HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=160830",
"previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=160828",
"results": [
{
"id": 1626482,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626482/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi Spika wa Muda."
},
{
"id": 1626483,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626483/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Veronica Maina",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": " Thank you, Sen. Mwaruma."
},
{
"id": 1626484,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626484/?format=api",
"text_counter": 160,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Veronica Maina",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": "Sen. David Wakoli Wafula, proceed."
},
{
"id": 1626485,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626485/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia na vile vile kupongeza mapendekezo ya usawazishaji wa raslimali katika nchi ya Kenya."
},
{
"id": 1626486,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626486/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nimewasikiza kwa makini sana baadhi ya viongozi wenzangu ambao wana hisia kwamba fedha ambazo mtoza ushuru anatoa, ni Lazima ziende tu maeneo yao pekee. Sisi ni kuangalia kupitia televisheni. Ni vyema waelewe kwamba japo kuna maeneo ambayo yalipata nafasi ya kupata mandeleo wakati ya awamu ya kwanza ya Serikali, kuna maeneo ambayo vile vile hayajapata maendeleo kwa muda huo. Ni Lazima tunapotathmini jinsi fedha hizi zinavyopeanwa, tuzingatie maeneo kama hayo."
},
{
"id": 1626487,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626487/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninasimama hapa kwa sababu Kaunti ya Bungoma kwa muda imekuwa kwa upinzani – siku za Mhe. Raisi Toroitich Arap Moi. Serikali zilizofuata, chini ya Mhe. Muigai Uhuru Kenyatta, tulikuwa katika upinzani. Ukiangalia jinsi fedha zilikuwa zinatolewa kupitia hazina kuu ya Serikali, wakati huo hatukuwa na cha kujivunia katika Serikali."
},
{
"id": 1626488,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626488/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninaamini kwamba ni haki Bungoma ipate fedha hizi kwa sababu eneo Bunge la Mlima Elgon na maeneo Bunge ambayo yanapakana na Mlima Elgon, kihistoria na kimaendeleo yalikuwa yamewachwa nyuma. Ni lazima wanapoweka fedha katika bajeti na jinsi nimeshukuru Kamati - mmenukuu eneo la Mlima Elgon - Lazima wajue kwamba miundo mbinu ambayo imo katika Mlima Elgon sio nzuri: Afya, Barabara, maji na kadhalika."
},
{
"id": 1626489,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626489/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninaomba mheshimiwa yeyote anaponyanyuka kutoa hoja, ajue kwamba Mkenya yeyote popote alipo anaposikiza, lazima tumpe moyo na sababu ya kujivunia kuwa Mkenya, japo fedha hazitoshi, lakini waone kuna jambo nzuri linatendeka katika Serikali ya Kenya. Lisilokuhusu, usiliandame. Sisi watu wa Bungoma tunashukuru kidogo tumepata lakini tunasema tunahitaji fedha zaidi. Wanapogawa muda mwingine, tunataka ipande kutoka Shilingi 95 milioni ije kama bilioni, jinsi kaunti zingine zinapata. Hii ni kwa sababu ukiangalia mgao wa fedha, jinsi tulivyopitisha hapo awali, baadhi ya kaunti ambazo zinapata fedha nyingi hata sasa, katika bajeti bado wanapata fedha nyingi na kwa muda mrefu wamekuwa wanapata hizi fedha. Lazima tufuatilie tujue, miradi gani inatekelezwa na serikali za kaunti; wanahusisha wananchi katika utekelezaji wa miradi na iwapo miradi hii inaafiki matarajio ya wapiga kura ama wanaoishi katika maeneo haya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1626490,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626490/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninapoangalia Kaunti ya Busia ambayo ni jirani yetu kule, wamepewa Shilingi 29 milioni. Hizi pesa hazijakuja kimzaha. Kuna sababu ambayo imeshinikiza Serikali kuweka fedha katika Kaunti ya Busia. Haimaanishi kwamba Busia ilipokuwa na Naibu wa Rais na Mawaziri ama walipokuwa na Mhe. Amos Wako katika Serikali watu wa Busia walikuwa katika shamba la asali na nyama. Haiwezekani. Kuna changamoto watu hawa walikuwa nazo ndiposa fedha zimewekwa kwa bajeti vile vile kama Wakenya waweze kuimarisha maisha yao. Nashukuru wameweka Kaunti ya Trans Nzoia hapa. Wamepewa Shilingi 12 milioni japo kuna viongozi huko hawashukuru kwa chochote. Wanabwata tu, wanaongea tu. Lazima tutafuata tujue hizi fedha zinazoenda Trans Nzoia zinatumika kivipi katika eneo Bunge la Endebbes. Lazima tutawaeleza watu katika eneo Bunge hili na Trans Nzoia fedha za usawazishaji zinatumika vipi ili wajue kuwa Seneti linawajali; japo kuna wale wanapinga na kutusi Serikali na wakututusi sisi Maseneta, tutawapa pesa lakini tutafuata kuhakikisha hizo pesa zinafanya kazi. Zaidi ya hapo, wanakandarasi wanaofanya hizo kazi lazima watoke katika kaunti husika. Hii ni kwa sababu Haiwezekani Seneti tunapitisha fedha kama hizi na wale wanakandarasi ni watalii wa kibiashara. Wanatoka Nairobi na kaunti zingine kufanya kazi ambayo wananchi wa kaunti husika wanaweza kufanya."
},
{
"id": 1626491,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626491/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninaunga mkono kaunti hizi ambazo zimeorodheshwa hapa. Wale waliopewa pesa kidogo waongezewe, kama ndugu yangu wa Taita Taveta. Ana haki ya kudai pesa ziongezwe. Wale ambao wamekuwa wanapewa pesa nyingi na hatuoni matunda, wapunguziwe kwa sababu huenda hizi pesa zinaenda katika mifuko ya watu wachache ilhali wengi wanaumia. Hawana maji, barabara au madawa hospitalini. Hatuwezi kukubali mambo kama haya katika awamu hii ya Serikali."
}
]
}