All parliamentary appearances
Entries 31 to 40 of 81.
-
15 May 2014 in Senate:
Madeni tuliyoyarithi kutoka kwa County Council ni Kshs1.3 billion. Pesa zitakazobaki ni ngapi? Tutabaki na Kshs400 milioni. Pesa hizi zitachukuliwa na Serikali ya kaunti. Waheshimiwa Bunge wa Kaunti watatumia pesa hizi kufanya kazi yao. Bw. Naibu Spika, miaka 50 sasa, Kaunti ya Lamu imebaguliwa kwa njia zote. Hatuna hata barabara hata kilomita moja ya lami. Nimewaona marais watatu. Nilimwambia Rais mstaafu baba Moi kuwa Lamu inahitajika barabara ya lami ilituweze kujivunie kama kaunti zingine lakini hakufanya hivyo kwa muda wa miaka kumi. Pia tumezungumza na Rais Kibaki kwa miaka kumi tuliyokuwa naye, tukizunguza siku ingia, siku toka, lakini hakuna barabara ...
view
-
15 May 2014 in Senate:
Bw. Naibu Spika, sikio la kufa halina dawa. Hivi sasa, tuko na Katiba mpya inayotupa haki ya kupata pesa sawa katika kaunti zote. Huo ndio wajibu mkubwa wa Bunge hili la Seneti. Lakini kwa miaka hii yote miwili iliyopita, Bunge hili haliwezi kujivunia ya kwamba wametupa pesa za kutosha katika kaunti yetu. Tumeletewa yale makadirio ya kwanza na yakapita; tukafanya mapendekezo ya Seneti yakapuuzwa na mapendekezo ya watu wengine yakachukuliwa. Hivi sasa, tunaulizwa kupitisha Kshs226 bilioni. Hata mimi ninaunga mkono Mswada huu huko kama nimefunga jicho moja.
view
-
15 May 2014 in Senate:
Lakini haya mambo yanayofanyika si haki. Mimi naiomba Seneti hii pamoja na ile Tume ya Cheserem waangalie ile mbinu ya kugawa pesa katika kaunti. Haiwezekani kuwa Lamu inapata pesa za chini ilhali najua kuwa Lamu ina watu masikini kushinda sehemu nyingi zote nchini. Watu wa Nairobi wakienda huko, huwa wanaenda katika kijiji cha Amu peke yake. Hawajui ya kwamba wapo watu wanaoishi katika kilomita 300 katika Kaunti ya Lamu ambao siku zingine hawawezi kupata chakula cha hata mara moja kwa siku.
view
-
15 May 2014 in Senate:
Hakuna haja kwa sababu si chama. Sisi tunawafuasi wa chama cha Jubilee na pia watu wa CORD walikuwako katika Serikali iliyopita ya nusu mkate. Hata hivyo hawakuweza kufanya Serikali ile ifanye kitu kama hicho. Hivi sasa, tunaendelea kubaguliwa na kudunishwa kwa kupatiwa pesa chache sana. Tutafurahi tu wakati tutapata haki zetu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
-
15 May 2014 in Senate:
Kwa hivyo, naiomba Seneti hii isimame kidete na Kaunti ya Lamu mwaka ujao ili tuweze kwa na mradi mingi ya maendeleo. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga Mswada huu mkono.
view
-
17 Apr 2014 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I have a Statement here with me. We received it today and we went through it with the other Members of the Committee. We have noted that this Statement is not adequate. I have also consulted with the distinguished Sen. (Prof.) Lesan and we have written back to the Cabinet Secretary to furnish us with an adequate answer. We have agreed to postpone issuing it to a later date.
view
-
17 Apr 2014 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, this was about Compensation on the Standard Gauge Railway.
view
-
17 Apr 2014 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, it was sought by Sen. (Prof.) Lesan.
view
-
17 Apr 2014 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, the question is very adequate. We will take it seriously to seek the clarification and everything that the Senator has requested. This will be done after the recess.
view
-
17 Apr 2014 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, either the first or second week after we resume.
view