Abdulswamad Sheriff Nassir

Parties & Coalitions

Post

PO BOX 16735, Mombasa, Kenya

Email

asnassir@radiorahma.co.ke

Link

Facebook

Telephone

0722333109

Telephone

0737333109

Link

@Asnassir on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 291 to 300 of 1018.

  • 5 Aug 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Bila shaka, kama Mbunge mkongwe. Nilikuwa nasema tu yakuwa Kamati iliendeshwa bila msukosuko wowote wa kisiasa. Nataka tu kuzungumza kwa uchache kwa sababu nataka wenzangu wazungumze natukamilishe ili iwe sheria leo. Leo hii tukiweza kumaliza, iwe sheria. Mashirika ambayo tumeweka katika Ripoti hii ni 48. Naisihi National Land Commission (NLC), kamisheni ambayo iliwekwa katika Katiba, kuhakikisha kwamba mambo ya ardhi yametatuliwa kisawasawa. Itoe title deed kwa haya mashirika ya Serikali hususa yale ambayo yamenyakuliwa na mabepari. Ardhi lazima irejeshwe ili iwafae Wakenya wote. Pia kuna mashirika ambayo yalikuwa yanateta bila kuelewana yanadaiana. Tumetoa ... view
  • 5 Aug 2020 in National Assembly: tutaweza kutoa uamuzi, kama Kamati, iwapo ni kweli vyombo vya habari vimezua au kulikuwa na ukweli fulani katika masuala yale. Nikimalizia, kuna jambo lingine ambalo mashirika yanaweza kuchezea. Ni hili jambo la riba, interest. Unapeana kandarasi kwa mtu, unaamua kutomlipa yule mtu kwa muda unaofaa. Ndani ya hii Ripoti kuna wale ambao tuna waambia “Ikiwa watu watadai riba kwa njia yoyote, ni lazima Board of Directors na management wapelekwe mbele na kusema ni kwa nini wanalipa riba.” Ukisoma hii Ripoti, mabilioni ya pesa, sio mamilioni, ambayo yangeweza Kulipa madeni ya nchi hii yanalipwa kwa wanakandarasi kwa sababu ya riba. Kisa ... view
  • 2 Jul 2020 in National Assembly: Hon. Speaker, I beg to lay the following Paper on the Table of the House today Thursday, 2nd July 2020. The 23rd Report of PIC on its consideration of the Auditor-General’s Report on Financial Statement of State Corporations. view
  • 2 Jul 2020 in National Assembly: Hon. Speaker, I beg to give notice of the following Motion: view
  • 2 Jul 2020 in National Assembly: THAT, this House adopts the 23rd Report of the PIC on its consideration of the Auditor-General’s Report on Financial Statement of State Corporations laid on the Table of the House on Thursday, 2nd July, 2020. view
  • 2 Jul 2020 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Spika. Nitatumia lugha ya taifa, Kiswahili. Wiki iliyopita, tulikubaliana na ukatoa amri kuwa Kamati ya Uchukuzi iweze kukaa na tukaweza kukaa jana na tukaafikiana vile mwenzangu alivyozungumza kwa Kiingereza kuwa amri ya kusafirishwa kwa mizigo na makasha yanayopelekwa nchi jirani kutumia SGR, kama ilivyokuwa amri ya kwanza ya kupeleka mizigo mpaka Nairobi, haipo tena. Wameiondoa amri hiyo. Huu si ushindi wa upizani bali ni ushindi wa hekima ya kutumia sheria vile inavyotakikana. Pili, kwa sababu Bunge hili hutengeza miswada na sheria, nawaomba Wakurugenzi wa Shirika la Reli nchini, wale wa Halmashauri ya Bandari ya Kenya, na wale ... view
  • 25 Jun 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika. Kupitia Kanuni za Kudumu Nambari 44(2)(c), naomba kuuliza na kusisitiza tena kupitia Kamati ya Uchukuzi, Kazi za Umma na Nyumba kuhusu ulazimishaji wa kusafirisha mizigo kupitia reli maarufu Standard Gauge Railway (SGR). Tarehe 2 Juni, 2020, nilileta ombi hili kuhusu ulazimishaji wa kusafirisha mizigo kutumia SGR. Ilipofika tarehe 16 Juni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi, Kazi za Umma na Nyumba akaleta Ripoti ambayo inatofauti kubwa na vile hali ilivyo mashinani. Alisema huu ni mpangilio wa Marais wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ya tarehe 12 May, 2020. Alisema kwamba mizigo yote ya nchi za nje ... view
  • 25 Jun 2020 in National Assembly: Mhe. Spika, katika Jumba hili, kama kuna watu ambao wanajulikana kwa hekima zao, wewe ni mmoja wao na utaingia kwenye kumbukumbu za historia kwa sababu ya hekima ambayo umeweza kuitumia hususa hivi sasa. Mmeweza kueleza lugha ya kisheria. Ningetaka tuzungumze lugha ya mtaani. Mpuuzi mpe sifa. Baadaya yote yale, hili Jumba ni Jumba ambalo rekodi zote zinawekwa. Inajulikana wazi ni nani anayeleta masuala yakutetea watu zaidi ya yeyote mwingine. Historia ipo katika Hansard iliyo hapa. Inajulikana wazi ni nani. Lakini leo, nakumbuka maneno ya marehemu Mzee wangu akiniambia usihofie…Nakumbuka kauli ya kuwa pale unapoona ya kuwa ghafla, mawe yanaanza kutupwa ... view
  • 18 Jun 2020 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika. Kwanza natoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti kwa kuelezea. Pili, asiyeweza kumshukuru binadamu hamshukuru Mwenyezi Mungu. Vijana 3,500 kutoka Mvita ni asilimia 11 ya vijana wote walioajiriwa katika Kenya hii. Vijana waliochukuliwa ni 31,448. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 18 Jun 2020 in National Assembly: Vijana hawakuwa wamelipwa siku nilipouliza hili Swali. Baada ya kuliuliza, vijana walilipwa. Nakubaliana na Mwenyekiti kuwa kuna vijana wamechukua mikopo ya Fuliza. Wengine wameweka majina ya girlfriends wao au waume wao. Hayo yametokea lakini tumefanya kikao na Assistant County Commissioner wa Mombasa na machifu. Tunajaribu kuyatatua kimjini. Hata hivyo, nina jambo kuhusu hili suala la vyombo na vifaa ambavyo walikuwa wapewe. Kwanza, kuna karatasi ambayo nimechukua kutoka Room 8 ama Table Office yetu ya Bunge. Ile karatasi inazungumza tofauti na alivyozungumza Mwenyekiti. Hii karatasi inaeleza wazi kuwa hawajatoa vifaa vyovyote. Ile Statement ambayo imesomwa na Mwenyekiti ni kuwa vifaa vimetolewa. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus