Zuleikha is grateful that her father’s postings abroad exposed her to a myriad of opportunities, which impacted on her life positively. While studying in South Africa, she recalls that she went through the stages of anger over apartheid. The realization of Zuleikha that one needed to be in politics to influence policy formulation prompted her to join politics. Initially, Zuleikha sought the Kaloleni parliamentary seat but was dissuaded. In parliament she has pushed the government to fund the National Youth Council.
21 Apr 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I rise under Standing Order No. 97 on limiting the time allocated to each Member to contribute. I would like to move that Members have, at least, five minutes each to contribute to this Bill.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Speaker, there have been many women from the Coast region who have been waiting for two weeks up to 6.30 p.m. and none of them has had a chance to contribute.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Speaker, I stand guided.
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi. Nitachukua muda mfupi. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu unapatia wanawake wa hii nchi nafasi ya kujumuika na viongozi wengine katika kufanya maamuzi ya maendeleo ya nchi hii. Tunakumbuka Rais Obama wa Marekani alipokuja nchini alitoa hotuba nzuri sana wa kuunga sheria kama hii mkono. Alitukumbusha kuwa tukiacha wanawake nyuma ni kama timu ya mpira inayochezesha wachezaji nusu. Kutengeneza sheria ili wanawake waongezeke hapa Bungeni ni kitu ambacho kitatufanya sisi kama nchi tusonge mbele kwa pamoja. Kitu kingine, utaona katika dini, mila zetu na maneno ya wahenga, kuna maneno ya ...
view
21 Apr 2016 in National Assembly:
Kitu kizuri kwa huu Mswada ni kusema kuwa wakati wowote kusiwe na zaidi ya theluthi mbili ya jinsia moja katika Bunge la Kitaifa au Seneti. Hii inahakikisha kuwa hakutakuwa wakati ambapo kuna wanaume au wanawake watupu Bungeni kama ilivyokuwa siku zilizopita katika nchi hii. Kitu ambacho nafurahia pia ni kuwa si wanawake tu wamepewa nafasi; ni kwa sababu hivi sasa walioachwa nyuma ni wanawake na sio wanaume. Haitupi tu nafasi ya kuteuliwa kama wanawake watakaochaguliwa, lakini pia imetuwekea kiwango cha miaka 20 kutoka sasa. Tunapewa miaka 20 wanawake wateuliwe na kupata uzoefu wa uongozi wa Bunge ili baada ya hapo ...
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
Shukrani sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Ningependa kuuliza ikiwa ni haki kweli kwa Mbunge huyu kuita Wabunge wenzake watoto wa darasa la kwanza? Ni haki kweli? Je, inaruhusiwa katika Sheria za Bunge?
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangia Mswada huu wa ardhi wa 2015. Ningependa kusema kuwa ninapinga Mswada huu vikali kwa sababu unakiuka Katiba ya Kenya. Kuna Mbunge aliyesimama na kutukosoa Wabunge ambao tunapinga Mswada huu. Alisema kuwa Tume ya Ardhi haiwezi kufanya kazi pekee na ni lazima ifanye kazi na Wizara ya Ardhi. Ningependa kumkumbusha Mbunge huyo kuwa Kipengele cha 249(2)(b) cha Katiba kinasema kuwa: “Tume ya Ardhi ni huru kufanya kazi zake bila kuelekezwa kazi na mtu au shirika lolote lile.”
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Maandiko ya kukumbusha habari katika Mswada huu yanasema kuwa sheria hii inataka kupunguza nguvu za Tume ya Ardhi ili ishughulikie tu masuala ya ardhi za umma lakini Kipengele cha 67(2)(c) cha Katiba kinasema kuwa: “Tume ya Ardhi inapaswa kushauri Serikali kuu kuhusu uandikishaji wa ardhi zote katika nchi yetu.” Katika mambo hayo mawili, sheria hii imekiuka Katiba. Zaidi ya hapo, inapunguza nguvu za Tume ya Ardhi kutengeneza sera za masuala ya ardhi. Kipengele cha 67(2)(b) cha Katiba kimeipa Tume ya Ardhi hii nguvu lakini Mswada huu unaiondoa. Vilevile, Mswada huu unataka kupunguza nguvu za Tume katika kuamua jinsi ardhi za ...
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, Mswada huu umeondoa kazi ya Tume ya Ardhi katika masuala ya kuendeleza kazi za ofisi za masuala ya ardhi.
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Masuala ya dhuluma za kihistoria yamezungumziwa kwa ufupi sana na yanafaa yazungumziwe kwa kinaga ubaga ili tuangalie njia ambazo watu wamekuwa wakidhulumiwa kwa sababu ya ardhi hizo siku zilizopita. Sababu kubwa ya kuleta Katiba hapa nchini na kuibadilisha ilikuwa kuhakikisha kuwa shida zote ambazo tumekuwa nazo kama nchi pamoja na shida za ardhi zimetafutiwa suluhu. Sheria hii inaturejesha pale tulipokuwa kabla ya kupata Katiba - siku za giza na kudhulumiana.
view