Zainab Kalekye Chidzuga

Before joining politics, Zainab was the Coast Province treasurer for Maendeleo ya Wanawake Organisation (MYWO) for more than two decades. At one point, she also served as the chairperson, MYWO Kwale District. International women politicians like Margaret Thatcher, Hillary Clinton and Sirleaf Johnson inspired her to join politics. She is a widow and in seeking elective office, had to overcome many negative cultural beliefs regarding women in leadership.

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 180.

  • 9 Jun 2015 in National Assembly: zinatokana na malori pamoja na mabasi. Mwishowe ni mauti ama majeruhi wengi sana. Lakini tutakapokuwa tunatumia reli, usafiri utakuwa na usalama zaidi. Nne, usafiri wa reli utatusaidia kwa sababu ukiangalia tabia ambayo inaendelezwa na Shirika la Ndege la Kenya, utagundua kwamba shirika hilo halimsaidii mwananchi. Kwa mfano, utafika katika kiwanja cha ndege ukijua utaondoka saa fulani. Mtawekwa pale na kile mtakachosikia ni matangazo tu: “Tunawaomba msamaha.” Lakini wewe ukichelewa kwa sababu pengine ya msongamano wa magari barabarani, ukifika pale unatozwa faini. Hii inamaanisha kwamba hili Shirika haliko pale kutusaidia sisi bali wana mambo yao wenyewe ambayo wanayaendeleza. Tano, mradi huu ... view
  • 26 May 2015 in National Assembly: Shukran, Mhe. Naibu wa Spika. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii na kuipongeza Seneti na pia Kamati za Nyumba zote mbili kwa sababu zimeonyesha uwiano. Nina imani kuwa uwiano huu utaendelea katika Miswada yote ili tuonekane kwamba tunafanya kazi kumsimamia mwananchi apate haki yake kwa pande ya Seneti na Bunge la Taifa lenyewe. Hoja hii imefungua mlango wa ajira zaidi kwa vijana, kina mama na wenzetu waliozaliwa na ulemavu. Hili limekuwa tatizo sugu katika maeneo yetu ya Bunge. Vijana wetu hawana kazi ilhali kandarasi zinatolewa kwa watu ambao si wenyeji wa lile jimbo na watu wetu wanawachwa bila chochote cha kujishikilia. ... view
  • 30 Apr 2015 in National Assembly: Shukrani Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti hii ambayo inasimamia umoja wa uti wa uchumi wa Kenya. Tutakapojenga huo mfereji wa kupitisha mafuta hiyo itakuwa ni njia moja ya kuokoa Wakenya kutokana na ajali nyingi ambazo zinatokana na magari ya kusafirisha mafuta. view
  • 30 Apr 2015 in National Assembly: Pia imeonekana wazi kwamba sharti tuweze kufuata mipangilio ya sheria kwa kuhusisha Mkuu wa Sheria katika mipango ya zabuni za Serikali na miradi tofauti tofauti. Tukifanya hivyo, miradi haitatugharimu sana. Tutaweza kuepuka ule ufisadi mwingi ambao umeonekana ukiingilia miradi mikubwa, ambayo ni ya manufaa kwa nchi hii na kwa mwananchi kwa jumla. view
  • 30 Apr 2015 in National Assembly: Pia kuhusu huu mradi, ninaonelea kwamba tungeweza kuhamazishwa zaidi kuhusu faida ambazo zitatokana na huu mradi. Kwa mfano, tungeweza kusikia kwamba mradi huu utaweza kushukisha bei ya mafuta. Bei ya mafuta imetuumiza sana, hasa tukichukulia, kwa mfano, uwanja wa ndege. Kila wakati tunapoambiwa bei ya mafuta imeshuka, hakuna wakati tunaambiwa kuwa bei ya tikiti ya ndege imeshuka. Badala yake, inaongezeka mara dufu. view
  • 30 Apr 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, katika mradi huu, tuzidi kuangazia vile ambavyo tutaweza kuweka mikakati ambayo itafanya bei ya mafuta iache kupanda kila mara. Hata inaposhuka katika soko ya ulimwengu, tubaki na ile bei ambayo sisi wenyewe tunaweza kuihimili na inaweza kumsaidia mwanchi wa kawaida. Pia, tuwe waangalifu tunapojenga huu mfereji. Je, huu mradi wetu ambao ndio mradi mkuu katika eneo letu la Pwani na unasimamia Kenya nzima ambao ni Kenya Refinery, ni vipi ambavyo tunaweza kuifufua Kenya Refenery ili iwe ndio chanzo cha kuwa na mahala pa kuweka mafuta yetu kuliko vile ilivyo wakati huu? Ule mradi mkuu wa refinery umekufa na ... view
  • 30 Apr 2015 in National Assembly: Ninaunga mkono huu mradi wa pipeline uweze kuendeshwa kisheria. view
  • 23 Apr 2015 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika. Naunga mkono ombi hili kama alivyozungumza Mheshimiwa. Jana tulizungumzia mambo ya ufisadi na tukachukua hatua kulingana na sheria vile ambavyo imetupatia uwezo. Lakini huu usiwe ndio mwanzo ama isiwe ndio tumeishia hapo kwa sababu ukiangalia matatizo yalio katika barabara zetu hususan barabara ya Mombasa, Eldoret mpaka kuvuka mpaka Uganda, barabara zimeharibika vibaya sana. Zimeharibika kwa sababu magari yanabeba uzani zaidi ya vile inatakikana. Unashangaa hivi vituo vya kupima uzani viko katika maeneo mbalimbali, mbona barabara ziharibike na yale magari hupita pale? Inamaanisha kuna mengi ambayo yanafanyika katika vile vituo vya kupima uzani na hakuna hatua inayochukuliwa. Sijui ... view
  • 23 Apr 2015 in National Assembly: Ukiangalia upande wa matatu, matatu nazo tulisema tuwekewe mikanda wakati wa nyuma na ikawekwa lakini hivi sasa hakuna mikanda na ukiangalia vile zinavyobeba, bado tunaharibu mpangilio wetu ambao tulikuwa tumeuweka kisheria na hali tunahesabu kwamba kuna watu wanasimamia maeneo hayo. view
  • 23 Apr 2015 in National Assembly: Tunaomba tuendeleze vita dhidi ya ufisadi. Kama vile Rais wetu alivyojitolea, na sisi pia tujitolee hivyo hivyo ili tuweze kusafisha hali hii ambayo imetuharibia uchumi wetu. Barabara zetu zinahitaji pesa nyingi sana ili zirekebishwe na kuwekwa katika hali ambayo inastahili. Hatuwezi kufikia kiwango hicho ikiwa ufisadi unaotendeka katika vituo vyetu vya kupima mizani hautakabiliwa vilivyo. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus