wameweza kuzunguka katika maeneo mengi wakijaribu kutatua haya mambo ya ardhi. Naiunga mkono hii Ripoti kwa sababu ukiangalia kiundani, utaona kwamba hili eneo la Taita ni moja kati ya maeneo ya Pwani ambayo yamedhulumika sana na mambo ya ardhi. Ikiwa tutaweza kuyafuatilia unyo unyo kama vile ilivyo saa hizi, nina imani tutaweza kuweka roho za wananchi katika hali ya usalama na kuweka roho za wananchi katika imani ya kuamini kwamba walichagua viongozi wanaowajali. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Mambo ya ardhi yamekuwa ni donda sugu sana hususan katika eneo letu la Pwani. Unapoliangalia kiundani utakuta wenyeji hawafaidiki bali ni watu wanaokuja kwa juu. Naishukuru Kamati ya Ardhi kwa maana imeweza kufika katika maeneo ya kwetu Kwale na tuna imani hivi karibuni wataweza kutoa Ripoti kulingana na yale ambayo wameweza kupata katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: eneo la Kwale. Pia, ningependa kuwahimiza viongozi wenzangu katika maeneo ya Pwani tuweze kushikana pamoja na tunapoona matatizo tuyakabili kwa sauti moja ndiposa hii Kamati iweze kuwa na nguvu ya kuweza kuyatatua haya matatizo. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Vilevile, ningependa kuiomba hii Kamati iweze kuangalia kiundani wakati hii ardhi inagawanywa, waweze kujua kama akina mama nao wamepata vipande vya ardhi kwa sababu sisi katika mila za Kiafrika, utakuta akina mama hawana kipande cha ardhi ambacho kinahesabika kwa jina la mama. Kwa hivyo, hii Kamati iangalie wakati ardhi inagawanywa, akina mama pia wapate sehemu za ardhi nao waweze kujivunia kama vile Wakenya wengine wanvyojivunia. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Pia, Kamati ya Ardhi iangalie kwa kina, katika wale ambao wanagawanya ardhi, kuna wengine ambao wanatumia ulaghai. Wanajihesabu kuwa wao ni maafisa wanaokuja kusaidia na kumbe palepale wanajikatia visehemu vyao. Tungependa kuona mkono wa sheria ukifanya kazi ili tuweze kuondoa tatizo hili sugu ambalo limetukabili haswa katika maeneo yetu ya Pwani. Tumeumia na mpaka sasa hatuna cha kujivunia. Hii ni hatari kubwa kwa sababu tumewahi kumwaga damu kwa sababu ya mambo ya ardhi. Hatutaki kuona tena nchi yetu ya Kenya tukipigana kwa sababu ya ardhi. Tunataka tupigane na tumbo, ukosefu wa kazi na mambo ya usalama, lakini siyo kwa mambo ... view
  • 9 Jun 2015 in National Assembly: Shukrani Mhe. Spika. Ninasimama kuunga mkono Ripoti ya hii kamati. Wakati ninaiunga mkono, ningetaka kuzungumzia maeneo tofauti ambayo kusema ukweli kutokana na huu mradi ulivyoanza na kule unapotuelekeza, ni mradi ambao utaleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa nchi hii yetu. Kwanza, ninapongeza huu mkataba kwa sababu umetuletea uwiano baina ya nchi yetu ya Kenya na zile nchi nyingine ambazo zimeingia katika mkataba. Hii ina maana kwamba wananchi katika hizi nchi zote nne wataweza kutembeleana kwa wakati wanaotaka bila kuchelewa hapa na pale kwa sababu ya usafiri. Pili, mradi huu, ukilinganishwa na mingine ambayo Serikali imeanzisha, umeweza kukimbizwa kwa haraka. Huu ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus