GET /api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=143841
HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "count": 1608389,
    "next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=143842",
    "previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=143840",
    "results": [
        {
            "id": 1456602,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456602/?format=api",
            "text_counter": 3992,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "Napongeza pia Kamati hii kwa sababu katika zile Technical and Vocational Education Training Institutes (TVETs), pia wamewekewa bajeti ya vijana. Kwa hivyo, mimi nawaomba vijana kule nje ambao walikua hawana ujuzi, bajeti imewekwa kwenu.Mara hii, sauti zenu zimesikika na mmewekewa bajeti nzuri sana ambayo inaweza kuwasaidia. Na mjitokeze muingie katika TVET na Vocational Training Centres ili muweze kupata taaluma mbali mbali ambayo itawawezesha nyinyi kupata ajira."
        },
        {
            "id": 1456603,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456603/?format=api",
            "text_counter": 3993,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "Nimeona pia katika Blue Economy ama Uchumi Samawati, kama mkaazi wa Mombasa ambaye anatoka sehemu ambayo ina bahari, tumeongezewa Ksh400 million katika ile kandarasi ya Liwatoni ambayo ni ya wavuvi wa samaki, ili waweze kuijenga na kuimaliza kwa sababu ilikua imekwama. Napongeza Kamati ya Bajeti na Makadirio kutukumbuka kama watu wanaotoka sehemu ambazo zina bahari ama uchumi samawati."
        },
        {
            "id": 1456604,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456604/?format=api",
            "text_counter": 3994,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "Mhe. Spika wa Muda, pia nimeangalia katika Rural Electrification and Renewable Energy Corporation (REREC). Inahusu mambo ya stima kuingia mashinani. Tukiangalia sehemu kwa mfano zenye ukame, ni sehemu ambazo hazijafikiwa na maendeleo kama kule ndani ndani Garissa na Ganze. Ikiwa hao wameongezewa pesa za kuweza kufikisha huduma ya stima hadi mashinani, napongeza sana. Ni kitu ambacho kitafanya maendeleo yafike mashinani."
        },
        {
            "id": 1456605,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456605/?format=api",
            "text_counter": 3995,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "Nimeangalia pia katika bajeti ya Ofisi ya Naibu wa Rais. Imepunguzwa, ijapokuwa sikuridhika ilivyopunguzwa. Ni kidogo. Imepunguzwa Ksh100 million pekee yake. Tuliona katika bajeti iliyopita kuwa Ksh600 million iliwekwa katika kurekebisha tu nyumba ambayo ilijengwa na takribani Ksh400 million. Kwa hivyo, ningependa kuomba hii Kamati ya Bajeti na Makadirio The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
        },
        {
            "id": 1456606,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456606/?format=api",
            "text_counter": 3996,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "waweze pia kuangalia jambo hilo. Wakati huu hatutaki kuangalia marekebisho ya manyumba kwa sababu Wakenya wanahangaika sana na Wakenya wanataka kuangalia vitu vinavyopewa kipa umbele, viwe vitu ambavyo vitaboresha uchumi na kushika kandarasi ya kuzalisha ili uchumi uweze kuinuka na ushuru uweze kupungua. Kwa hivyo, katika hiyo pia naomba wazidi kupunguza. Licha ya sekta ya ukulima kuongezewa mgao ili iwawezeshe kukuza vyakula, Kshs100 milioni iliyotengewa Mto wa Nairobi imetolewa. Huu mto hupeleka maji sehemu kubwa za umwagiliaji maji, usafisaji na mambo mengine. Wametoa asilimia hiyo na kupelekwa katika Ofisi ya Naibu wa Rais. Ninaomba Kamati husika wairegeshe kwenye umwagiliaji wa maji katika kilimo maana ulisaidia pakubwa. Mhe. Spika wa Muda, kwenye Kitengo cha Ardhi, wameongeza Kshs750 millioni. Nimefurahi maana wakaazi wa Mombasa na sehemu ya Taita Taveta ambao walipoteza mashamba yao wako kwenye orodha ya wale watafidiwa. Pesa zimeingia sehemu husika. Watoto wetu, Gen.Z, wamefanya kazi nzuri sana. Wameamsha hili Bunge. Wameamsha bongo za waheshimiwa na sasa, zinafanya kazi. Sasa, wanaweka pesa sehemu ambazo zinakusudiwa. Nawapongeza sana. Ule mwamko ulikuwa mzuri isipokuwa waliokuwa na nia mbaya waliingilia kati. Tumepata funzo kama Wabunge na Bunge hili limeamka na kuimarika."
        },
        {
            "id": 1456607,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456607/?format=api",
            "text_counter": 3997,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "Mhe. Spika wa Muda, nimeona pia waalimu wetu wa shule ya Junior Secondary School"
        },
        {
            "id": 1456608,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456608/?format=api",
            "text_counter": 3998,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "(JSS)"
        },
        {
            "id": 1456609,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456609/?format=api",
            "text_counter": 3999,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
            "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
            "speaker": null,
            "content": "waliokuwa hawana mishahara wamepewa bajeti yao na imeongezwa. Nawapongeza. Wengi wao walikuwa wamejitolea kufunza bila malipo. Hawakuwa na mishahara. Wengi walitufuata huku wakilia ili tuwahakikishie kuwa wao pia watapata mishahara kwa kuwatetea Bungeni. Kwa sasa, watapata pesa itakayowasaidia kujimudu kiafya na kusomesha watoto wao. Kuwalipa mshahara kumenifurahisha sana. Limetua mzigo mkubwa mgongoni mwa wananchi. Kuna wakati wazazi ilibidi wachange kitu kidogo ya kuwawezesha waalimu wa JSS kupata kitu ya kujimudu. Sasa, wamepata mgao wao na mambo yao yataenda shwari. Mhe. Spika wa Muda, matibabu ya saratani katika Hospitali Kuu ya Kenyatta yamepunguziwa mgao wao. Ningependa kuwaambia wanakamati kuwa hawangeguza mgao huo. Wananchi wengi wanahangaika maana ugonjwa wa saratani hauchagui tajiri wala maskini. Ninawahisi wauregeshe maana hakuna kitu kizuri kama afya. Mengi wamefanya mazuri na nawapongeza. Naunga Mkono hii S upplementary Budget . Ofisi ya Naibu wa Rais ilikuwa na malimbikizo mengi. Nawasihi wapungunze mgao wao maana hiyo pesa waliotengewa haikuwa inaeleweka kazi yake. Hata kama wamepunguza Ksh100 millioni, nawasihi wazidi kupunguza zaidi. Yote tisa, la kumi ni kuwapongeza kwa kazi yenu nzuri. Tunaomba Nchi yetu ya Kenya iwe na amani. Tuwache vita. Hakutafanyika chochote kusipokuwa na amani. Tutakuwa kama nchi ya Sudan ama mataifa yanayopigana. Tunataka amani katika taifa letu ili tuweze kuyarekebisha yanayotutatiza tukiwa katika Jumba hili. Ahsante."
        },
        {
            "id": 1456610,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456610/?format=api",
            "text_counter": 4000,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "[The Temporary Speaker (Hon. Martha Wangari) left the Chair]"
        },
        {
            "id": 1456611,
            "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1456611/?format=api",
            "text_counter": 4001,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "[The Temporary Speaker (Hon. Peter Kaluma) took the Chair]"
        }
    ]
}