23 Apr 2015 in National Assembly:
Mwaka uliopita, nilizuru viwanda ambavyo vinasafisha na kuweka samaki katika mikebe. Nilisikitika kuona kuwa idadi ya watu waliokuwa wameajiriwa kwenye kiwanda hicho ilikuwa ni ndogo sana, na hali Wakenya huenda kwenye nchi kama vile Ushelisheli ili kupata ajira katika sekta ya uvuaji samaki. Sababu kuu ni kwamba nchi nyingine zimeweka sheria kuhusu uvuaji wa samaki. Uvuaji wa samaki ni shughuli ambayo huziletea nchi nyingi ulimwenguni dola kwa mabilioni. Jambo la kusikitisha ni kwamba, katika nchi hii, mwenye meli yake anaweza kuingia na akiweza kulipa dola elfu hamsini, anaweza kuvua samaki wanaoweza kujaa meli yake. Wengine huvua mpaka meli zao zikafikia ...
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumshukuru mwenzetu Mhe. Wangamati kwa kuileta Hoja hii katika Bunge. Ningetaka kuipeleka Kenya katika mwaka 1913 ambapo katika maeneo ya Pwani, kulikuwa na mwanamke wa Kigiriama aliyejulikana kama Mekatilili wa Menza aliyekataa mila, desturi, uonevu na unyanyasaji wa Uingereza. Alikataa maonevu ya kiuchumi. Wakoloni walikuwa wakiweka kila aina ya ushuru katika biashara zao na kuathiri maswala mengi yakiwemo kulipa ushuru kwa kila nyumba almaarufu ikijulikana kama Hut Tax. Katika mwaka huu wa 1913, Mekatilili wa Menza, pamoja na mwenzake, Wanje wa Moderikola, walishikwa na kupelekwa hadi sehemu ya Mumias. Baada ya miezi, ...
view
18 Feb 2015 in National Assembly:
On a point order, hon. Speaker. We are aware that our colleagues voted twice and it is very evident. We would like to know the names of those who voted twice.
view
12 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusema kwamba sauti ya Bunge hili ni sauti ya Wakenya. Rai yangu kwa wakuu wa elimu ni kwamba wazibebe sauti zetu wakijua kwanba wamebeba maoni ya Wakenya na sauti ya kila mmoja alioko hapa ambaye amezungumza kwa bughutha kuhusu hali ya elimu ilivyo; hususan, masuala ya karo katika shule za upili. Serikali ilikaa na ikatengeneza Ripoti ambayo ilipeana. Ripoti ya Jopo lililoongozwa na Kilemi Mwiria iliandika kwa umakinifu kwamba: Kama sekta ya elimu nchini ingepewa Kshs11 bilioni, basi kila asomaye katika shule ya upili atasoma bure, isipokuwa wale wasomao katika shule za ...
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika. Kwa niaba ya watu wa Mvita, ningetaka kuchukua fursa hii kutoa pole na risala za rambirambi kwa familia ya Mhe. Muchai pamoja na wale askari na dereva wake. Kuna kitu ambacho ningependa kutaja. Wenzetu ambao wameinuka wamesema kuwa kuna haja ya askari wa Wabunge kuongezwa na kupatiwa vifaa zaidi. Lakini kando na kujifikiria na kutufikiria sisi, tunafaa kuchua fursa na kuweka mbele maswala mawili. La kwanza, ni kuuliza ikiwa zile kamera ambazo zimetumia thamani kubwa ya pesa za wakenya zimetumika kwa njia inayofaa. La pili, ni lazima sisi kama Wabunge tukubaliane na tuhakikishe tumepitisha Miswada kuhakikisha ...
view
13 Nov 2014 in National Assembly:
Thank you hon. Temporary Deputy Chairman.
view
13 Nov 2014 in National Assembly:
Actually, hon. Temporary Deputy Chairman, the reason why I had put it is because I was hoping that we shall have finalised on that particular question and it was for the upcoming statement.
view
12 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie Mswada huu ambao umeletwa mbele ya Bunge hili. Ningependa kutoa mifano ya vipengele na maelezo yake ambayo yamenifurahisha katika Mswada huu na sababu za umuhimu wake katika Kenya hii ya leo. Kwanza, kipengele cha tano kinazungumzia uaminifu, uadilifu, uwasi na ufuataji wa sheria ambao unastahilika kwa kila mfanyakazi wa umma. Kipengele cha tisa kinaelezea uwazi kuwa kila mmoja atahukumiwa kulingana na vile ambavyo atakavyokuwa amefanya yeye mwenyewe. Mtu hatakuwa na sababu ya kusema kuwa alifanya vile alivyofanya kwa sababu aliambiwa na mkubwa wake ama alifanya vile alivyofanya kwa ...
view
12 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie Mswada huu ambao umeletwa mbele ya Bunge hili. Ningependa kutoa mifano ya vipengele na maelezo yake ambayo yamenifurahisha katika Mswada huu na sababu za umuhimu wake katika Kenya hii ya leo. Kwanza, kipengele cha tano kinazungumzia uaminifu, uadilifu, uwasi na ufuataji wa sheria ambao unastahilika kwa kila mfanyakazi wa umma. Kipengele cha tisa kinaelezea uwazi kuwa kila mmoja atahukumiwa kulingana na vile ambavyo atakavyokuwa amefanya yeye mwenyewe. Mtu hatakuwa na sababu ya kusema kuwa alifanya vile alivyofanya kwa sababu aliambiwa na mkubwa wake ama alifanya vile alivyofanya kwa ...
view
12 Nov 2014 in National Assembly:
lililowekwa. Swali tunalouliza; ni lini matumbo ya mama zetu yakawa hayawezi kutoa watu wanaostahili kushika nyadhifa katika sekta hii?
view