HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=160829",
"previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=160827",
"results": [
{
"id": 1626472,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626472/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa hii fursa umenipa, kuunga mkono Mswada huu wa usawazishaji wa maeneo ya magatuzi, almaarufu Equalization Fund. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono shingo upande kwa sababu yale maeneo 14 ambayo yalitarajiwa yafaidike na hizi fedha yalipanuliwa mpaka yakawa maeneo 34. Historia ya Kenya iko bado bayana ya kwamba tulipopata Uhuru, kuna sera iliyoandikwa na aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Maendeleo, Mhe. Tom Mboya, inaitwa Sessional Paper No.10 of 1965, ilyosema kwamba tumepata Uhuru na saa hii tunajitawala wenyewe, je fedha zetu tutazisambaza namna gani ili Kenya yetu iendelee? Fedha nyingi zilipelekwa maeneo ambayo yana mvua nyingi, na rotuba ya juu, kwa kimombo, highpotential areas . Haya maeneo yalikuwa Mlima Kenya, Bonde la Ufa, Magharibi na Nyanza. Maeneo ya Pwani, Lower Eastern na Northern Frontier District yaliachwa nyuma kimaendeleo kwa sababu rotuba ya huko ilikuwa kidogo na pia mvua ilikuwa chini sana. Bi. Spika wa Muda, wakati wa kuandika Katiba mpya, waandishi wa Katiba wakasema tuache Ibara ya 204 ili tutenge fedha chache za kusawazisha maeneo ambayo yaliachwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ya ile sera ya waka 1965 ama Sessional Paper No.10. Jambo la kushangaza ni kwamba Bunge hili liliunga mkono kuongeza yale maeneo ambayo yangefaidika. Kati ya zile kaunti 14 zinazofaa kufaidika na fedha za usawazishaji wa maeneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo, Taita Taveta ilikuwa mojawapo. Kwa zile fedha za kwanza zilizokuja kwa magatuzi hayo, Taita Taveta ilitumia kutoa maji kutoka laini ya kwanza ya Mzima na maeneo kama Mbulia na Mbololo yakapata maji. Wakati sera hii ilibadilishwa ama sera ya pili kuchapishwa, Taita Taveta imebakia na maeneo mawili peke yake. Moja ni kata ndogo kule Kasighau, ambayo huu mwaka inapata Shilingi 10,300,000. Kuna maeneo mengine ya Taveta, kata ndogo ya Challa, ambayo inapata Shilingi 11,000,000. Kuna swali nauliza kila siku. Wakati tulisema Kaunti ya Taita Taveta haina maji kwa sababu zile pesa zilikuwa zitekeleze miradi ya maji, je, inaonyesha ya kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1626473,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626473/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "maeneo yote yalipata maji? Zile changamoto zilizokuwa zinakumba maeneo mengi ya Taita Taveta kama ukosefu wa maji mpaka leo zipo. Wakati kata ndogo kama Kasighau inapewa Shilingi 11,000,000 ya kutekeleza miradi ya maji, hapo kando kuna maeneo ya Marungu ambayo pia ni kame sana. Hapo karibu kuna maeneo ya Sagala ambayo pia ni kame sana. Ukiangalia kata ndogo ya kule Taveta kama Challa wanapopewa Shilingi 10 milioni za kufanya mradi wa maji, hapo kando kuna wadi ya Mahoho na Mata ambazo hazina maji. Vigezo vilivyotumika katika utafiti na hii Tume ya Commission on Revenue Allocation (CRA) kubaini ni maeneo gani yatakayopata fedha vilikuwa vya aina gani? Kando na maji, fedha hizi zilifaa kutengenezeza barabara. Tangu tupate Uhuru, barabara ambazo zimetengenezwa ni za vichochoroni. Kuna barabara zinaitwa International Trunk Roads, kama hii ya Voi kwenda Taveta. Ile ni barabara inayounganisha nchi mbili. Barabara nyingine iliyotengenezwa Taita Taveta kando na hiyo ni ya kutoka Mwatate kwenda Wundanyi. Barabara nyingine iliyotengenezwa ni kilomita sita ya Bura Mission kwenda Bura Station. Barabara zingine zote, tingatinga huwa zinakuja kufungua mradi halafu zinakimbia. Barabara hizo zinachukua miaka na mikaka kutengenezwa. Kwa mfano, barabara ya Bura-Mughange-Werugha-Wundanyi-Mtoa Magoti, tangu izinduliwe mwaka 2020 mpaka leo, haijaisha ilhali inahitaji Shilingi 2 bilioni peke yake. Bi. Spika wa Muda, tulitazamia ya kwamba tukipata hizi pesa za kusawazisha maeneo ya Kenya, tungezitumia kutengeneza barabara zetu sisi wenyewe. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Mhe. Raila Odinga, siku moja alitumia barabara ya Bura-Mghange- Werugha. Ile barabara ilikuwa mbaya na akasema ni kama ya kuenda jehanamu. Nashukuru kwani mwaka 2020 wakati tulienda kule Ikulu kupigania fedha za Division on Revenue Allocation (DORA), alimwomba Mhe. Rais Uhuru tutengenezewe ile barabara na Mhe. Rais akakubali ingawaje kutekelezwa kwa mradi huo kumekuwa kwa shida. Barabara nyingi za Kaunti ya Taita Taveta ni mbaya. Kama tungegawigwa zile pesa za usawazishaji, tungefanya hiyo miradi ya kuboresha barabara zetu. Taita Taveta ni eneo ambalo udongo wake uko na rotuba nyingi lakini shida ni maji. Iwapo Kenya inataka kuongeza utajiri kupitia kuuza bidhaa ng’ambo, basi, tungeangazia ile milioni moja ya mashamba ya Taita Taveta ya range land . Tungetumia hela hizo kulisha ng’ombe na mifugo na kuuza ng’ambo kwa kuwekeza tu kwa miradi ya maji. Challa, Njoro na Mzima kuna maji mengi. Tungefanyiwa mradi wa kuleta maji ili yatumike kwa ukulima wa unyunyiziaji wa mashamba, tungekuwa na nyasi nyingi za kuuza mpaka ulaya, lakini miradi hiyo haijafanyika. Fedha kama hizi za kusawazisha maeneo mbalimbali ya Kenya ni muhimu kufanya miradi kama hiyo. Bi. Spika wa Muda, Taita Taveta ina maji mengi sana. Kuna Mzima II ambayo inasambaza maji kuanzia Kaunti ya Taita Taveta, Kwale, Kilifi hadi Mombasa. Tungepata fedha kama hizi, tungezitumia kufanya miradi kama hiyo. Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya mradi wa Mzima II kutotekelezwa, leo hii tunasikia kuna mabwenyenye, watu wasioeleweka, wamechukua maji Kutoka Mzima II kwa kutumia Line 1 ya Kenya Pipeline Corporation (KPC). Sijui wanayatumia kufanya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1626474,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626474/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "nini, lakini ni jambo la kuhuzunisha. Ni jambo la kuudhi kwamba tunaweza kutoa maji Taita Taveta kupatia watu wengine, ilhali watu wa Taita Taveta hawana maji. Kaunti ya Taita Taveta imewachwa kimakosa kwa hizi pesa za usawazishaji wa maeneo kiuchumi. Nikiangalia majirani wetu wote, kuanzia na jirani wa kwanza, Kaunti ya Kilifi, inapata Shilingi 878,000,000. Jirani mwengine ni Kaunti ya Kitui ambayo inapata Shilingi 646,000,000. Jirani mwengine ni Kaunti ya Kwale, ambayo inapata Shilingi 475,000,000. Eneo Bunge moja la Kinango, ambalo tumepakana upande wa Macknon Road, linapata Shilingi 265,000,000. Kaunti ya Kajiado pia ni jirani yetu na inapata Shilingi 674,000,000. Kaunti ya Tana River ambao pia ni jirani yetu inapata Shilingi 719,000,000. Ninachojiuliza ni: Je, ni vigezo gani vinavyoonyesha kwamba Kaunti ya Taita Taveta haihitaji pesa za kusawazisha maeneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo hadi inapewa Shilingi 21,000,000 pekee? Hilo ni jambo la kutamausha, kuudhi na kufisha moyo. Watu wa Taita Taveta hawajisikii kama wako Kenya. Nafikiri ni kwa sababu ni watu wachache mno, ndio maana watu wanaona kwamba hawafai sababu kura yao siyo nyingi. Wakati wa kupeana pesa za kusawazisha maeneo yaliyowachwa nyuma kimaendeleo, wakaona hawafai maana hawana kura. Kando na kuwa tuko wachache, hatuna maji, barabara na vituo vya afya wala stima. Kero la wanyama pori ni kitu kingine ambacho Serikali ya Kenya imekataa kuangazia kabisa. Hao watu wameachwa nyuma kimaendeleo, hawana mtetezi, hawajui watajisaidia namna gani na katika bidii yao ya kulima, kufuga mifugo kama mbuzi, ng’ombe na kondoo, Wanyama pori kama simba na chui wanawala wanyama wao. Ndovu wanamaliza chakula chao. Kama kungekuwa na njia, kule Taita Taveta - sisi tunapakana na Tanzania – tukatiwe eneo letu twende Tanzania. Hii ni kwa sababu haifai tena, haina maana tena kusikia kwamba sisi ni Wakenya lakini yale madhila na shida tunazopata kama Wakenya ziko vile zilivyo."
},
{
"id": 1626475,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626475/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi. Spika wa Muda, sipendi kuendelea zaidi ya hapo lakini ningeomba Kamati ya Seneti ya Fedha na Bajeti, wakati wa sera ya tatu ya kugawanya hizi fedha za kusawazisha maeneo yalioachwa nyuma kimaendeleo, basi tuangalie ili watu wa Taita na Taveta waangaziwe ili ---"
},
{
"id": 1626476,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626476/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Veronica Maina",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": " Sen. Sifuna, do you have an intervention? Point of information? Would you wish to be informed?"
},
{
"id": 1626477,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626477/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Huyu ni kiranja wangu na nitafurahi sana akinipatia hiyo taarifa."
},
{
"id": 1626478,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626478/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Veronica Maina",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": " Proceed, Senator Sifuna."
},
{
"id": 1626479,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626479/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sifuna",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ndugu yangu, Mhe. Mwaruma, nimekusikiza kweli ukizungumza hapa na hata mwenzangu, Mhe. Ledama Olekina – tunapata huzuni sana lakini tunashangaa maanake ripoti zipo kwamba baadhi ya viongozi wakuu katika taifa hili la Kenya, ni wakaazi wa Taita Taveta. Hivi ni kusema hawana habari ya dhila hizi zote ambazo mnazipitia? Hilo tu ndilo swali nilikuwa ninataka nimjulishe kwamba mkaazi mmoja wa Taita Taveta ni kiongozi mkuu wa taifa hili. Kwa hivyo, sielewi kama Mkenya, mambo haya yanawezaje kuendelea ilhali una wadosi pale. Labda atuelezee shida iko wapi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1626480,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626480/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Asante Seneta wa Nairobi, Sen. Sifuna, kwa hiyo taarifa uliyonipa. Ni kweli kwamba wakuu wengi wa nchi hii wako huko lakini yale maendeleo ukiangalia pale wako ni kweli maendeleo yanatokea. Kwa mfano, kuna barabara mbili kubwa sana ambazo zimetengenezwa. Zimetumia mabilioni ya pesa, ya kuelekea shambani ya hawa wakubwa lakini huko kwingine tumeachwa nyuma. Sina haja kusema maanake tukienda huko leo, utaona kwamba zile barabara kubwa zinaelekea kwa hawa wakubwa ambao unasema."
},
{
"id": 1626481,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626481/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi Spika wa Muda, ninaomba niachie hapo. Kamati ya Fedha na Bajeti watuangalie wakati wa sera ya tatu ya kugawanya pesa hizi."
}
]
}